Raymond2n2
New Member
- Apr 18, 2016
- 1
- 0
GoodHeshima kwenu viongozi
Nimeona ni vyema na sisi wenye lengo la kuacha kazi tukawa na uzi wetu kama wenye agenda nyingine walivyoanzisha uwanja wao.
Lengo la nyuzi hii ni kupeana mawazo, moyo na uzoefu wa mbinu bora tunazotumia katika maandalizi yetu ya kuachana na aina Mpya ya utumwa, yaani KUAJIRIWA.
Lengo lingine la uzi huu ni kuonesha sababu ya uamuzi wa kutaka kuacha kazi ili kila mtu apime kama sababu yake ni sababu tosha ya kufanya hivyo ama la, lakini hii pia inatoa fursa kwa wachangiaji wengine kufanya assessment ya maamuzi hayo.
Kuacha kazi na kujiajiri na pengine baadae kufikia hatua ya kuajiri ni uamuzi wa kuyatoa maisha yako mikononi mwa mtu mwingine (muajiri) na kuyakabidhi mikononi mwako mwenyewe. Ni kujitoa katika kutawaliwa na kuamua kujitawala mwenyewe. Ni vyema pia tukajulishana gharama za maamuzi hayo mazito ya kutoka Misri kuelekea Kanani. NI WAZI HAITAKUWA SAFARI NYEPESI.
Tushauriane time scale, mfano mimi ninakimbizana na miaka Mitatu kabla sijatoka kwenye hii Jela. Baada ya hapo ntarudi uraiani, nyumbani kuishi maisha yangu ya uhuru.
Tunaotaka tutoke hii Jela Tushauriane humu, je tukusanye mtaji sasa bila kufanya ujasiriamali na tutakapoacha tu kazi ndio tuanze rasmi ujasiriamali? Ama tuanze sasa hivi kufanya kazi na ujasiriamali ili tu-taste ladha ya ujasiriamali kabla hatujaacha kazi? (Ila hata mambo yakiwa magumu kwenye ujasiriamali kipindi tupo kazini na tunafanya ujasiriamali, kuendelea na kazi sio option). Kubaki Jela haiwezi kuwa option kisa kuna dona na maharage ya bure, bora kuwa uraiani ule mlo mmoja wa maharage na ugali kwa mwaka mmoja ili uje kula asali na maziwa kwa miaka mingi ijayo.
Kila mtu anaweza kuwa na sababu yake ya kuacha kazi. Wengine watakwambia kazini kipato kidogo, lakini amini nakwambia hata ukiajiri na kutoweka mwili, moyo na roho yako kwenye hiyo kazi, unaweza kupata kipato kidogo kuliko hata kile cha kazini. Katika swala la kipato, tofauti ya kipato cha kuajiriwa na kujiajiri ni kipato kimoja Anapanga mtu akulipe kiasi gani, na Kingine Unapanga wewe uingize kiasi gani.
Wengine watakwambia, wanataka waache kazi sababu ya Mateso kazini,ubabe wa mwajiri, kutojali kwa mwajiri. Yote hayo yanakupa HASIRA, geuza hasira zako kuwa DRIVES, zigeuze kuwa USONGO.
Kwanini nataka niache kazi, nataka kuwa huru, nataka kusafiri huku na kule bila kujali bosi atahesabu siku tatu sipo kazini anifute kazi. Sitaki kumpigia mtu mmoja Magoti (bosi) ili kipato changu kiendelea kutiririka. Bora nipigie magoti watu wengi (wateja) ili kipato kiingie, kwani mteja mmoja akiamua kunifukuza kazi ntakuwa na option kwa mteja mwingine.
Uzi wetu TUNAOPANGA KUACHA KAZI, the clock is clicking....LET'S DO IT, LET'S GO.... Tunapenda pia kuchota busara za wale walioacha kazi na wapo wanaendelea kupambana.