Kumuelezea mpenzi wako historia yako ya kimapenzi kwa ulipotoka ni sawa?

Tatizo lenu mnaona kila mtu anatembeza hiyo nanihi yake hovyo hovyo ,mnapenda kudanganywa.


exactly Mentor na hasa kama Past yenyewe ina utata utata hivi unaweza kuspoil kila kitu aisee

Hivi ni kwa nini wengi hasa wasichana utasikia wanasema "wewe ni wa tatu, wa tatu tu, wa kwanza primare, o level nilikuwa na mmoja akanizingua hapa nina miaka 5 sijawa na uhusiano wa kimapenzi" ...dammn,,uwongo mtupu bora wasiseme kabisa....
 
Mie nina mifano mingi sana kuhusu issue hii ndio maana napigia debe kujua historia ya mwenzi. Nitauweka mfano mmoja hai hapa nafasi ikiruhusu kama sio leo baadaye basi kesho. Mambo ya kuchukuana kimzobemzobe kama unabeba tenga la nyanya MWIKO! Kama unachukua Changu doa basi hilo linaeleweka :)

Hata tenga la nyanya utataka kulifungua na kuangalia nyanya kama nyingi ni nzima au zimeshaharibika kabla ya kufanya uamuzi wa kununua tenga lile au kuangalia lingine :)

Mwanamke/Mwanaume akutaka kukutenda atakutenda tu siyo kwa sababu ya kile ulichomwambia kuhusu mahusiano yako ya nyuma. Ndio maana hata waliokutwa bikira nao wanatendwa katika mahusiano kama wale ambao hawakukutwa bikira.
 
wengi walio kwenye uhusiano mpya huwa wanapenda kumwambia au kumuelezea mpz wake historia yake ya kimapenzi uko alipo toka,utakuta mpz wako anakwambia yaan nilikuwa sijatulia kweli yaani nilikuwa mtu wa mademu au wanaume sana yaan nilikuwa napenda sana starehe.je ipo sana?

Wazungu tu ndo wanaweza hii mambo na wabongo wenye kuleta uzungu uzungu
 
With this principal of Don't ask, don't tell" there is no room to ask for anything!
Ofcourse there is...unless you start off by telling your partner not to ask a single question about your past.As far as your formula is concerned it only works “if the other person doesn‘t ask ... you don‘t tell.“ Maybe you should change it from DADT to DABIWT - Don‘t Ask Because I Won‘t Tell ...or EIYAIWT- Even If You Ask I Won‘t Tell.
 
Mie nina mifano mingi sana kuhusu issue hii ndio maana napigia debe kujua historia ya mwenzi. Nitauweka mfano mmoja hai hapa nafasi ikiruhusu kama sio leo baadaye basi kesho. Mambo ya kuchukuana kimzobemzobe kama unabeba tenga la nyanya MWIKO! Kama unachukua Changu doa basi hilo linaeleweka :)Hata tenga la nyanya utataka kulifungua na kuangalia nyanya kama nyingi ni nzima au zimeshaharibika kabla ya kufanya uamuzi wa kununua tenga lile au kuangalia lingine :)Mwanamke/Mwanaume akutaka kukutenda atakutenda tu siyo kwa sababu ya kile ulichomwambia kuhusu mahusiano yako ya nyuma. Ndio maana hata waliokutwa bikira nao wanatendwa katika mahusiano kama wale ambao hawakukutwa bikira.
BAK nakubaliana na wewe mwanzo mwisho.Hicho kisa naomba ukiharakishe maana tayari sili wala sitamani kulala kwa curiousity.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maan! Kuuliza au kujua historia ni vyema. Jamani hata km c vyema mie huwa cwez ku2liza nafsi, lazm nikufanyie u-CIA wa nguvu kabla cjajitoa kwako jumla. Hao wanaojidai past doesnt matter wanasema tu ila naturaly lazma utamani kujua past ya mwenzio. Walisema curiosity killed the cat ila bora afe na ukweli uwe wazi. Past inasaidia sn kujua m2 ulienae yukoje so utajiweka tayari kisaikolojia, kimwili na hata kiuchumi....ili kukabiliana na changamoto mbalimbali! UKIWA WANGU JIANDAE KUJIELEZA NA KUCHUNGUZWA TENA SANA....!
 
Maan! Kuuliza au kujua historia ni vyema. Jamani hata km c vyema mie huwa cwez ku2liza nafsi, lazm nikufanyie u-CIA wa nguvu kabla cjajitoa kwako jumla. Hao wanaojidai past doesnt matter wanasema tu ila naturaly lazma utamani kujua past ya mwenzio. Walisema curiosity killed the cat ila bora afe na ukweli uwe wazi. Past inasaidia sn kujua m2 ulienae yukoje so utajiweka tayari kisaikolojia, kimwili na hata kiuchumi....ili kukabiliana na changamoto mbalimbali! UKIWA WANGU JIANDAE KUJIELEZA NA KUCHUNGUZWA TENA SANA....!
ngoja nikuandalie zawadi yako.Usipouliza mara nyingine unaonekana hujali. Kama ni watu mnaotaka kudumu kwenye uhusiano ni vizuri kuulizana. Kama ni kucheza cheza tu haina haja.
 
Based On True Story

Njemba ilikuwa inaonana mara kwa mara na binti mmoja mrembo katika mitaa ya katikati ya jiji la Dar. Walikuwa wanafahamiana kwa sababu walisoma katika shule zilizokuwa jirani japo kufahamiana huko hakukuwa kwa ukaribu kiasi hicho. Kila walipokutana binti alimsalimia jamaa kwa heshima tele na kila mara alimsalimia kwa kupeana mikono, na mara nyingi alikuwa na marafiki zake. Iliendelea hivyo kwa muda mpaka yule njemba mapigo ya moyo yalipoanza kuongezeka kila akutanapo na yule binti. Siku moja akaamua kuuliza yule binti anapofanya kazi, binti bila hiana akamibu yuko katika ofisi moja ya kimataifa katikati ya jiji na pia kumpa business card yake.

Ijumaa moja njemba ikaamua kupita ofisini kwa binti yule kumsalimia, bahati nzuri binti alikuwepo ofisini jamaa akamwambia nilikuwa mitaa ya jirani nikaona nije nikujulie hali, binti akafurahi sana na pia kushukuru. Njemba ikamuomba kama kesho yake wanaweza kukutana majira ya saa nne asubuhi pale snow cream, bila hiana binti akajibu hakuna tatizo atajitahidi kuwepo pale saa nne juu ya alama. Njemba ikatoka pale inachekelea kwa kupata kidate cha asubuhisubuhi na binti ambaye tayari ameshaanza kuupeleka puta J moyo wake.

Baada ya vidate vya wiki chache vya sehemu mbali za maraha za jiji la Dar. Njemba ikaamua siku moja imuweke binti yule kwenye kiti moto kuhusiana na mahusiano yake ya nyuma na kama alikuwa na mtu wakati ule. Binti akauliza unataka nianzie wapi? Njemba ikajibu anzia popote pale ambapo mwenyewe ungependa kuanzia. Binti akaanza kuanika mahusiano yake ya nyuma kwa jamaa. Nilipokuwa kidatu cha tatu nilikutana na jamaa ambaye wakati huo alikuwa kidatu cha nne. Huyu ndio alikuwa Vasco Da Gama. Uhusiano wetu haukuwa wa muda mrefu maana jamaa alikuwa mwingi kupita kiasi basi nilivyogundua hivyo nikaamua kujiweka pembeni na kumpa nafasi ili aendelee kwa raha zake. Nilipokaribia kumaliza O'level nikakutana na na jamaa mwingine ambaye yeye pia alikuwa anamalizia O'level. Huyu tulipendana sana kusema kweli. Majibu yalipotoka wote tukapata bahati ya kuchaguliwa kuendelea A'level katika shule za jijini na hivyo kubahatika kuendelea na penzi letu. Tulipoanza tu kidatu cha 6 jamaa akaanza kuumwa alidai alikuwa anasumbuliwa na tumbo hali iliendelea hivyo kwa karibu miezi mitatu hatimaye ikaamuliwa alazwe Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na matibabu. Baada ya kama wiki mbili tangu alazwe akafariki dunia.

