Kumtegemea Rais kupata majibu ya kila tatizo la nchi ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumtegemea Rais kupata majibu ya kila tatizo la nchi ni sawa?

Discussion in 'Great Thinkers' started by WomanOfSubstance, Jul 23, 2011.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kitu kinachoniumiza kichwa hasa kwenye tatizo la umeme ni kujaribu kuelewa ni nani mwenye "suluhisho la kudumu" la kumaliza hili tatizo sugu kwa kila awamu ya urais hasa awamu hizi mbili za mwisho.

  Rais wetu keshasema yeye hana uwezo kumwambia Mungu anyeshee mvua mabwawa yajae, umeme uzalishwe.Fair enough na ni kweli.Kwanini tunadhani rais ndio mwenye "ufunguo" wa kufungua mlango/milango ya utatuzi? Je hiyo milango ni ipi, iko wapi?

  Nilimsikiliza kwa makini Mh John Mnyika akielezea kwa ufasaha tatizo lilivyo na baadhi ya njia za kulitatua na kwamba inahitajika ushirikiano baina ya wadau wote - serikali, kambi ya upinzani na hata sekta binafsi kukaa pamoja na kuweka vichwa pamoja kupata suluhu. Hapo nilijiuliza, kwanini hili halifanyiki?

  Nimekuwa pia nikisikia mara kwa mara serikali ikilaumu upinzani kwa kutokutaka kutambua mazuri yanayofanywa na serikali na badala yake wanapinga tu.Je ushirika huu wenye manufaa kwa watanzania badala ya vyama, ushirika unaohitajika wakati huu kuliko wakati mwingine wowote si ndio ungeonyesha namna gani vyama vya siasa vinavyoweza kuweka tofauti zao kiitikadi na kuweka ajenda ya taifa mbele na maslahi ya wananchi juu ya maslahi binafsi ya wanasiasa?

  Hivi ndugu zanguni, hivi vyama vya siasa viko kwa manufaa ya nani? Ikumbukwe kwamba wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa ni wachache sana hawazidi hata nusu ya watanzania wote wanaoathirika na hili tatizo la umeme.Je serikali inawatendea haki gani wale wasio wanachama wa chama chochote wanaolipa kodi zao wakitarajia huduma mbalimbali ikiwemo umeme.

  Naombeni mnisaidia kupata majibu ya hayo maswali na labda wanasiasa na viongozi wa serikali wanaopita humu JF nao watusaidie sisi wananchi tuliokaa pembeni tukiangalia hili igizo kuelewa.

  Asante kunisoma na pia kutafakari na hata kuchangia.

  ANGALIZO: Ukiona mada inakukera basi potezea tu badala ya kuweka hasira na maneno yasiyo ya lazima.
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata sijaona swali hapo zaidi ya maelezo mareeeeefu yaliyopindapinda kama Mizengo
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Pole sana ndugu..kweli hujazoea maswali bali amri tu!
  Alama hii "?" unaielewa? Kama ndio umeiona mara ngapi. Tafakari kisha chukua hatua!
   
 4. u

  ugawafisi Senior Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tutafakari nini wakati wewe mwenyewe hujatafakari kabla kuandika? Unauliza swali, unalijibu ww mwenyewe halafu unalipinga. Du!
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  hahahha kweli hili giza linaleta mambo! Hasira utadhani mimi ndio nimekuzimia umeme! Lol!! poleeeee!

  Tuko pamoja ndugu!
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Dada WoS,

  Kama kawaida heshima mbele. Natumai umzima na unaendelea vyema na shughuli zako. Mimi nitakujibu kama ifuatavyo.

  Kwa Tanzania ndiyo. Kuna msemo wa Kiingereza usemao "With great power comes great responsibility." Nchi kama Tanzania hatuna checks and balances. Raisi anauwezo wa kuteua watu wake toka juu (waziri mkuu, mawaziri nk) mpaka chini (Wakuu wa wilaya nk). Pia Bunge linaongozwa na chama chake ambacho kila siku tunaona sera za serikali zikipitishwa kwa "Ndiyooo, nakubaliana kwa asilimia 100". Sasa dada WoS kwenye nchi ambayo raisi ana nguvu zote hizo tumuulize nani? Kila ambae anapaswa kuulizwa kateuliwa na raisi tena bila vetting yoyote ya Bunge. Sasa kama una nguvu ya kuteua watu wako from top to bottom iweje usiwe na majibu?

  Waziri wake mwenyewe wa Nishati na Madini alisema tatizo la umeme litakua historia ifikapo June mwaka huu. Akabadilisha tena tena na kusema ni mpaka 2015. Sasa wakati serikali yake ilivyo kuwa inatuambia tatizo la umeme litakua historia ilikua inajua raisi wake si wingu? Ahadi wanazitoa wenyewe. Kumbuka dada ahadi ni deni.

  Sijawahi ona upinzani wowote duniani unaosifia sifia serikali wala chama kilichopo madarakani. Nia na madhumuni ya kuwa mpinzani ni kuonyesha kwamba wewe unaweza fanya kazi nzuri zaidi ukipewa nafasi. Sasa ukisifia sifia ina maana una kubali kazi inayofanywa na chama tawala kwa hiyo wananchi hawana haja ya kukukabidhi wewe madaraka. Pia kazi ya upinzani ni kuipa serikali changamoto na changamoto hizi ni kutoa njia mbadala kwa kusema hata kama umefanya hivi ungefanya hivi ingekua vizuri zaidi. Lakini pia CCM isiwe wanafiki. Ni wao lini wamekubali mazuri ya upinzani? Ni mara ngapi wabunge wa upinzani wanatoa hoja nzuri lakini hupingwa kisa tu imetolewa na upinzani? Wao kusifia hawataki lakini kusifiwa wanapenda???

  Kila chama ni kwa manufaa ya wanachama sijui kwa nini hii tunaona haiapply kwa vyama vya siasa? Kwa mfano chama cha wafanyakazi kipo kwa ajili ya kina nani? Chama cha walemavu? Chama cha walimu? Ukichunguza vyama vyote vipo kwa manufaa ya wanachama wake. Huo ndiyo ukweli.
   
 7. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Goosh Sounds like interview ya JK na BBC!
   
 8. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kikwazo kikubwa katika utatuzi wa matatizo yanayoikabili nchi hii si tu umeme, ila hata Muungano, Maisha duni ya wananchi/wafanyakazi, ufisadi, mauaji haramu ya raia, Elimu duni (awali na vyuo), afya to mention few ni "dakta" JAKAYA MRISHO KIKWETE.
  Hataki walau kufuata, let alone kusikiliza,ushauri wenye malengo mazuri kwa Tanzania. Remember ndo yeye kashika kila mpini wa maendeleo na uharibifu wa Nchi.
  Kukujibu ni kuwa: Ndiyo tumtegemee kupata jibu la kila tatizo Tanzania.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
   
 10. k

  kamimbi Senior Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais hausiki na hili, kunawizara ambayo inashughurikia mambo hayo, hawa ndo wachawi wa tatizo kwasababu hata JK mwenyewe akitaka kujua nini kinaendelea juu ya utata wa umeme lazima awaulize wahusika wa wizara hiyo ndo anapata kujiamini kwa majibu atakayoyatoa, Kwani Ngereja na Jairo wao wanalizungumziaje suala hili? wakuu mi nadhani tuanze kumtafuta mchawi wa umeme ndani ya mjengo wa umeme (wizara husika).
   
 11. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Kwa mfano nikikosa pesa ya kununua luku ni tatzo langu lakini kama nina ela yangu alafu nchi iko gizani hatupati umeme hapo rais anatakiwa kuwajibika kama mkuu wa nchi..Yap!!
   
 12. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Kwa mfano nikikosa pesa ya kununua luku ni tatzo langu lakini kama nina ela yangu alafu nchi iko gizani hatupati umeme hapo rais anatakiwa kuwajibika kama mkuu wa nchi..Yap!!
   
 13. nzumbe

  nzumbe Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali yote kwa ujumla imeajiriwa na sisi wananchi, na ndiyo maana tumewachagua na kuwaweka hapo juu waweze kutuongoza!!.. Sasa wizara husika inatakiwa kuwajibika na si kumtoa kafara katibu wao!!.. waziri na naibu waziri pamoja na waliobakia wooote kwa ujumla wawajibike...
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Tumeshasikia mengi kuhusu kisa na mkasa wa kukosa umeme- kuanzia TANESCO na mapungufu yake hadi wizarani.Siamini kama ni tatizo la mtu mmoja kwenye hizi taasisi maana wengi wamekuja na kulikuta tatizo. Kumbuka Ngereja kama Waziri kaongoza Wizara hiyo siyo zaidi ya miaka mitatu kama sikosei. Kabla ya hapo walikuwepo wengine waliojiuzulu.Kabla yao walikuwepo wengine akiwa ni pamoja na Mh.Rais wetu wa sasa.Kadhalika TANESCO nako hivyo hivyo. Mchawi tunampataje? Hapa tunaongelea tatizo la kimfumo ( systemic) na ninavyoona mimi, kutaka Waziri Ngeleja au MD wa TANESCO wajiuzulu kisa kukosekana umeme ni kuwaonea.Labda tupembue zaidi tuone huo uwajibikaji wao kwanini uwabane wao tu ilhali wao walikuja wakalikuta tatizo?
   
