Kuna athari gani kukua kwa haraka?

Omuregi Wasu

JF-Expert Member
May 21, 2009
749
148
Ninaomba msaada wenu maana mtoto wangu ameongezeka urefu wa sentimeta 4 na uzito wa kilo mbili ndani ya mwezi mmoja.

Alipoenda kliniki jana baada ya vipimo hata daktari alishituka lakini ni daktari huyo huyo aliyenishauri nimpe mtoto vitu vifuatvyo mwezi uliopita (consultation ya Octoba):

1. Anatumia maziwa ya Dumex (sasa hivi kwa umri wake anatumia serial 3). Hakuwahi kunyonya maziwa ya mama yake tangu amezaliwa.

2. Anatumia yai moja la kuku na mawili ya ndege aina ya Tombo au Quail (kiingereza) kila siku majira ya saa nne.

3. Anatumia vitamin Fe,Zn,Ca kiasi cha 10 g kila siku. Mchanganyiko huu wa vitamini unaitwa (her yao pian) sijui kiingreza wala kiswahili chake.

4. Anatumia matunda hasa madrasini, zabibu n.k

5. Anakunywa juice za aina mbalimbali za viwandani

6. Anapenda sana kula tambi za watoto

Daktari alishtuka lakini baada ya kumbana akasema ni sawa tu ila tumpunguzie vitu vya sukari na baada ya wiki 2 tukapime mchanganyiko wa madini kwenye damu yake.

Je, hili ongezeko lina madhara kwa mtoto wa miaka 2.
 
Ninaomba msaada wenu maana mtoto wangu ameongezeka urefu wa sentimeta 4 na uzito wa kilo mbili ndani ya mwezi mmoja. Alipoenda kliniki jana baada ya vipimo hata daktari alishituka lakini ni daktari huyo huyo aliyenishauri nimpe mtoto vitu vifuatvyo mwezi uliopita (consultation ya Octoba):
1. Anatumia maziwa ya Dumex (sasa hivi kwa umri wake anatumia serial 3). Hakuwahi kunyonya maziwa ya mama yake tangu amezaliwa.
2. Anatumia yai moja la kuku na mawili ya ndege aina ya Tombo au Quail (kiingereza) kila siku majira ya saa nne.
3. Anatumia vitamin Fe,Zn,Ca kiasi cha 10 g kila siku. Mchanganyiko huu wa vitamini unaitwa (her yao pian) sijui kiingreza wala kiswahili chake.
4. Anatumia matunda hasa madrasini, zabibu n.k
5. Anakunywa juice za aina mbalimbali za viwandani
6. Anapenda sana kula tambi za watoto

Daktari alishtuka lakini baada ya kumbana akasema ni sawa tu ila tumpunguzie vitu vya sukari na baada ya wiki 2 tukapime mchanganyiko wa madini kwenye damu yake.

Je, hili ongezeko lina madhara kwa mtoto wa miaka 2.

Wakati JF Dokta akisubiriwa, naomba ufafanue sehemu za / sentensi zilikolezwa wekundu na weusi.

Natanguliza shukrani.
 
Wakati JF Dokta akisubiriwa, naomba ufafanue sehemu za / sentensi zilikolezwa wekundu na weusi.

Natanguliza shukrani.
Umetaka nitoe ufafanuzi'
1. Hiyo vitamini hiko kwenye kimiminika na inaitwa 哈药牌 baada ya kumkuta mtoto anaupungufu wa vitamini Ca,Fe na Zn (consultation ya oktoba) daktari akashauri apewe hizo dawa na amezitumia kwa kipindi cha mwezi mzima. Ni vitamin tu kama ilivyo vitamin B n.k
2.Mtoto anatumia juice za watoto. Ni juice maalum kwa ajiri ya watoto kama wahaha, grape juice, xiaoji liang, xijilang n.k
Amekuwa akitumia hizi juice kama miezi sita iliyopita lakini hajawahi kuongezeka urefu kiasi hicho ndani ya muda wa mwezi mmoja.
 
Am lost hapa, hata sijaelewa hii diet ya mtoto wako! sikui uko china ama japan ama korea? just joking!
 
Apart from urefu umecheki na weight yake pia? Mie binafsi nipo nchi za magharibi na Dr kanikataza kabisa kumpa mtoto juice amesema maji na maziwa vinatosha.

Sababu kuu hasa ni kwamba juice inaacha sukari kwenye gums ambazo zitakuwa na madhara. Pia nisisahau kukwambia kwamba kwa ushauri wa Dr mtoto wangu haruhusiwi kula kitu chenye chumvi wala sukari.
 
Kwanza kabisa inabidi utueleze umri wa mtoto, alizaliwa na uzito gani, uzito huo umeongezeka kwa vipindi vya muda gani.

Kuhusu kuongezeka urefu hilo ni jambo la kawaida kwani anakuwa, lakini pia tueleze amekuwa anaongezeka kwa kasi na kiasi gani.

Tatizo la uzito ambalo [sitalihusisha na mtoto wako mpaka nipate majibu ya maswali] ni kuwa, uzito unaweza kumchelesha kufikia hatua fulani [milestones].

Uzito pia unaweza ku kuchagiza hali zilizojificha za kibinadamu kujitokeza mapema. Kwa mfano kama mtoto ana vnasaba[Genes] za kuritihi kutoka kwa wazazi kwa ugonjwa kama diabetes basi hali hiyo inaweza kuanza kumtokea mtoto mapema zaidi.

Vitamini na minerals ni nzuri lakini kumbuka kila kitu kina kadiri yake [anything too much is harmful].
Kwa maelezo yako ni vema umpe mtoto juice asili kwani za viwandani zinamichanganyiko ya vitu vingi[chemical] hata kama ni za matunda halisi.

Hii inatokana na processing[utayarishaji] ambao huhusisha ongezeko la kemikali.

Kwa faida ya wasomaji mtoto huzaliwa kwa uzito unaotegemea mambo mengi kwa mfano muda aliozaliwa.

Kama ni njiti uwezekano wa kuwa na uzito mdogo ni mkubwa. Uzito hutegemea pia maumbile ya wazazi ingawa kinyume chake pia chaweza kutokea. Inategemea mzazi alikuwa anahuduiwa vipi kilishe kabla ya uzazi. Kitaalamu uzito wa kilo 2.5- 3.5 ni ideal [wakufirika] ndio wa kuzaliwa nao. Inatakiwa katika umri wa miezi sita mtoto awe na uzito mara mbili ya ule aliozaliwa nao, na baada ya hapo kuna ongezeko la kiasi.

Ikumbukwe kuwa hii inategemea pia lishe na maradhi. Isieleweke kuwa hiyo ni formula bali ni muongozo [standard] unaotumika.

Hadi hapo tutakapopata majibu ya maswali ya msingi tunatarajia utakuwa umepata mwanga.
 
Back
Top Bottom