Kumuahidi mtoto zawadi ni kumfundisha au kumuharibu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumuahidi mtoto zawadi ni kumfundisha au kumuharibu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jun 4, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,186
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Thursday, June 4, 2009
  KUMUAHIDI MTOTO ZAWADI NI KUMFUNDISHA AU KUMUHARIBU?
  Kuna tabia ya sisi wazazi kuwaahidi watoto kwamba tutawapa zawadi fulani kama watafanya kitu fulani. Tatizo la kwanza linalojitokeza hapa ni kwa mtoto kushindwa kujua kwamba anapaswa kufanya mambo mazuri hata kama hakuna zawadi.

  Kila wakati mtoto atakuwa akifanya jambo au mambo mazuri kwa matarajio ya zawadi na endapo kutakuwa hakuna zawadi hataona sababu ya kufanya hivyo

  Mtoto anapoambiwa kwa mfano kwamba akiwa wa kwanza darasani atapatiwa viatu, anakuwa anajengewa dhana kwamba viatu sio haki yake bali ni mpaka afikie matarajio fulani ya mzazi wake ili aweze kupata viatu.

  Kuna wazazi ambao huwaahidi watoto wao zawadi kama nguo, midoli, baskeli na vitu vingine vinavyofanana na hivyo, ambavyo kimsingi ni haki yake.

  Wengi wetu tumelelewa katika mazingira ya aina hii. Tulipokuwa wadogo wazazi wetu walishindwa kujua kwamba viatu, nguo, midoli na kadhalika ni haki yetu, bila kujali kama tumefanya vizuri darasani au tumefanya jambo lolote tulilopaswa kulifanya kwa ustadi mkubwa, kama walivyotarajia.

  Kwa mtindo huo wa malezi wametufanya tuamini kwamba ili tupate haki zetu ni lazima tufikie matarajio ya wazazi.
  Na sisi tumejikuta tunatumia mbinu hiyo hiyo katika kuwalea watoto wetu.
  Je? malezi ya aina hii yana athari gani katika ustawi wa watoto wetu?
  Labda hilo niwaachie wasomaji mtoe maoni yenu, kwani mimi hili linanitatiza¬Ö.
  Na: Yasinta Ngonyani kl. 9:48 AM 1 Maoni
  Etiketter: maisha, mtoto, zawadi
  Ushauri wako:

  Wednesday, June 3, 2009
  HAPPY BIRTHDAY OUR SON AND LITTLE BROTHER


  Tarehe hii ya leo imepita miaka nane tangu huyu kijana azaliwe. Sisi Familia yake tunapenda kumpa pongezi kwa siku hii. Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa ni Baba, Mama na dada yako ndio wanakupengeaza. Uwe na siku njema Erik.
  Na: Yasinta Ngonyani kl. 12:25 AM 14 Maoni
  Etiketter: Furaha, maisha, miaka, mkubwa
  Ushauri wako:

  Tuesday, June 2, 2009
  KISWAHILI
  Mara nyingi huwa nakasirishwa kuona / kusikia watu wanatumia vibaya baadhi ya maneno ya kiswahili. Hapa nimechukua au nataka kutoa mfano haya maneno matatu. Karibu, Jambo na Habari

  Karibu: Ni kuto kuwa mbali kwa wakati au mahali, kiasi cha kukadria. Lakini watu wengi wanaelewa zaidi karibu ni tamko litumikalo kuitikia hodi au wakati mtu anapokaribishwa au kupokewa mahali fulani.

  Jambo: Watalii wengi wanafikiri wanaweza kiswahili, kusalimia wasemapo jambo hawajui kwamba Kiswahili sananifu hutamkwa hujambo/haujambo/hamjambo? kwani ukisema hivi anashindwa kuitikia sijambo. Si afadhali hata wangefundishwa kusema hali yako.....

  Habari: Neno habari limekuwa linanitatanisha sana. Kama kawaida maneno mengi ya kiswahili yana maana mbili azu zaidi. (1) Habari ni melezo ya jambo fulani lililotokea, taarifa, ujumbe na ripoti.
  2) Habari hutumika katika kuamkiana na kuulizana hali. Lakini inaonekena wengi hatuwazi sana tunapoongea hili neno litumikeje.
  Na: Yasinta Ngonyani kl. 12:32 PM 6 Maoni
  Etiketter: afrika, kiswahili, lugha, raha, tanzania
  Ushauri wako:

  NANI AMESEMA MA-TRACTOR HAYABEBI WATU ULAYA? HII NI KUTOKA UINGEREZA

  Na: Yasinta Ngonyani kl. 9:56 AM 1 Maoni
  Etiketter: maisha, usafiri
  Ushauri wako:

  Monday, June 1, 2009
  JE? NI VIGUMU KUISHI BILA NGONO?
  Wengi tunajua/pia tunajadili ukimwi na ngono, lakini tunahitaji kukumbuka kuwa sio waTanzania wote ama binadamu wote ni hivyo. Cha muhimu ni kuelewa kuwa ugonjwa huu unaua binadamu, na kwamba, hawa binadamu wanatokea katika kila sekta ya maisha, wanadini, wapagani, wasio na elimu, wenye elimu, wamjini, wanavijiji, nk.
  Je? kuna ubaya gani kuwaelimisha wengine kuhusiana na matumizi ya ndomu?

