Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
1. Tumesikia mara kwa mara kwamba baadhi ya Wabunge, hasa wale wanaodai kupambana na ufisadi kulalamika kwamba kuna mafisadi wanaomwaga fedha majimboni mwao kwa nia ya kuwang'oa.
2. Hao ni pamoja na Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), Mbunge wa Kyela na Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) na Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM). Wengine ni Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa (CCM), Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (Chadema) na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM). Mbunge mwingine aliyedai hadharani kuwa mafisadi wanasambaza fedha katika jimbo lake kwa lengo la kumung'oa ni Benson Mpesya (Mbeya Mjini).
3. Kwa kuwa wabunge ni watu wa kuheshimika sana kwenye jamii watu wengi wanaamini kwamba tuhuma hizo ni za kweli!
4. Kwa maana hiyo hali hiyo inaviweka vyombo vya kupambana na ufisadi na rushwa kuonekana kama havifanyi kazi sawasawa, kwa kuwa ETI vyombo hivyo vina NAMNA ya kupata taarifa, hata bila ya kupitia kwa walalamikaji.
5. Waheshimiwa hawa wanapenda kutumia VYOMBO VYA HABARI, sana sana magazeti, zaidi ili kufikisha ujumbe wao.
6. Mimi naona hapa kuna walakini. Nitaeleza:
(a) Wabunge hawa badala ya kutoa taarifa ambazo ni TOO GENERAL (kwamba MAFISADI WANAMWAGA FEDHA MAJIMBONI, bila hata kutaja majina yao au kufikisha taarifa kwenye vyombo husika vya dola) kwenye magazeti, ambapo inaonekana ni kama kujihami vile ili wakishindwa kuwe na sababu ya kujitetea.
(b) Ni kweli kwamba vyombo vya dola vinaweza kupata taarifa kutoka sehemu nyingine, badala ya walalamikaji. Lakini ikumbukwe kuwa WALALAMIKAJI SIO MALAIKA, wanaweza kucheza rafu vile vile ili kuwachafua wenzao kupitia vyombo vya habari! Mtu kama hajafanya ufisadi leo haimaanishi kesho hatafanya ufisadi. Wapambanaji wa ufisadi wa leo wanaweza kuwa mafisadi wa kesho.
(c) Kutokana na (b) hapo juu ni vizuri walalamikaji wenyewe wakafikisha taarifa kwenye vyombo husika vya dola ili ziweze kufanyiwa kazi. Taarifa iliyowasilishwa na mlalamikaji mwenyewe ina uzito kuliko zile za kupata kupitia third party.
(d) Ukifikisha taarifa kwenye vyombo vya dola itarekodiwa ili endapo kama umetoa taarifa ya uwongo uweze kushtakiwa mahakamani kwa kosa la kutoa taarifa hiyo ya uwongo.
MWISHO: (e) Wabunge Wapambanaji kuweni serious jamani suala la kupambana na ufisadi msichukulie kama ngazi ya kujipandisha chati ya kisiasa kwa maana kwamba wananchi ukishawa-fool kupitia vyombo vya habari kwamba unapambana na ufisadi then wakaridhika, basi unakuwa umefanya kazi yako, that's not right at all! Chukueni mfano wa Mbunge wa Karatu, Dkt Wilbrod Slaa ambaye alipeleka hata vielelezo vya kurasa 1,000 Bungeni kuthibitisha madai yake. Vyombo vya Habari then vitachukua taarifa baada au wakati wa kuifikisha kwenye vyombo vya dola!