Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Heshima kwenu viongozi

Nimeona ni vyema na sisi wenye lengo la kuacha kazi tukawa na uzi wetu kama wenye agenda nyingine walivyoanzisha uwanja wao.

Lengo la nyuzi hii ni kupeana mawazo, moyo na uzoefu wa mbinu bora tunazotumia katika maandalizi yetu ya kuachana na aina Mpya ya utumwa, yaani KUAJIRIWA.

Lengo lingine la uzi huu ni kuonesha sababu ya uamuzi wa kutaka kuacha kazi ili kila mtu apime kama sababu yake ni sababu tosha ya kufanya hivyo ama la, lakini hii pia inatoa fursa kwa wachangiaji wengine kufanya assessment ya maamuzi hayo.

Kuacha kazi na kujiajiri na pengine baadae kufikia hatua ya kuajiri ni uamuzi wa kuyatoa maisha yako mikononi mwa mtu mwingine (muajiri) na kuyakabidhi mikononi mwako mwenyewe. Ni kujitoa katika kutawaliwa na kuamua kujitawala mwenyewe. Ni vyema pia tukajulishana gharama za maamuzi hayo mazito ya kutoka Misri kuelekea Kanani. NI WAZI HAITAKUWA SAFARI NYEPESI.

Tushauriane time scale, mfano mimi ninakimbizana na miaka Mitatu kabla sijatoka kwenye hii Jela. Baada ya hapo ntarudi uraiani, nyumbani kuishi maisha yangu ya uhuru.

Tunaotaka tutoke hii Jela Tushauriane humu, je tukusanye mtaji sasa bila kufanya ujasiriamali na tutakapoacha tu kazi ndio tuanze rasmi ujasiriamali? Ama tuanze sasa hivi kufanya kazi na ujasiriamali ili tu-taste ladha ya ujasiriamali kabla hatujaacha kazi? (Ila hata mambo yakiwa magumu kwenye ujasiriamali kipindi tupo kazini na tunafanya ujasiriamali, kuendelea na kazi sio option). Kubaki Jela haiwezi kuwa option kisa kuna dona na maharage ya bure, bora kuwa uraiani ule mlo mmoja wa maharage na ugali kwa mwaka mmoja ili uje kula asali na maziwa kwa miaka mingi ijayo.

Kila mtu anaweza kuwa na sababu yake ya kuacha kazi. Wengine watakwambia kazini kipato kidogo, lakini amini nakwambia hata ukiajiri na kutoweka mwili, moyo na roho yako kwenye hiyo kazi, unaweza kupata kipato kidogo kuliko hata kile cha kazini. Katika swala la kipato, tofauti ya kipato cha kuajiriwa na kujiajiri ni kipato kimoja Anapanga mtu akulipe kiasi gani, na Kingine Unapanga wewe uingize kiasi gani.

Wengine watakwambia, wanataka waache kazi sababu ya Mateso kazini,ubabe wa mwajiri, kutojali kwa mwajiri. Yote hayo yanakupa HASIRA, geuza hasira zako kuwa DRIVES, zigeuze kuwa USONGO.

Kwanini nataka niache kazi, nataka kuwa huru, nataka kusafiri huku na kule bila kujali bosi atahesabu siku tatu sipo kazini anifute kazi. Sitaki kumpigia mtu mmoja Magoti (bosi) ili kipato changu kiendelea kutiririka. Bora nipigie magoti watu wengi (wateja) ili kipato kiingie, kwani mteja mmoja akiamua kunifukuza kazi ntakuwa na option kwa mteja mwingine.

Uzi wetu TUNAOPANGA KUACHA KAZI, the clock is clicking....LET'S DO IT, LET'S GO.... Tunapenda pia kuchota busara za wale walioacha kazi na wapo wanaendelea kupambana.
Good
 
Wote mnataka kuwa bilionea?

That is not life reality!!

Take a look at the universe and all is creation, you will realize diversity is universe reality

You become who you were meant to be!

A cat can't be a lion

Monkey can't be an elephant

Those meant to be business man will always find a way to be in business

But I'm surely telling you... there's bunch of people who are made to serve as workers

These can be acknowledged by looking all business run by bilionea and tilionea have employed majority of us and these is the reality.

