Kuna anayejua Marekani imefanya nini nchini Afghanistan?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
996
1,016
VCG111343849737.jpg

VCG111343921535.jpg

VCG111343920027.jpg
Hivi karibuni dunia imeshangazwa baada ya kusikia Rais Ashraf Ghan wa Afghanistan amekimbia mji mkuu wa nchi hiyo Kabul, baada ya mji huo kuzingirwa na wapiganaji wa kundi la Taliban. Kukimbia Kabul kwa Rais Ghani kuna maana kuwa ni wazi kuwa kundi la Taliban sasa limetwaa madaraka ya uongozi wa Afghanistan.

Katika muda wa miaka 20 iliyopita tangu Septemba 11 2001, kundi la Taliban lilitangazwa kuwa adui mkubwa baada ya Marekani kusema kundi hilo lilikuwa mwenyeji wa kundi la Al-Qaeda lililofanya shambulizi la Septemba 11. Na katika muda wote huo Marekani imetumia pesa nyingi kuongoza majeshi ya NATO kufanya mashambulizi mara kwa mara kulenga wapiganaji wa kundi la Taliban, na kuaminisha dunia kuwa kutokana na uwezo mkubwa wa kundi la NATO, kundi la Taliban limetokomezwa, na utaratibu wa kidemokrasia umeanzishwa nchini Afghanistan.

Mara kwa mara jumuiya ya kimataifa, hasa nchi jirani na Afghanistan, zilikuwa zikipaza sauti kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwenye mgogoro wa Afghanistan. Na wanaoifahamu vizuri historia ya Afghanistan na siasa zake, pia walisema mara kwa mara kuwa mgogoro wa Afghanistan utatatuliwa kwa njia ya mazungumzo na mchakato wa kisiasa unaoshirikisha watu wa Afghanistan, lakini sauti hizo zote zilipuuzwa.

Bahati mbaya ni kuwa Marekani iliendelea kusisitiza suluhisho la kijeshi, na kutumia pesa nyingi kuweka vituo vya kijeshi na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Afghanistan, mashambulizi ambayo sio tu yalisababisha vifo vya wenyeji wengi bali pia vya wanajeshi wa Marekani na wa nchi za magharibi. Mchakato wa kisiasa iliotetea Marekani, ulikuwa ni ule uliolenga kuiweka madarakani serikali inayoitaka, na sio ile iliyochaguliwa na watu wa Afghanistan.

Pamoja na kuwa baadhi ya watu wameonyesha kushangazwa na uamuzi wa serikali ya Joe Biden kuondoa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, ukweli ni kuwa nia hiyo ilikuwepo tangu wakati wa serikali ya Barack Obama na hata wakati wa serikali ya Rais Donald Trump. Ile kauli ya muda mrefu ya kuwa kamwe Marekani haiwezi kufanya majadiliano na kundi la kigaidi, ilipuuzwa na serikali ya Donald Trump ilianza kufanya mazungumzo na kundi la Taliban. Hili lilianza kuleta maswali kuhusu msimamo na lengo hasa la Marekani.

Sababu ni kuwa Marekani ilitambua toka mwanzo kuwa uamuzi wa kutuma jeshi nchini Afghanistan ulikuwa na dosari nyingi, lakini kulikuwa na hofu aibu ya kuondoka bila kupata ushindi. Hata hivyo kuondoka kwa majeshi ya Marekani na kundi la Taliban kuingia Kabul kiulaini bila pingamizi lolote, kunaleta picha ya kuwa Taliban wameshinda na Marekani wameshindwa.

Hadi sasa watu zaidi ya watu laki 2.4 wameuawa nchini Afghanistan na katika baadhi ya maeneo ya Pakistan kutokana na mashambulizi ya NATO na Marekani, na hasara ya kiuchumi haielezeki. Wengi wangetarajia kuwa wapiganaji wa Taliban wameangamizwa, na nguvu yake kiuchumi imedhoofishwa, lakini hicho si kinachoonekana.

