Kumwagiza mtu aliyefariki akawasalimie waliofariki kabla yake ina maana gani?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,354
Wakuu,

Poleni na msiba wa Kitaifa uliopo mbele yetu.

Tukiwa bado katika maombolezo ya Kifo cha Raisi Mstaafu BM Mkapa, naomba kuuliza jambo;

Kumekuwa na nyimbo na mashairi katika misiba hasa hii ya watu mashuhuri,tangu kwa Ruge, Mengi wengine wengine maarufu waliofariki hapa Tanzania ambapo wamesikika waimbaji wakiwaambia marehemu awasalimie watu ambao nao tayari waliokwisha fariki kabla yao, mfano Nyerere maana yake nini hasa?

Au huwa wana maana gani hasa kusema hivyo,au wengine huenda mbali zaidi na kuwapa maagizo kwamba marehemu awaeleze waliotangulia kwamba huku duniani kuna hiki na kile kinaendelea?

Je, huwa wanamini watakutana wapi? na kwa Imani ya ipi hasa?

Naomba kufahamishwa.

Asante.


[URLhttps://youtu.be/WIPrNLMFvO4][/URL]
 
hawamuagizi bali wanajisemea tu kama kujifariji,ndio kuna mswahili mmoja huko twitter ananibishia sana mimi ninaposema kwamba ki uhalisia hapo huwa wanatoa tribute sio kumuagiza marehemu
 

Attachments

  • 08640C44-B427-44D0-A4CE-C2EC6D95F992.png
    08640C44-B427-44D0-A4CE-C2EC6D95F992.png
    55.8 KB · Views: 1
Nyimbo, Misa plus neno la Mungu ile ni faraja kwa wafiwa ili wasiendelee kumlilia mda mrefu. Na vinginevyo
Ok,sasa kwanini maneno ya faraja yasiwalenge zaidi waliofiwa kama familia na tuliobaki badala yake marehemu ndio anakuwa main focus?
 
Imani tu isiyo na ushahidi wowote wenye maana yoyote.

Ila ingekuwa na ushahidi kuwa ujumbe unafika watu wangekuwa wanapewa maagizo wakiwa hai halafu wanauliwa wapeleke ujumbe.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom