Kumuomboleza Marehemu kwa nyimbo za Maombolezo na maneno ya kumpamba ni Kumpenda au ni Unafiki tu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
Je kumuomboleza ' Marehemu ' kwa Nyimbo za ' Maombolezo ' pale tu habari za ' Kifo ' chake zikisikika na kabla bado ' hajazikwa ' huku ' Watu ' wengine nao ' wakimpamba ' hata kwa mengineyo ambayo kiuhalisia ' Marehemu ' alikuwa hayafanyi na pengine hata asingeyafanya ni ' ishara ' ya Kumpenda au ni ' muendelezo ' tu ule ule wa ' Unafiki ' wetu ' uliotukuka ' sisi Waombolezaji?

Nitashukuru nikijibiwa hili swali langu na vile vile naomba nichukue tu ' fursa ' hii ' adhimu ' kabisa kuwatakia ' Rest in Peace ' wale wote waliozikwa kitambo, juzi, jana na watakaozikwa pia leo hii katika ' Makaburi ' mbalimbali hapa nchini Tanzania. Mbele wao sisi nyuma!

Nawasilisha.
 
cha kwanza umesema "nyimbo za maombolezo" hii ni sahihi kwa kua watu wanaomboleza msiba wa mpendwa wao hapa mimi sioni kama kuna unafki wowote.
Hili la watu kumpamba marehemu kwa mambo kedekede mazur ambayo mengine ni ya uongo na kuacha yale mabaya ambayo ameyatenda mimi naona ni unafki uliotukuka ambao umefkia kiwango cha lami
 
Mbona kama Kejeli mkuu...Marehemu hapaswi kunenewa mabaya muda mwingine

Hizo 'Kekeli ' umeziona na unazijua Wewe Mkuu ila Mimi ' Hoja ' yangu ipo pale pale kwamba kwamba Je kumuomboleza Marehemu kwa kumpigia Nyimbo za maombolezo ' mfululizo ' huku ' Wadau ' wengine ' wakimpamba ' kwa ' Sifa ' mbalimbali pengine hata kwa yale ambayo labda ' Marehemu ' hakuyafanya na asingeyafanya ni ' ishara ' ya Kumpenda au ni unafiki tu?

Jikite katika ' Content ' yangu na acha ' blah blah ' tafadhali.

Rest in peace sana kwa wale wote ' waliozikwa ' Kitambo, juzi, jana na kama pia wapo watakaozikwa leo sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania. Mbele wao sisi tupo nyuma yao!
 
cha kwanza umesema "nyimbo za maombolezo" hii ni sahihi kwa kua watu wanaomboleza msiba wa mpendwa wao hapa mimi sioni kama kuna unafki wowote.
Hili la watu kumpamba marehemu kwa mambo kedekede mazur ambayo mengine ni ya uongo na kuacha yale mabaya ambayo ameyatenda mimi naona ni unafki uliotukuka ambao umefkia kiwango cha lami

Nashukuru kwa ' mchango ' wako.
 
Hizo 'Kekeli ' umeziona na unazijua Wewe Mkuu ila Mimi ' Hoja ' yangu ipo pale pale kwamba kwamba Je kumuomboleza Marehemu kwa kumpigia Nyimbo za maombolezo ' mfululizo ' huku ' Wadau ' wengine ' wakimpamba ' kwa ' Sifa ' mbalimbali pengine hata kwa yale ambayo labda ' Marehemu ' hakuyafanya na asingeyafanya ni ' ishara ' ya Kumpenda au ni unafiki tu?

Jikite katika ' Content ' yangu na acha ' blah blah ' tafadhali.

Rest in peace sana kwa wale wote ' waliozikwa ' Kitambo, juzi, jana na kama pia wapo watakaozikwa leo sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania. Mbele wao sisi tupo nyuma yao!
Ni ishara ya heshima tu nadhani..haipaswi kumnena kwa mabaya
 
Mleta mada umeleta changamoto kubwa sana ambayo ipo ktk jamii zetu..

Ila kuhusiana na mada mie sina comment

Sent from my Bravo Z11 using JamiiForums mobile app
 
Hata katika kuwaombea,nadhani iwe Marehemu alazwe mahali anapostahili peponi/kuzimu kwa shetani.

Philips X2560

Utakuta lijitu lilikua linafanya upuuzi duniani halafu likifa eti unalisemea mema niujinga wakiwango chalami ya zege.

Napenda Watu ' waelewa ' kama Wewe humu JF. Safi sana na tupo pamoja na comment yako nimeipenda na nimeikubali.
 
Back
Top Bottom