Kuna aina ya viongozi na watu ambao wangeishi zama fulani tusingekuwa na maendeleo wala ugunduzi wowote katika sekta ya afya

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
992
1,155
Ndugu wanajukwaa

Nimejaribu kuwaza aina ya mawazo na fikra za baadhi ya viongozi na raia walizonazo kwenye karne ya 21 , zikanipa shida kidogo
Najiuliza Kama wangeishi zama za milipuko ya magonjwa mbalimbali tusingekuwa na chanjo Wala dawa yoyote, maana fikra zingekuwa hizihizi.
Ni watu wepesi kupinga tafiti bila tafiti mpya.
Nawaza hizi fikra tukiziruhusu huko mbeleni hata hospital zinaweza kufungwa maana wanajidai kuogopa watu ambao wanatengeneza asilimia tisini ya madawa na vifaa tiba ambavyo tumetumia miaka na tunaendelea kutumia.
Wanasahau nguvu kubwa inatumika kushawishi kwa sababu ya aina ya fikra walizonazo .
Tangu lini serikali ikawajibika kusaini kwa matibabu ya mtu binafsi,
Kuna kazi kubwa ya kusaidia kubadilisha hizi fikra ,
Nje ya hapo zikipata nafasi ya kutawala tutakuwa na taifa lisilojali taalum tafiti , sayansi, na tutarudi nyuma sana.
Naomba tusitumie kutokujua kwa watu kuwapotosha zaidi

Maandiko yanasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
 
Back
Top Bottom