By these... I Call for those meant to be workers to develop themselves and be creative enough to alleviate all the financial constraints facing them

And those employee others should straive to pay descent renumeration for their workers including government

There is no problem with being an employee...but the poor wages paid.

Dear professionals... kindly don't leave our school and universities running to to do business

We really need you for the call God has given you

Let's unite together fighting for the rights and well-being of all works in our nation for the betterment of our society

Tuheshimiane sote

Watumishi kongore kwenu

Wafanyabihashara na wajasiliamali hongera kwenu

Gap za maisha is Life reality and not inferiority

Kind regards
 
Mkuu tukipata ubilionea watu 200 wa humu jf kuna ubaya gani?
Watu wa kutumikishwa bado watabaki wengi sana hawawezi kuisha.
 
Jambo la Msingi kama unataka kuacha kazi na kujiajiri ni kuwa na Malengo ya biashara na uwe na commitment ya kuanza na kidogo ulichonacho ukiwa bado umeajiriwa unaweza ukachukua hata mshahara wa mwezi mmoja ukaanzia hii inakusaidia kugain experience wakati unapunguza risk ya kupoteza pesa nyingi kwa wakati mmoja kitu kingine jipe muda Kila siku wa kuifanya mwenyewe hiyo biashara yako hata kama umemuajiri mtu
 
Kwa mimi bora niajiriwe, kwa sababu naona kama unakuwa umejihakikishia pesa fulani kila mwezi. Kunawatu wanasema ati ukijiajiri unakuwa huru, lakin mimj naona waajiriwa wako huru zaid, na walijiajiri wako busy sana na kazi kwa sababu wanajua wakizembea hawatapat kitu.
lakin pia risk ni kubwa sana, mim nimewaona watu wakiacha kazi na kuingia kwenye biashara na kilimo. Kiukweli nimewaona asilimia chini ya hamsini wakifanikiwa. Ila wengi wameishia kuanguka na wanatafuta kazi kwenye private school. Kilimo hakiaminiki na biashara inaanguk mda wowote au kukua muda wowote.

Mwisho, kama wew kichwa chako ni cha biashara basi usitegemee kutoka kinaisha kwa kuwa mfanyakazi, kwasabau kanuni ya mfanya biashara ni kwamba ukifanya kazi sana na kipato kitakuwa kikubwa na kwenye ajira hata ufanye kazi sana mshahara utabaki pake pale regardless of efforts you made
Ila kuajiriwa kuna raha yake
 
Mkuu uko sahihi.
Kwenye kujiajiri ukiingia kwa kukaririshwa unapotea mazima.
Ndio maana wajanja huwa wanafanya biashara huku wameajiriwa pia.
Assume Kuna jamaa mmoja tulikuwa tunafanya naye kazi.
Alikuwa ana biashara kubwa tu ya kuagiza magari na kuuza na pia ana daladala/coaster zake zaidi ya 10 mjini dar.
Na mshahara wake ulikuwa ni wa kawaida tu Kama milioni 2 tu lkn hakuthubutu kuacha kazi.
 
Shukrani mkuu.

Siku chache kuanzia leo nita-post uzi kuelezea hili wazo nipo nalo ili watu waone namna gani wanaweza tumia platform yangu kujiingizia kipato.

Mimi ni mjasiriamali kwahiyo jambo la kwanza kabisa nikijua potential clients wanataka nini.

Nitaleta hapa JF.

Wazo lako liliishia wapi mkuu?
 
kozi ya environmental sciences and management inayotoleawa ardhi kwa level ya degree yupo ndugu amemaliza ila anatafuta mwanga wa kujiajiri mwenyewe. kuanza kujiajiri kwa mtaji mdogo. cpa hajapitia (nemc) naombeni msaada
 
Kujiajiri sio lazima utumie hyo fani yako bali ni ubunifu wako tu wa kujifunza vitu mbalimbali.
Unaposema kujiajiri kwa kutumia hyo fani ni kwa kujipanga sana maana yake utahitajika usajili kampuni uwe contractor au consultant na kuanza kutafuta tender Kama unavyowaona contractors wa civil engineering.
Kwa hyo sio Jambo la mchezo mchezo kwamba umetoka chuo tu na kukurupuka.
 
Back
Top Bottom