Kumwagwa Kwa Fedha za Ufisadi Majimboni: Wabunge "Wapambanaji" Acheni Siasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumwagwa Kwa Fedha za Ufisadi Majimboni: Wabunge "Wapambanaji" Acheni Siasa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jan 12, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. Tumesikia mara kwa mara kwamba baadhi ya Wabunge, hasa wale wanaodai kupambana na ufisadi kulalamika kwamba kuna mafisadi wanaomwaga fedha majimboni mwao kwa nia ya kuwang'oa.
  2. Hao ni pamoja na Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), Mbunge wa Kyela na Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) na Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM). Wengine ni Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa (CCM), Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (Chadema) na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM). Mbunge mwingine aliyedai hadharani kuwa mafisadi wanasambaza fedha katika jimbo lake kwa lengo la kumung'oa ni Benson Mpesya (Mbeya Mjini).
  3. Kwa kuwa wabunge ni watu wa kuheshimika sana kwenye jamii watu wengi wanaamini kwamba tuhuma hizo ni za kweli!
  4. Kwa maana hiyo hali hiyo inaviweka vyombo vya kupambana na ufisadi na rushwa kuonekana kama havifanyi kazi sawasawa, kwa kuwa ETI vyombo hivyo vina NAMNA ya kupata taarifa, hata bila ya kupitia kwa walalamikaji.
  5. Waheshimiwa hawa wanapenda kutumia VYOMBO VYA HABARI, sana sana magazeti, zaidi ili kufikisha ujumbe wao.
  6. Mimi naona hapa kuna walakini. Nitaeleza:
  (a) Wabunge hawa badala ya kutoa taarifa ambazo ni TOO GENERAL (kwamba MAFISADI WANAMWAGA FEDHA MAJIMBONI, bila hata kutaja majina yao au kufikisha taarifa kwenye vyombo husika vya dola) kwenye magazeti, ambapo inaonekana ni kama kujihami vile ili wakishindwa kuwe na sababu ya kujitetea.
  (b) Ni kweli kwamba vyombo vya dola vinaweza kupata taarifa kutoka sehemu nyingine, badala ya walalamikaji. Lakini ikumbukwe kuwa WALALAMIKAJI SIO MALAIKA, wanaweza kucheza rafu vile vile ili kuwachafua wenzao kupitia vyombo vya habari! Mtu kama hajafanya ufisadi leo haimaanishi kesho hatafanya ufisadi. Wapambanaji wa ufisadi wa leo wanaweza kuwa mafisadi wa kesho.
  (c) Kutokana na (b) hapo juu ni vizuri walalamikaji wenyewe wakafikisha taarifa kwenye vyombo husika vya dola ili ziweze kufanyiwa kazi. Taarifa iliyowasilishwa na mlalamikaji mwenyewe ina uzito kuliko zile za kupata kupitia third party.
  (d) Ukifikisha taarifa kwenye vyombo vya dola itarekodiwa ili endapo kama umetoa taarifa ya uwongo uweze kushtakiwa mahakamani kwa kosa la kutoa taarifa hiyo ya uwongo.
  MWISHO: (e) Wabunge Wapambanaji kuweni serious jamani suala la kupambana na ufisadi msichukulie kama ngazi ya kujipandisha chati ya kisiasa kwa maana kwamba wananchi ukishawa-fool kupitia vyombo vya habari kwamba unapambana na ufisadi then wakaridhika, basi unakuwa umefanya kazi yako, that's not right at all! Chukueni mfano wa Mbunge wa Karatu, Dkt Wilbrod Slaa ambaye alipeleka hata vielelezo vya kurasa 1,000 Bungeni kuthibitisha madai yake. Vyombo vya Habari then vitachukua taarifa baada au wakati wa kuifikisha kwenye vyombo vya dola!
   
 2. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wewe mwenyewe kwanza Buchanan una maoni gani kweli mafisadi hawamwagi pesa majimboni?
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sina data ndugu Facts1, kama unazo tumwagie hapa. Nani, lini na alimwaga "EPA" ngapi na akina nani!
   
 4. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Taarifa za mafisadi kumwaga fedha majimboni ni za siku nyingi. Ni taarifa za kweli kwani moja ya mikakati ya mafisadi ni kuhakikisha wabunge wote wanakuwa loyal kwao ili waendelee kutuibia. Kamwe hawapendi kuona watu kama akina Dk Mwakyembe wanarudi tena Bungeni. Ni mikakati ambayo imekuwa ikipangwa usiku na mchana na mafisadi chini ya uratibu wa EL na RA.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huo ukweli wa taarifa ni upi?
   
 6. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Hao wabunge wa Si SI SI M wanaosema wanapingana na ufisadi na mafisadi mbona hawawataji mafisadi wanaopingana nao. Mie sielewi kabisa na ni wasaniii.

