Kumuondosha Mathayo David bila Tibaijuka, rais hachanganyi na zake?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Kuhusu agizo la rais la kutenga maeneo David alipashwa ashirikishwe tu na Tibaijuka, Sasa kumwadhibu David wakati mwenye ardhi/maeneo kama rais alivyosema ni Tibaijuka, Mpaka sasa watu wanakukfa kwa mapigano ya kugombea ardhi, sera iko wapi??? bado mtz hana uhakika wa kupata ardhi kama hajakura ganji kubwa, Je ni sahihi rais kuidhinisha Daivd out wakati Tibaijuka akibaki????

Rais hatumii tu ripoti ya kamati ya bunge pia anavyombo na uelewa mpana, angeongeza jina la Tiba ingekuwa rais makini, labda tusubiri orodha za mawaziri mzigo.

Nawasilisha
 
Si ndiye muasisi wa akili za kuambiwa changanya na zako??? au labda alipigiwa simu wakati mionzi ya kuchunguza afya bado iko kichwani????
 
Hata mimi ilinichanganya kidogo Mh Pinda aliposema David Mathayo anawajibika kwa sababu mifugo iliyokuwa inaua na kuteswa au wafugaji walioteswa ni wa wizara yake ila alikaa kimya hakuchukua hatua zo zote(uzembe).

Basi na Ardhi iliyokuwa inagombaniwa ni ya wakulima ambayo waziri hakuwalinda na ardhi yao wakati wafugaji wanawavamia. Wakulima wengi wamepoteza maisha wote mashahidi.

Hapa mama Tibajuka amepona kwa sababu "scope of work" ya kamati haikuguza ardhi ya wananchi ni maeneo ya hifadhi tu.

Naomba waziri wa Kilimo, Mifugo(ameshaondoka) na ardhi pia wawajibishwe kwa mauji ya wakulima na wafugaji. Hii ni mbaya zaidi maana kila kukucha watu wanakufa. Pinda unda kamati hili swali ni gumu na tumechoka kusikia haya mauji
 
SasaMathayo ametoka kwa nn?Lembeli ameshindwa kutushawishi wananchi tuamini Mathayo amekosea isipokuwa Mathayo amejieleza mpaka tumegundua ameonewa,fikiria anaomba sh 300b ya kuchimba malambo ili mifugo isizurure anaambiwa atapewa 60 ila mpk sasa kapewa 14 tu.Hapo mi naona tatizo ni mfumo mzima wa uongozi serekali,tungefumua wote kwani kuanza upya si ujinga
 
Au mawaziri wa kike wana kifyonza mtikisiko???? yaani rais kama taasis hawakutaka kumsikiliza david, japo walimuona kimakosa, JE TUTAFIKA??? inamaana hawamwoni Tibaijuka kabisaaaaaaaa, Kweli ukizaliwa mwanaume ni mateso na kuhangaika
 
Ukipima vizuri na kulinganisha serikali za awamu zotee...hii ya jk itakuwa ya mwisho kwa ufanisi. Raisi sio mfuatiliaji kabisa wa mambo yanayotokea nchini. Kila jambo anataraji aambiwe na washauri ama na watendaji husika kwenye sekta fulani....he has no individual effort to monitor issues....kila siku kiguu na njia. Mimi najiuliza iweje raisi atangaze operesheni alafu asijue hiyo operation inatekelezwaje? Haya mambo ya kutoa watu kafara bila kuangalia mfumo ulivyo na kuurekebisha hautasaidia. Wizara ya maliasili ni kitimoto na haikaliki....ni kwa nini? Kwangu mimi hii ni great failure of my president....kiongozi kazi yake sio kuteua na kutengua tu ni zaidi ya hayo.
 
SasaMathayo ametoka kwa nn?Lembeli ameshindwa kutushawishi wananchi tuamini Mathayo amekosea isipokuwa Mathayo amejieleza mpaka tumegundua ameonewa,fikiria anaomba sh 300b ya kuchimba malambo ili mifugo isizurure anaambiwa atapewa 60 ila mpk sasa kapewa 14 tu.Hapo mi naona tatizo ni mfumo mzima wa uongozi serekali,tungefumua wote kwani kuanza upya si ujinga

Rais hana uwezo wa kuchaganya na zake, kwel mathayo pumzika ila bila tibaijuka umeonewa sana, umedhalilishwa sana, ila fanya kaz ya ubunge tu
 
Hata mimi ilinichanganya kidogo Mh Pinda aliposema David Mathayo anawajibika kwa sababu mifugo iliyokuwa inaua na kuteswa au wafugaji walioteswa ni wa wizara yake ila alikaa kimya hakuchukua hatua zo zote(uzembe).

Basi na Ardhi iliyokuwa inagombaniwa ni ya wakulima ambayo waziri hakuwalinda na ardhi yao wakati wafugaji wanawavamia. Wakulima wengi wamepoteza maisha wote mashahidi.

Hapa mama Tibajuka amepona kwa sababu "scope of work" ya kamati haikuguza ardhi ya wananchi ni maeneo ya hifadhi tu.

Naomba waziri wa Kilimo, Mifugo(ameshaondoka) na ardhi pia wawajibishwe kwa mauji ya wakulima na wafugaji. Hii ni mbaya zaidi maana kila kukucha watu wanakufa. Pinda unda kamati hili swali ni gumu na tumechoka kusikia haya mauji

Ni scope of work or scope of reasoning ya viongozi wetu
 
Ukipima vizuri na kulinganisha serikali za awamu zotee...hii ya jk itakuwa ya mwisho kwa ufanisi. Raisi sio mfuatiliaji kabisa wa mambo yanayotokea nchini. Kila jambo anataraji aambiwe na washauri ama na watendaji husika kwenye sekta fulani....he has no individual effort to monitor issues....kila siku kiguu na njia. Mimi najiuliza iweje raisi atangaze operesheni alafu asijue hiyo operation inatekelezwaje? Haya mambo ya kutoa watu kafara bila kuangalia mfumo ulivyo na kuurekebisha hautasaidia. Wizara ya maliasili ni kitimoto na haikaliki....ni kwa nini? Kwangu mimi hii ni great failure of my president....kiongozi kazi yake sio kuteua na kutengua tu ni zaidi ya hayo.

Rais anachagua prof harafu prof anakuwa kama darasa la pili, sasa atafanye??
 
Tukisema Anna T hufai unasema eti tuna chuki, kwa hilo na hayo ya kupewa hela chafu waziri ni aibu na hufai hata kuwa mama wa nyumbani
 
Bado una msimamo wako kuwa tunachuki tu, au sasa umejua kuwa wewe ni mkwapuaji wa hela za umma na hufai, ondoka mama, hatuandika kwa kuonea watu, hutufai ondoka, ikibidi ukakutane na mkono wa sheria. Unafanye money laundry ukiwa waziri???
 
nenda mama nenda, nenda mama nenda, mpango wa makazi na viwanja kwa umma umekushinda sasa unapewa hela tu unachukua bila kujua lazima ufanye kazi ili kupata hela nenda mama nenda, au umelelewaje
 
Back
Top Bottom