kuna aliy wahi nunua kupitia hawa Alibaba wa China? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kuna aliy wahi nunua kupitia hawa Alibaba wa China?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHASHA FARMING, Oct 30, 2012.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  wakuu kuna kitu nataka kununua china na niliwasiliana na wale watu wanao kuwa online kule alibaba na imefikia nitume pesa kwa njia ya western union then wanitumie mzigo kwa njia ya Hongkong Posta Air, ni kama mzigo wa Dolla 54.4, ila bado si jalipa make nasikia ni matapeli sana
   
 2. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kaka,

  Mimi nimeshawahi kununua Alibaba vitu tofauti tofauti, mara kadhaa kwa muda sasa.

  Kuna wafanya biashara wazuri Alibaba na pia kuna matapeli kama ulivyosema. Cha msingi ni kuwa makini na mtu unaefanya nae biashara. Angalia kama ni "Gold Supplier" na kama amekuwa "Verified" na Alibaba. Hizi ni moja ya hatua za awali kuhakikisha kama haufanyi biashara na tapeli.

  Make sure you transact with a verified supplier.

  Pili, cheki kama wana website, na itembelee website yao. Wafanya biashara wengi wa China walio makini wanakua na website nzuri kuonyesha umakini wao.

  Pia, mwambie akupe physical address yake na mtaarifu kuwa una mtu China ambae atakuja kufanya local pick-up. Wafanya biashara wengi matapeli utawajua tu inapofikia hatua hii.

  Kama bado unasita, nitumie link ya Alibaba profile ya hiyo kampuni unayotaka kufanya nayo kazi nione kama naweza kukusaidia.

  Mimi nimenunua vitu Alibaba mara nyingi. Na hata last month nimepokea mizigo miwili kupitia EMS na DHL. Sijawahi kutapeliwa, ila inahitaji uwe makini sana. Wachina ni tapeli sana.
   
 3. Kishaju

  Kishaju Senior Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 106
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  yes na mimi nilishaagiza mzigo na nilipata na kuna mzigo mwingine waliniwekea kwa njia ya meli upo njiani unakuja. mimi nilishafanya biashara nao karibia US$ 2,500
   
 4. v

  viking JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 985
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Never ever buy goods online and make payment through western union .You will beconned
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Kwa nini haifai kulipia via western union? Mbona kampuni nying sana za china zina hiyo optional?
   
 6. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  don't generalize
   
 7. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Yeah, matapeli wengi hutumia njia hii kirahisi zaidi.

  Ni kweli wanaweza kuwa supplier wa uhakika ila kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kutapeliwa ni mkubwa zaidi kwa njia hiyo
   
 8. chash

  chash JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Dola 54 ni pata potea. Ni kiwango kizuri cha kufanyia mazoezi ya kupoteza hela kwa kuwa utachukia lakini kwa mda mfupi alafu utasahau.
   
 9. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,879
  Likes Received: 2,827
  Trophy Points: 280
  Mkuu unamaanisha Dollar 54.4 ambayo hata Tsh.100,000/= haifiki? Basi hiyo mkuu unaweza kuituma tu na hata ikipotea utakuwa umepata uzoefu!!!
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Nov 2, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hata kwenye kutapeliwa kunahitaji uzoefu?
   
 11. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,879
  Likes Received: 2,827
  Trophy Points: 280
  Mkuu kila kitu kinahitaji uzoefu!

  Unafikri akitapeliwa leo na hao Alibaba atarudia tena? Thubutu!! Hivyo hata kutapeliwa nako kunahitaji uzoefu ili usirudie kosa tena!!
   
 12. mayome

  mayome Member

  #12
  Nov 5, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  alibaba wako vizuri sana tu me pia nimeshanunua zaidi ya mara 2, tena malipo kwa western union zaidi ya dola 2000! we chamuhimu ni kujiridhisha kwa huyo supplier wako, ikibidi usimpatie direct peyment kwa mara ya kwanza, utumie acount za alibaba wenyewe co acount za supplier! itakusaidia kua na uhakika.
   
Loading...