Kuna athari gani za kiusalama kupiga picha kwenye pantoni Feri?

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
482
1,053
Naomba kujuzwa athari za kiusalama za kupiga picha ya smartphone ndani ya pantoni tena ukijipiga au kumpiga mtu. Maana yake ukipiga, unakamatwa na kuna faini.
 
  • Thanks
Reactions: Eco
Athari za kiusalama sijui, labda waje wataalam waelezee. Ila mimi nakumbuka kuna siku nilibahatika kuingia bandarini nikataka kupiga picha meli ikiwa imetia nanga!

Pona yangu ni yule mwenyeji wangu alikuwa mzito kidogo nikasameheka. walidai maeneo hayo ni millitary zones hivyo picha haziruhusiwi.
 
Zamani nadhani ilikuwa na sababu ila kwa dunia ya sasa sidhani kama kuna sababu ya msingi...
Ni kweli. Hizi ni sababu za ile miaka ya zamani kabisa kipindi ambacho technolojia ipo chini sana. Dunia ya sasa kuna satelite na vyombo kibao vinavyoweza kupiga picha nzuri kabisa hata rais akiwa uani kwake. Ila sehemu kama Muhimbili wanakataza ili kuficha baadhi ya mambo ambayo hayako sawa. NB: Sehemu kama hospital wodini, emergency area na maeneo mengine hata mimi naunga mkono wakataze kupiga picha kwani tangu kila mtu awe na kamera kuna ulimbukeni wa kupiga picha kwa matukio yanayohotaji privacy.
 
Itakuwa pia ni njia ya kuepuka lawama iwapo chombo kitapata ajali halafu ibainike kwamba chanzo ilikuwa ni uzembe wa TEMESA kwa kubeba abiria kuliko capacity ya chombo. Overloading bado imekuwa ni kizungumkuti katika sekta ya usafirishaji abiria katika nchi hii.
Kumbe
 
Back
Top Bottom