  Waweke orodha ya ufisadi na mafisadi hadharani kama Shujaa Dk SLAA
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure, hizi taarifa kuwa TOO GENERAL ndio mimi nakuwa na wasiwasi nazo. Mbona Dkt Wilbrod Slaa alitaja orodha ya mafisadi hadharani na vielelezo akatoa! Sasa hawa "wapambanaji" wengine wanadai kuwa eti "kuna fedha zinamwagwa." Lini zilimwagwa, na nani, walimwagiwa akina nani, kiasi gani, hawasemi! Vita gani hiyo isiyokuwa na maadui wanaojulikana? Kama wanafanya hao maadui kuwa ni siri yao na vitendo vya maadui nako ni siri yao, ushahidi ni siri yao, kwa nini wanaropoka kupitia magazeti?
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hapa unajua mchezo unaweza ukawa hivi: Kwa kuwa RA, EL, et al wametuhumiwa kwa ufisadi mara kwa mara, wananchi wakiambiwa kwamba MAFISADI, hata bila kuwataja majina, wamemwaga fedha wataamini moja kwa moja kwamba taarifa ni za kweli na kwa implication watakuwa ni EL, RA, et al. Siwatetei mafisadi lakini vilevile sipendi watu wanao-take advantage! Kutoa data ndio kitakachotenganisha ukweli na uwongo!
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hao wanataka huruma ya wananchi tu.

  Mimi kule Kyela niliwaambia CCM kwamba hayo ni madai makubwa na inabidi wachunguze. Majibu yao ni kwamba wote wanajua ni maneno ya siasa yasiyo na ukweli wowote.

  Ila kama ulivyosema, kule wilayani kuna wananchi wengi tu wanaamini hayo maneno yana ukweli. Kuna vijana wengi walijiunga na kambi yetu wakidhani kuna pesa milioni 400 za ufisadi. Zaidi ya nusu wameshatukimbia walipoona hatuna uwezo wa kuwawezesha au uwezo wa kuwapa pikipiki au baiskeli.

  Hiyo ndio level ya siasa za Tanzania kwasasa, ni accusations juu ya accusations na hakuna anayejali hata kuona kama kuna ukweli. Wacha ifike muda, tutawaambia wawaonyeshe wananchi nani alikuwa anamwaga hizo pesa na nani alipewa.

  Mfano kwenye makala ya Kubenea kuhusu siasa za Kyela, alitaja na jina la mtu anaitwa Matai aliyesema ni kweli watu wanapewa pesa. Tumemtafuta huyo mtu kwenye kijiji walichosema anatoka, wala hayupo; tulitaka sheria ifuate mkondo wake.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ndg Mtanzania nasikia huko Kyela wananchi angalau wameelimika na wanafuatilia mambo! Sehemu zingine wananchi wanakula usingizi si mchezo, they are easily manipulated by politicians! Sehemu nyingine, they simply don't care, akija so n so analeta sera zake na akija mwingine wanaonekana ni sawa tu hata kama sera zao ni tofauti, who cares? So sad!
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  leta ushahidi otherwise ni majungu na mambo ya mitaani tu haya
   
 12. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa tafsiri ya kuwa Wabunge wote wa CCM ni mafisadi?
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbona ushindi waCCM ulikuwa mtamu kwan wote? Iwe leo wanakanana?
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure, hawa "wapambanaji" wasije wakatuteka nyara na wakatuaminisha kwamba "ulalamikaji na majungu" ndio upambanaji wenyewe! Huko ni kuuziana mbuzi kwenye gunia!
   
 15. K

  Kibori Member

  #15
  Jan 13, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa Kama hata wewe unakiri kuwa vyombo vyetu vya kupambana na rushwa vina namna ya kupata habari na kuzifanyia kazi wenyewe kwanini hilo hawalioni, kimisingi hakuna mtu aliye lazimishwa kutoa taarifa kwa chombo hili bali CHOMBO chenyewe kilitakiwa kuona na kufanyia kazi .

  TENA wakati mwingine unawezakusema ukakuta umehatarisha siri zako bila chochote kufanyika !

  Kama unataka kuelewa kwa UPANA zaidi wewe Kama huamini kuwa MAFISADI wanamwaga FEDHA katika majimbo ? Je unaamini Repoti ya Kamati Teule ya Mh. Dr. Mwakiembe ?

  Swali lingine jiulize kwanini Takukuru walisema hakukuwa na shida yeyote na hatimae kubariki kazi iendelee ?

  Swali lingine MBONA EL NA RA ambao ndio wanasikika sana washutumiwa kuhusu kumwaga FEDHA kwanini haya yote yatokea baada ya Repoti ya Mwakiembe ? Maanake hakukuwana na shida hizi wakati wa uchaguzi 2005...... dhidi ya ndugu hao wanaotuhimiwa... Kutoka kwa wabunge hao, tena kwanza wengi wao wanalalamika ndio mara yao ya kwanza kuingia BUNGENI ..... lakini haya yote yanatokea baada ya kuonyesha misimamo yao ya kuwatetea wanatanzania na mali za taifa kazi ambayo waliwaomba radhaa wananchi kuifanya.