  Tukumbuke ya kwamba baada ya Hawa na Adam kula lile tunda baya, sote tulizaliwa madhambini, na tunashawishika kirahisi. Yaani, hata Hawa na Adam , ghafla waligundua ya kuwa wako uchi, nadhani mle bustanini kulikuwa kuzuri na kulikuwa na hewa bora yaani jua lilikuwa haliwachomi, majani hayakuwakata.Walipofukuzwa ndio walilazimika kuvaa nguo kwa sababu ya jua kali, mavumbi, miiba nk. Hakuna aliyewaamrisha kuvaa nguo.

  Ngono inashawishiwa maishani kwa mbinu nyingi ambazo ni vipofu tu wasioziona. Katika magazeti, mavazi, sinema, hadithi za waliojaribu, umbea nk. Ni kama vile Hawa na Adamu, walivyoshawishika kula lile tunda hata walivyojua Mungu wao aliwakataza, lakini sisi wengine tunashawishika kirahisi kula hili tunda liitwalo "ngono". Wote tunajua tukishalionja tunda hata yeyote akikuambia "basi acha" wengi tunacheka ana kushangaa? Hii in kama vile mtoto akishaonja pipi, halafu ategemewe kutotamani pipi mbeleni.

  Pipi zitakuwepo duniani kwa miaka mingi, vishawishi vya ngono vitakuwepo duniani kwa miaka mingi. Hii ndio sababu tunahitaji kuelimishwa kuwa pipi si nzuri kiafya. Lakini pia tunahitaji kuelimishwa kuwa wale watakao tamani basi wale nyingi na wasisahau kupiga mswaki. Naamaanisha, ujumbe wa kuacha ngono uambatane na ujumbe wa kupunguza kufanya ngono na watu wengi NA elimu ya kutumia ndomu.
   
 2. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Neither!

  Kumpa au kumuahidi mtoto zawadi pale unapoona anastahili ni kumpa motisha. Ikiwa watu wazima wanapewa zawadi kuwamotisha, kwa nini watoto wasipewe pia?

  Kibaya ni kile unapomuahidi mtoto zawadi wakati unajua kuwa huwezi kufanikisha ahadi hiyo. Hii ni moja ya tabia mbaya sana kutoka kwa wazazi kuwafanyia watoto wao. Haijalishi mtoto ni mdogo kiasi gani, unapoahidi zawadi ni lazima uitekeleze. Vinginevyo hakuna haja ya kuahidi. Well, kama kuna sababu ya msingi ambayo imekufanya umeshindwa kufanikisha ahadi, basi hakikisha unaifafanua kiukweli kwa mtoto wako. Mtoto ni binadamu. Anasikia maumivu pia. Kukausha au kumdanganya ni kumuumiza moyo. Usipende kumweka doa la maumivu moyoni mtoto mdogo. Hatalisahau maishani mwake mwote!
   
 3. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2014
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kumpatia mtoto zawadi sio kitu kibaya. Ila kuna mambo ya lazima ambayo haipaswi kuhaidiwa kwa mtoto Kama motisha ya yeye kufanikisha Jambo Fulani kwa ustadi wa hali ya juu zaidi. Inatupasa tukubali Kwamba kuna mambo au vitu ambavyo Kama wazazi ni jukumu letu tuwapatie watoto wetu bila ya kujali wamefanya Jambo gani kwa ustadi/ubora zaidi.
   
 4. Makamee

  Makamee JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2014
  Joined: Nov 29, 2013
  Messages: 2,005
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Pdidy wa enzi hizo kumbe alikua makini sana.
   
 5. Moisemusajiografii

  Moisemusajiografii JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2014
  Joined: Nov 3, 2013
  Messages: 6,408
  Likes Received: 4,620
  Trophy Points: 280
  Mbona jamaa alikuwa katulia sana,makini,gt hasa!Kumbe nini kimemsibu siku hizi?Natafakari.
   
 6. Makamee

  Makamee JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2014
  Joined: Nov 29, 2013
  Messages: 2,005
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Itakua mtu amechukua id yake.
   
Loading...