Nilikonda sana kwa woga maana sikujua sababu halisi ya kuugua kwake na mpaka anafariki kwa kuwa alikuwa hali vizuri basi mwili wote ulikuwa umekwisha kabisa. Niliamua nikishapata nguvu na mshtuko ule niende kupima ili kuhakikisha afya yangu bado iko salama. Nilipopima majibu yakawa mazuri kwamba sijaathirika hivyo nikaendelea na masomo na kumaliza vizuri na kuchaguliwa kuingia chuo. Nilipoingia chuo kuna jamaa ambaye wakati mimi naanza pale yeye tayari alikuwa mwaka wa pili katika program tofauti lakini alinisaidia sana katika tips mbali mbali za maisha ya pale chuo na baada ya muda mfupi tukawa marafiki. Tuliendelea naye mpaka namaliza chuo nikaanza kazi baada kama ya miezi 10 tangu nimalize chuo ndio akaamua kuniangushia bomu. Akaniambia tutoke siku hiyo na kwenda katika sehemu tuliyopenda kwenda mara nyingi tu saa za mchana kula nyama choma na moja moto moja baridi. Akaanza hadithi yake na kudai kwamba pamoja na kuwa tumekuwa pamoja kama wapenzi kwa zaidi ya miaka tatu lakini tangu mwanzo wazazi na ndugu zake hawakunikubali. Alidhani kwamba baada ya muda mrefu wa kuwa pamoja watabadili msimamo wao lakini bado sikubaliki ndani ya familia yao. Kwa hiiyo inabidi atafute GF mwingine ambaye wazazi na ndugu zake watamkubali kama mkwe/shemeji yao hivyo alikuwa ananifahamisha rasmi kwamba uhusiano wetu ndio umefikia tamati. Niliumia sana lakini mbele yake ilibidi nijitahidi sana ili nisiangushe hata tone la chozi. Hii ilitokana na sababu za kuamini kwamba uhusiano wetu ulikuwa unaenda vizuri sana na sikuamini kama kunaweza kuwa na bomu kama hilo. Niliporudi nyumbani nililia sana lakini pia nilimshukuru badala ya kunipotezea wakati wangu kumbe yeye anatafuta mchumba ambaye atakubalika kwa wazazi na nduguze. Ni miezi sita sasa tangu hili tukio litokee. Nakaribisha maswali. Jamaa akauliza huyo jamaa wwaliyeachana yuko jijini, binti akajibu ndio. Anaitwa nani akataja jina la kwanza tu, jamaa akauliza na la pili binti akataja, lakini binti naye akauliza kwanini unataka kujua majina yake? Jamaa akajibu mara nyingi watu kama hawa baada ya muda hugundua kwamba wamefanya makosa na hivyo kuja kuomba samahani kwa makosa yao na hivy kutaka kurudiana. Kwa maoni yangu kwa muda mfupi niliokufahamu naona kafanya makosa makubwa sana kuachana nawe, sijui lakini. Jamaa akaongeza swali jingine anafanya kazi wapi, binti akajibu. Jamaa akamalizia kwa kusema kwamba hana maswali zaidi ila kama binti angependa kujua ya nyuma naye alikuwa tayari kumwambia.