Baadhi ya wachambuzi wanafananisha kitendo cha Marekani kuondoa wafanyakazi wake kwenye ubalozi wa Marekani nchini Afghanistan, kilichotokea Saigon, Vietnam miaka 46 iliyopita, yaani kuondoka kwa aibu baada ya mwelekeo wa vita kutoeleweka. Nchini Vietnam hatimaye adui mkubwa aliyefanya Marekani ianzishe vita, aliibuka mshindi na kuwa mtawala hadi sasa. Kinachoonekana Afghanistan ni sawa na hicho, yaani waliotangazwa kuwa maadui hatimaye ndio washindi na baadaye kuunda serikali.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Anthony Blinken ametetea kuondoka kwa jeshi la Marekani, kwa kusema lengo la uwepo wa majeshi ya Marekani lilikuwa ni kupambana na kundi la Al-Qaeda. Lakini hajasema lolote kuhusu matokeo ya kuleta demokrasia nchini Afghanistan, au matokeo ya mchakato wa kulijengea uwezo jeshi la Afghanistan kulinda usalama wa Afghanistan.
 
Mbona mzee Joe Biden kajibu swali lako leo kuwa waafghanistan wasitegemee Marekani kutatua matatizo yao hasa ubadhilifu, uvivu na utegemezi? Nadhani hii pia ni taarifa kwa watawala wa kiarabu wanaotegemea ulinzi wa Marekani dhidi ya watu wao. Biden ametangaza sera mpya ya Marekani kuachana na ukoloni na ugaidi.

Isitoshe, Afghanistan haina mafuta wala gesi vilivyo endelevu ambavyo vingewafanya wezi hawa wa kimarekani kuendelea kukalia nchi hii kapuku na hafidhina. Baada ya majambazi na mabwana vita kama akina Hamid Karzai na Ghani kula pesa yake, Marekani imechoka. Waafghanistan na wengine ambao ni tegemezi kwa Marekani ni kama watoto, wakinya wanataka uwatawaze na kutupa mavi yao. Mambo sasa yanaanza kubadilika. Kimsingi, Marekani wamekula dili na magaidi wenzao wa Taleban na kuwatosa mabwana vita.
 
Marekani ni wazee wa kupuyanga. Ni mabingwa wa kulizua, halafu mwisho wa siku wanashindwa kulinywa.
 
Vita ambavyo Marekani anashinda ni vile vya kwenye sinema za Hollywood tu. Kansela wa ujerumani anasema makosa yalitumika siyo kwa ujerumani tu kwa wote walioshiriki vita hivyo akimaanisha Marekani na umoja wa kujihami Ulaya Magharibi (NATO). Hizi nchi kubwa zinaamini migogoro yoote itamalizwa kwa kutumia nguvu za kijeshi tu.

Nguvu saa nyengine hazitatui kitu hii ni aibu kubwa kwa Dunia miaka 20 ambayo wameitumia kuunda serikali ya demokrasia imeanguka ndani ya mwezi mmoja na sijui kama imefika mwezi.Marekani inabidi ilaumu ilipodondokea na isilaumu ilipojikwaa. Somalia waliondoka kwa aibu.

Vietnam ndiyo doa kubwa pia limebaki. Hawa Taleban nao wapo tu kimaslahi yao na nyuma yao kuna mataifa yanawafadhili.Adui wa adui yangu ni rafiki yangu.Wachina wanatumia fursa pamoja na urusi wawekeze sasa Afghanistan.
 
Tambua kitu kimoja.

Nchi za ukanda wa umoja wa ulaya ukiunganisha na Marekani haziwezi kukupa ufahari wakati hauna tija kwao.

Counseler wa Ujerumani ni mzandiki sana kwenye siasa za kimataifa, anapo ongea jambo siyo la kutoka kwenye vikao vyao vya ndani ila analichakachua kulileta kwenye media kuonekana walifanya makosa same as marekani now.

Wameshaona hakuna faida Afghanistan so wameamua kuwapa makavu raia na viongozi wao kuwa there's no more kula vya bure wakati hawana kitu

Ngoja tuone WATAKAVYO UPIGA MWINGI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom