Kumuacha Idd Amin dada afe kifo cha asili tulifanya mfano mbaya sana kwa madikteta

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,707
71,003
Habari wakuu,

Kitendo cha kumuacha idd amin dada akimbie na kumuacha mpaka afe kwa amani kilikuwa ni mfano mbaya sana kwa madikteta, sasa madikteta wanajua wanaweza kuichezea nchi yetu na wakakimbia bila kuchapwa, huu ulikuwa ni mfano mbaya sana, kosa kama hili tusilirudie tena
Asanteni
 
Duh..Aliyemfukuza ni Nyerere ila jamaa alikuwa na marafiki wenye nguvu tu na walikuwa wakiona yupo sawa Gadafi anayetajwa sana ni mzuri alimtumia shehena ya silaha Saudia walimpa hifadhi

Nyerere naye alikuwa akiingilia mataifa ya watu na kupindua serikali zao huku akizituhumu zimemchokoza kama Marekani inavyofanya,
Alipindua Serikali ya Uganda ikiwa huru, Serikali ya Zanzibar ikiwa huru, na akaunga mkono waasi huko Nigeria waliotaka kujitenga
Wafuasi wake watasema alikuwa anafanya kwa nia njema ila kwenye siasa kila mtu akifanya kitu anadai anafanya kwa nia njema
 
Pia makosa makubwa sana yanafanyika kuwaacha wachochezi kama wewe amini nawaambia watakuja teketeza taifa.Mbona wanaoumwa kipindupindu tunawatenga na wazima kwanini wenyefikra kama hizi wasichomwe moto?
 
Pia makosa makubwa sana yanafanyika kuwaacha wachochezi kama wewe amini nawaambia watakuja teketeza taifa.Mbona wanaoumwa kipindupindu tunawatenga na wazima kwanini wenyefikra kama hizi wasichomwe moto?
Mkuu sasa hapa nimechochea nini?, acha uchonganishi
 
Back
Top Bottom