Jamaa akaelezea kwamba aliwahi kuwa na mahusiano ya nguvu mara moja na binti ambaye alidhani kwamba angekuwa mkewe, lakini alisafiri nje ya nchi kwa masomo ya muda mfupi kwa miezi sita na alipirudi alimkuta ana mimba. Kitendo cha kusalitiwa na mpenzi wake kilimuuma sana tena kwa kipindi kirefu. Halafu jamaa aliyempa mimba baada ya kujifungua akaingia mitini bila kuhusika kwa namna yoyote ile na malezi ya yule mtoto. Huyo dada yuko mjini lakini kimaisha hali yake ni mbaya sana ameniomba mara chungu nzima nimsamehe turudiane lakini hakukubali kabisa kurudiana naye. Jamaa akadai kwamba kwa wakati ule alikuwa na binti mwingine ambaye wamekuwa naye kwa karibu miaka miwili ila hawajawahi kuongea chochote kuhusu kufunga pingu za maisha na hajampenda kiasi hicho cha kuamua kuwa naye kama mke. Na kutokana na mahusiano yao ya muda mfupi kuanza vizuri sana amemfahamisha huyo binti kwamba ana GF mwingine na hivyo kusitisha mahusiano na huyo aliyekuwa naye ambaye alilalamika sana na kusema kwamba yuko tayari kuwa wa pembeni. Jamaa akakataa.
Waliendelea na mapenzi yao na mpaka sasa wamejaliwa watoto watatu na mwaka kesho watatimiza miaka 12 tangu waone. Kama huwajui ukiwaona utadhani ni newly weds maana pamoja na miaka 12 ya ndoa na miaka 14 ya kuwa pamoja mapenzi yao bado ni ya hali ya juu.

Nimewauliza kama uamuzi wa kuambiana mahusiano yao ya nyuma kwa namna moja au nyingine uliwafanya wawe karibu mno kimapenzi, na wote wakakubaliana uwazi wao kuhusiana mahusiano yao yaliyopita ulisaidia sana katika kuwafanya wawe karibu mno kimapenzi na hawajui kama kutoambiana mahusiano ya nyuma kwa namna moja au nyingine kungeathiri mapenzi yao, lakini wote wakasema mtu anapokuwa hayuko tayari kuwa muwazi na mahusiano yake ya nyuma hasa pale mwenzie angependa kufahamu basi unaanza kuwa na wasiwasi na kujiuliza maswali mengi huku ukiwa na dhana kwamba labda kuna mengine nikiyajua labda sitapenda kuendelea na mahusiano haya.

Binadamu tunatofautiana wengine wanapenda kujua yaliyopita na wengine hawana haja ya kuyafahamu lakini kama penzi litakolea basi usije kushangaa kama alivyoandika Annie kuletewa watoto wa mama/baba mbali mbali, "Hawa ni watoto wangu nilijaaliwa kuwapata katika mahusiano yangu ya nyuma." mdomo unamwagika maana ulijua umepata kumbe umepatikana

NB: I received consent from those 2 love birds to share this story with you
:)





 
Last edited by a moderator:
mueleze kila atakachokuuliza.....at least ndo ninavoamini mimi!ukinidanganya na nikaja kujua mwenyewe,labda tunaweza tusiachane,lakini SITAKUJA KUKUAMINI KAMWE!u kan imajin kutoaminika na mtu wako wa karibu hivo,kama mpenzi hata kama hakuna mazingira hatarishi kati yenu.ukweli utakuweka huru.
 
mimi na fikiri ni bora mzungumze in detail past zenu coz through this kila mtu ata kuwa awere na mwenzake yukoje ana penda nn ili muweze kuji funza ku pitia makosa yenu ya nyuma ni hayo tu ila kiu kweli some time ina umiza
 
let the past be the past-mambo yakuanza kuelezana story za zamani-siku mkija gombana kidogo tu-mtaanza ku-refer mambo ya zamani na kujikuta mna-complicate mambo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom