Kumtegemea mtu mmoja ni tatizo, ACT Wazalendo inaweza kufa baada ya Maalim Seif kufariki

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,598
141,415
Maalim Seif alikuwa ndio nguzo ya CUF na alipohama CUF nayo ikawa imekufa " kimsingi " Maalimu Seif akawa nguzo ya ACT Wazalendo ambayo wabunge wake wote ni wafuasi binafsi wa Seif. Kufariki kwa Maalim Seif kunaweza kuwa ndio mwanzo wa kifo cha ACT Wazalendo pia.

Lakini naamini Mwamba Zitto Kabwe atawavusha ACT Wazalendo.

Poleni sana ACT Wazalendo, Zanzibar, Wapinzani na wananchi wote wapenda amani Tanzania.

Maendeleo hayana vyama.
 
Kwani si alihamia?

Yeye ndo mwanzilishi?

Akiondoka Zitto itakuwa ndiyo msiba wa ACT
 
Babu Duni, Jussa, na wengine wataisogeza mbele ACT, mtu kufariki dunia sio jambo la kumaliza vyote alivyokuwa akiviongoza au kuvisimamia, ila kama hilo likitokea basi utakuwa ni uzembe wao viongozi kwasababu kama ni mtaji wa wapenzi na wanachama bado wanao.
 
CCM iko madarakani kwa kutegemea msaada wa yombo vya dola. Bila wizi wa kura leo CCM ingelikuwa maiti. Jiwe akidondoka tu, CCM imekufa, maana imewakatili wengi, hawasemi kuogopa matokeo. ACT imeanzishwa na Zito, siyo Maalim hivyo it is there to stay! Nakubaliana na wewe kuwa Maalim alipendwa sana ZB, kupata mtu wa kumrithi might take time.
 
Sure
 
Back
Top Bottom