Kumteka na kumtesa Ulimboka ingekuwa Tunisia au Libya ingekuwaje?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Kila mwenye uchungu na Tanzania analaani kitendo cha kijinga na kihuni alichofanyiwa dk Steven Ulimboka mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari. Hivi watanzania wataendelea kutumiwa na kila atakaye kulinda kitumbua chake hata kwa kuwatoa roho? Je kumteka na hata kumuua Ulimboka ndilo jibu wanalotaka madaktari? Je hapa haki ya kila mtanzania kufaidi ulinzi iko wapi iwapo watu tena wanaolipwa pesa ya umma wanaweza kuingilia haki za wengine na hata kutishia maisha yao? Tusaidiane na kujifunza toka kwa wenzetu. Je hii ingetokea Misri au Tunisia hali ingekuwaje?
 
watz wote tulaani kitendo hiki kinachokwenda kinyume na haki za binadamu.inachoonekana hivi sasa ni kuwa serikali imeshindwa kutatua kero za wananchi na sasa kila aliye 'kimbelembele ' kudai haki, sina shaka hiki ndicho kitakuwa kinampata.lakini, ninajiuliza, hata lini serikali na chama chake wataendelea kutumia mbinu hizi chafu? ni wazi sasa kuwa kadiri inavyotumia njia haramu kuzima harakati zozote za ukombozi, ndivyo mwamko wa watz utakavyozidi, hence, mwisho wao u karibu.
 
Kila mwenye uchungu na Tanzania analaani kitendo cha kijinga na kihuni alichofanyiwa dk Steven Ulimboka mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari. Hivi watanzania wataendelea kutumiwa na kila atakaye kulinda kitumbua chake hata kwa kuwatoa roho? Je kumteka na hata kumuua Ulimboka ndilo jibu wanalotaka madaktari? Je hapa haki ya kila mtanzania kufaidi ulinzi iko wapi iwapo watu tena wanaolipwa pesa ya umma wanaweza kuingilia haki za wengine na hata kutishia maisha yao? Tusaidiane na kujifunza toka kwa wenzetu. Je hii ingetokea Misri au Tunisia hali ingekuwaje?

wamisri wangalliitwa magaidi humu ukumbini
 
hiyo sio njia ya kutafuta suluhu bali kuongeza hasira za madaktari , lazima serikali ikae na itafute njia mbadala kuliko kufanya kitu kama alichofanyiwa dokta.....
 
Ila kama kweli kitendo hiki kimetokea, haki ya Mungu Tanzania imekwisha na sijui viongozi tunaotegemea kutulinda wanafanya nini na au hivi vitendo vya kihuni.
 
mambo haya hata tunisia waliyavumilia,ila baada ya mda,hali ikawa kama ilivyo sasa.tusipofanya maamuzi sie ni yunisia ya miaka ijayo.
 
HAWA MIJIMBWA ILIYOTUMWA KWENDA KUMLIMBOKA dr ULIMBOKA WAO WATAISHI MILELE?
 
Back
Top Bottom