Buchanan,
Tatizo la sisi Watanzania wengi ni kushindwa kuwa na msimamo mmoja. Kosa ni kosa kwasababu linamhusu mbaya wako lakini kama liko kwa kipenzi basi huyo anaonewa.
Matokeo yake tutaendelea kuhamisha goal posts ili ku fit malengo yetu.
Kwa kila siku kupiga kelele za mafisadi hata pale pasipo na ufisadi wamefanya hilo neno libadilika kutoka kuwa kosa kubwa na kuwa kijembe cha kisiasa ambacho kila mmoja anaweza kutumia dhidi ya mwingine. Hata wale mafisadi wakubwa sasa wana raha maana sio wao tu wanaotajwa na badala yake malaki ya Watanzania wanaitwa mafisadi, wakiwemo wale ambao hawajawahi kuiba hata senti tano ya mtu.
Hao wanaolalamika majimboni kwamba pesa zinamwaga, wanajua ukweli wake na ndio maana hawako tayari hata kufuatilia. Wanachokifanya sio kutatua tatizo la ufisadi, bali kuwadanganya wananchi majukwaani.
Kuna mheshimiwa mmoja, anadai kwenye mikutano yake kwamba mafisadi wanamwaga pesa na kuwapa wajumbe, yeye mwenyewe akimaliza anawapa wajumbe hao hao pesa. Mtu unabaki kujiuliza, hivi wananchi wanafanywa wajinga kiasi hicho?
Watu wanataka maendeleo na sio kelele za majukwaani. Mpambano wa 2010 utakuwa juu ya nani ana vision nzuri ya kulisukuma jimbo mbele, ikiwa ni pamoja na kupambana na majanga mbalimbali pamoja na matumizi mabaya ya pesa za wananchi, na sio tu nani ana uwezo mkubwa wa kupiga kelele za mafisadi akiwa jukwaani.