  Please kama utajibu maswali haya utajua kama FEDHA zinamwagwa na nani wapi au la ?

  Please ukishasoma na kutafakari do not hesitate pia kuonyesha mtazamo wako !


  Sasa kwanini TAKUKURU isifanye hii kazi wenyewe halafu wao wenyewe kwa sababu ndicho chombo husika, watoe taarifa baada ya hapo kusema kwa umma kwamba wanachosema wabunge hao ni UONGO au LA ?

  KAMA TAKUKURU njia yao MOJA ya kupata taarifa nikujua watu wanalalamikia nini, kwanini wasione hili ambalo limezua Mjadala wa Kitaifa au Mpaka Mh. Rais awaagize wafanye hivyo ?

  Ha ha ha ha ha ha ha ha HUYU RAIS anakazi kweli kweli ! Mpaka kila kitu afanye yeye wakati watu walikula KIAPO cha KUHESHIMU NA KUILINDA KATIBA !

  ITS TOUGH TO BE PAID FOR THE JOB THAT YOU EITHER DONT KNOW OR THAT YOU ARE NOT DOING AT ALL.

  Sasa kama mtu umeajiriwa kula Rushwa sasa utapambanaje na Rushwa ! Utakuwa tu unasubiri Maagizo ya Mh. RAIS because hujui unachotakiwa kufanya.
   
 16. m

  magoli Member

  #16
  Jan 13, 2010
  Joined: Nov 14, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .
  Ndugu,
  Hauelewi kiswahili?.Umeambiwa sema.Wapi na ni akina nani?.Tumechoka na maneno ya uvumi na umbea.Huu ni ukumbi wa wazi na kama alivyosema aliyeleta hii thread.

  Wewe tueleze hizo pesa walimpa nani?.

  Sawa RA na EL Hawapendi watu kama Mwakyembe arudi bungeni,lakini kwa upande mwingine Mh Mwakyembe naye Hapendi RA na EL warudi tena Bungeni.

  Sasa Hizo pesa uliziona?
   
 17. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Katika wabunge wanaojitambulisha kama wapiganaji kuna ambao "wame-undeperfom maeneo yao ya bunge" sasa wanataka kuwadanganya wananchi wasije kuelezwa mapungufu yao...

  Nionavyo mimi kwakuwa ni wana ccm wacha watwangane kwenye chama chao ni advantage kwa upinzani maana watakuwa wamepambana kwenye chama kabla ya kwenda kwa wananchi na kutakuwa na majeraha mengi sana.

  Hawa wabunge waache demokrasia ichukue mkondo wake na kama wanataarifa za pesa chafu watumie vyombo husika au ikibidi vyombo vya habari (wananchi) ikiwa watakosa ushirikiano kutoka kwa TAKUKURU
   
 18. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  I like this, mtu kaajiriwa kula rushwa na analipwa, kaaazi kweli kweli!
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. Ni kweli nilisema kuwa vyombo vyetu vina namna ya kupata taarifa vyenyewe, lakini kumbuka kuwa suala la rushwa ni gumu sana kupambana nalo kwa kuwa mtoaji na mpokeaji wanakuwa wamekubaliana. Ipo kazi kubwa ya kumfanya mtoaji au mpokeaji akupe taarifa huku akijua kwamba alifaidika. Just imagine Mpendazoe kalalamika kupitia kwenye magazeti kuwa kule Jimbo la Kishapu MAFISADI wamemwaga fedha kibao! Hataji hao MAFISADI ni akina nani, lini walimwaga, walimmwagia nani, kiasi gani. Sasa hiyo ni taarifa au ni ujinga mtupu? Na wakichunguza kama walivyofanya baadhi ya wananchi Wilayani Kyela wakakuta taarifa ni za uzushi akamatwe kwa kutoa taarifa ya uwongo? Si atakuruka mita mia?
  2. Jukumu la kutoa taarifa ni la yule aliyeona kosa la rushwa likitendeka kulingana na kifungu cha 39 (1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, 2007, Na. 11 ya 2007 ambacho kinasema: "Every person who is or becomes aware of the commission of or the intention by another person to commit an offence under this Act shall be required to give information to the
  Bureau.
  " Hicho kifungu kimetumia neno SHALL kuonyesha kwamba ni LAZIMA kutoa taarifa na sio kuifanya hiyo taarifa kuwa SIRI yako kama maelezo yako uliyoyatoa hapo juu.

  3. Ripoti ya Mwakyembe inahusikaje na umwagaji wa fedha majimboni? Na kama kweli umwagaji unaousema kuwa upo in connection na Ripoti hiyo basi solution sio malalamiko ambayo yanakwepa liability!
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Afadhali wewe umenielewa ndugu yangu!
   
Loading...