 15. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Oktoba 31, 2010 tulikimbilia kwenye ballot box. yeye akatumia silaha ya juu.
  Options-
  1. Barabarani.
  2. Mwituni- hoping TPDF inasplit otherwise refer to option 1.
  Kikwete and his filthy regime has to go if Tanzania is to move. He is expendable.
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  "Ningekuwa ni mimi,ningekuja hapa na kutoa uamuzi maana hili halivumiliki,lakini protocol zinanizuia ngoja nimsuburi mh atue nimwambie hii habari"---JIPANGE MKUU
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  WOS,

  First off i do respect you.

  However nadhani una ujuzi zaidi kwenye yale majukwaa mengine.(You know what i am talking about)
  Thread yako hii inaonyesha kutokuelewa masuala ya kiutawala na siasa.Soma katiba kidogo utagunduwa ni kwanini the bucks stops with Mkulu/Rais.

  Mada hii haijanikera kwasababu kutokuelewa kwako si kubaya sana,utaweza kueleweshwa tu kwasababu kuna tutakaofanya hivyo.We know you are a smart lady,you just need a little bit of brushin' in this arena.

  Nchi yetu imeingia kwenye mfumo wa vyama vingi just recently,na CCM wana majority all the times huko bungeni kama ni kweli wanataka ama walitaka kupitisha maamuzi muhimu na yenye tija ili kutuondoa kwenye hii dhahma ya ukosefu wa umeme.

  Pia kwamba tatizo hili halikuanza leo,hilo nalo limekuwa ni kama sababu ya kujitetea ya viongozi wetu.

  Tatizo letu ni kwamba hatuna katiba ya kuwabana.Tunaweza kuweka ultmatum kwamba if you can't fix this problem,then we will fire you right away!Rais ni lazima aulizwe kila kitu,si kazi rahisi kuwa rais wa nchi masikini.Ni dedication,unaweza kufa kwa presha kama kweli umeingia madarakani kwa dhumuni la kuiongoza nchi yetu na kuindoa kwenye umasikini.

  Imenisikitisha wewe kuja na kauli kuwa it is fair enough for the president to say that he is not capable of asking God to provide us with rain.Hii si caliber ya great thinking.Nasikitika kwamba ulianza kuwa defensive na kudai watu wasiweke maneno yasiyo ya lazima.I hope you will be patient and read what you dont like without getting personal.

  Nchi haiendeshwi kiimani na hatutarajii majibu ya kiimani mara baada ya kuingia ikulu.Hivi unadhani angetoa jibu sawa na hilo kama angekuwa ni wakati wa kuomba kura?Inasikitisha sana kuona kwamba sisi watu wa level hii hatuelewi,sasa vipi kuhusu hao wananchi lukuki wasiojuwa hata internet ni nini na hata kura hawapigi?Wasio juwa haki zao za kiraia?Umeme ni anasa na hata milo miwili kwa siku?aagh!

  Narudia tena dada yangu,hii issue si ya vyama vya siasa kama unavyotaka kuiweka.Tafadhali elewa kuwa tatizo si kutokuweza kwa JK kumwuliza Mungu kuhusu mvua(Tafadhali elewa hilo)

  Kama unaelewa hilo la Mnyika,then fuatilia alichojibu Mh Rais pale alipoullizwa kuhusu hilo.Akisema Mnyika aweke maarifa yake.Sasa wewe nileze kama hiyo hotuba ya Mnyika ina constitute maarifa ama la,then come back up here and tell me if you have changed yout mind or no.Mh Rais alikejeli.Sasa labda ungemsaidia na kumwambia next time aseme yeye hatakiwi kuulizwa kila kitu.

  Wewe unapoamini kuwa rais hatakiwi kuwa na majibu ya kila tatizo,unakuwa kama na wewe una tatizo la kuelewa kuwa issue ya umeme si just "Kila tatizo"

  Tunahitaji viongozi wenye priorities za kitaifa.Hi tatizo sugu na lilitakiwa lipewe kipaumbele na si majibu rahisi rahisi na majibu wa siasa kukwepa maswali magumu kwa kudai eti "Si kila tatizo la nchi linahitaji majibu ya rais"

  Unajuwa nchi ya marekani ilivyo kubwa na karibu kila tatizo rais wake anaulizwa?Na tena i mean almost everything,sasa nchi yetu masikini,na hivyo karibu kila tatizo tulilonalo ni la kimsingi.Matatizo ambayo ni lazima tuyashughulikie otherwise hatutaweza kus survive as a nation.

  Kwa kumalizia,naomba usijali kuhusu baadhi ya maneno niliyoyatumia kama utakuwa hujayapenda.
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Dah! Hivi kulikuwa na ulazima wa kuyasema yote hayo?
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Ndiyo,umemwuliza kama na yeye alikuwa na ulazima wa kuyasema hayo yote?Ama na wewe ni super hero?Huko kwenye majukwaa yenu si kwangu.Humu nipo.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Jul 23, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Uncalled-for hubris!
   
Loading...