Kumuacha Idd Amin dada afe kifo cha asili tulifanya mfano mbaya sana kwa madikteta

Sasa mauaji ya wananchi wake aliyofanya amini ulitaka aachwe?
mambo ya ndani ya nchi hayo, Uganda ni nchi huru, si ndio wanajibu hapa Tz wakikosolewa? kwani Nyerere hakuwa mbabe pia kwa watu aliowaona wanampa challenge kisiasa? Nyerere ana tofauti gani na akina Obama aliyempimdua Ghaddhafi madarakani kisa alikuwa akiua raia wake ambao Magufuli na nchi nyingi za Afrika kila siku zinapiga kelele kulaani kuwa ni mabeberu?
 
Hawa wote walikuwa madikteta wakitofautiana styles
Mpaka sasa hakuna sababu makini ya vile vita, ndio maana hata walio take over akina M7 na PK bado wana u Dictator
Hivi Idd Amin ana tofauti gani na M7 au PK ?? na wote walikuwa trained hapa kwetu

Achana na Idd Amin ambaye ameishakufa jee M7 na PK nao wafanywe nini ????
Idd Amin alikuwa ni dikteta kichaa kichaa, asietabirika..Kagame na Museveni ni madikteta ila wapo stable kichwani
 
Hapo alipopatia ni wapi? Kuvifadhili vikundi vya kiasi vya kina obote wakati wa utawala wa Amini kule Uganda?
Kuifadhili ASP na kufanya Mapinduzi kule Unguja?
Au kumuhifadhi Kabila?

Mkuu kati ya Iddi Amini na Obote nani alikua Muasi?
 
kwangu mimi idd amin ni rais ambaye anapaswa kuigwa........acheni kudanganywa na mikanda ya propaganda ndo mtaelewa kwanini nasema idd amin ni rais wa kuigwa
Kwa hizi line nne Za sentence. Ndio unataka ubadili fikra hizo

Fungua MA Paragraph hapa tuone mazuri yake tujue Kweli tulikua tunadanganywa.
 
Habari wakuu,

Kitendo cha kumuacha idd amin dada akimbie na kumuacha mpaka afe kwa amani kilikuwa ni mfano mbaya sana kwa madikteta, sasa madikteta wanajua wanaweza kuichezea nchi yetu na wakakimbia bila kuchapwa, huu ulikuwa ni mfano mbaya sana, kosa kama hili tusilirudie tena
Asanteni
Hukupata wasaa wa kukaa nae ukasikiliza maelezo yake,hukupata kukaa na waganda chini ya utawala wa Amin ukawahoji,maneno yako ya bias kwa kuwa umesoma tu historia ya upande mmoja! Ni sawa na sheikh kuombea kitimoto wakati kwa imani ya kiisilamu ni jambo lisilokubalika! Rudi kwenye maandiko, pitia historia za pande zote za mgogoro kisha uje kuedit bandiko lako!
 
Sawa mkuu 😂😂
 
Sawa mkuu 😂😂
Amin alikuwa muungwana na muwazi kwa kuwa alikuwa anaua wazi na kuzika wazi. Museven anaua kwa siri na kuzika kwa siri so kutojua kwamba anaua haina maana kwamba yeye ni mzuri kuliko Id Amin! Kilichotokea ilikuwa vita vya ubepari na Ujamaa na ukiwa ni mfuatiliaji mzuri wa historia utakumbuka Amin alipata support kubwa sana na mataifa yaliyokuwa na policy ya ubepari wakati mjamaa Nyerere akisimama mwenyewe kwa kuwa marafiki zake waliokuwa na Ideology ya Ujamaa walikuwa wanachechemea kama sisi. Asante!
 
Asante kwa elimu
 
Wakati Iddi Amini akiwa raisi Obote alikua ni muasi.

Hivi labda nikuulize tu, Kwa mfano Kambona angetimkia Kenya halafu akawa anasaidiwa na Kenyata katika mapambano ya kujaribu kumuondoa Mwalimu madarakani hivi wewe unahisi Serekali ya Mwalimu ingelichukua maamuzi gani?
Tulikosea kumpokea obote kama mkimbizi kwenye nchi yetu
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom