Kuna athari zozote kama tukivunja uhusiano na WB,IMF au Marekani?

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,457
2,000
Hivi kuna jambo lolote baya litatokea kama Tanzania tukiamua kuvunja uhusiano na Shirika la fedha Ulimwenguni (IMF), Benki ya Dunia (WB), au nchi ya Marekani? Badala ya mjadala wa kuendelea ama kutokuendelea kuwa na uhusiano na taasisi hizo ama nchi ya Marekani kwa nini kama taifa tusiamue uhusiano ufe?

Maana ni kama kila wakati inakuwa ni mjadala wa nani kibaraka ama mzalendo kuelekea taasisi hizo na nchi ya Marekani. Hivi kuna ulazima wa kuwa na Mahusiano nao?

Ni wakati wa kusimama na kutembea kwa miguu yetu wenyewe!!
 

Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
13,102
2,000
hakuna nchi imewahi kuvunja uhusiano na WB na IMF, kuhusu Marekani athari yake ni tutakosa misaada lakini kuvunja uhusiano nao inawezekana mfano Zaire ilivunja uhusiano na Marekani kwa sababu Marekani ilishiriki jaribio la kumpindua Rais na ikavunja uhusiano na Belgium kwa sababu kuna mwandishi wa ki belgiji aliandika kitabu cha kumkashifu rais
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
11,105
2,000
Kwani kuvunja siyo msimamo?? Tuvunje tu kila mtu akae kwake!!
Yes tuvunje hata leo. But can we live without them?
Tunaweza jitegemea ?
For the record bado tunapokea misaada yao.
My point is tuvunje pale ambapo misaada yao ilikuwa inasaidiwa tuwe na uwezo wa kuendesha bila misaada yao.
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,709
2,000
Duh! Kazi ipo. Na hayo madeni yote wanayokudai utayalipaje?

Leo wadau wakichomoa hata waya wa SWIFT kwa mabenki yetu, kesho tu tutakuwa tunataftana.

Hivi unajua hata benki yako CRDB imekuwa inaendeshwa kwa ufadhili na msaada mkubwa wa nani?
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
4,533
2,000
Kuvunja inawezekana lakini je tunaweza kutoboa?

Huko nyuma Mwl.Nyerere Nyerere aliwahi kuvunja uhusiano na Marekani sababu ya Rhodesia enzi za Mlowezi Ian Smith lakini haikuleta mabadiriko yoyote kwa USA haikubadirisha sera yake juu Rhodesia. Akarudisha baada ya muda mfupi.

Ila nakumbuka huyo Raisi Dr.Mwl.Julius Nyerere aliingia mgogoro na IMF, na Word Bank lakini hakuvunja.

Sababu wao ndio guarantee au ni reference ya sisi kukopa hata mabenki ya nchi nyingine.

Mara nyingi wamebadirisha madeni yetu kuwa misaada au wamefuta madeni yetu kabisa.
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
24,596
2,000
Yes tuvunje hata leo. But can we live without them?
Tunaweza jitegemea ?
For the record bado tunapokea misaada yao.
My point is tuvunje pale ambapo misaada yao ilikuwa inasaidiwa tuwe na uwezo wa kuendesha bila misaada yao.
Hivi bado bajeti yetu inawategemea wao kwa 40%?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom