Kumtazama Lissu kwa jicho la dharau kunakofanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali, ni kufanya kosa kubwa sana la kiufundi!

Omary Ndama

JF-Expert Member
Apr 16, 2017
3,368
4,056
Nami nimeona nitoe mawazo na mtazamo wangu kama raia huru juu ya mijadala inayoendelea kushika kasi mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kumhusu Lissu! Binafsi nimekuwa mtazamaji tu na mfuatiliaji wa kinachoendelea! Ila nimeona kuna jambo wengi wanashindwa kuling'amua juu ya huyu Lissu! Jambo hili ni Udharula wa kifo chake!

Inawezekana wengi hata wenye Mamlaka kuna jambo la msingi hawajalitafakari vyema! Na jambo hili linawafanya wengi kumchukulia Lissu kawaida sana! Kuna jambo hapa la kutafakari!

Yaani imetokea binadamu mwenye nyama na damu kama wanadamu wengine wenye damu kapigwa risasi 16 (madaktari wamethibitisha hili) sehemu mbalimbali za mwili wake- hakufa hapohapo! ni ajabu! Katika harakati za kutibiwa ili asife baadaye, akajikuta ananyimwa fedha za matibabu na mamlaka inayohusika, Lakini kingine cha ajabu ukavuma upepo tu wa michango akatibiwa kwa michango ya wasamaria wema!!!. Hivyo kumfanya kuwa hai mpaka leo! Kuna nini katika hili? Ukilitazama jambo hili kwa utulivu na tafakuri kubwa huku ukijiweka kando ya ukereketwa kwa muda.... Utagundua lipo jambo nyuma ya pazia!! Jambo hili ni jambo gani? Hapo sasa wengi tunajikuta hatuna majibu sahihi, wengine wanajaribu kugawana fikra kwa miono tofautitofauti- Ambapo nimewasikia wengine wakibuni kupona kwake kuna lengo la yeye kukusudiwa kushika nafasi kubwa kabisa ya kisiasa nchini! Hata Mimi sina hakika! Ila nina uhakika kuwa, kupona kwa Lissu kuna sababu kubwa sana! Ukubwa wa sababu hiyo unalingana na ukubwa wa muujiza wa kupona kwake! Hata kama sababu siyo hiyo inayotajwa, hakika ipo sababu kubwa ya kupona kwake' yawezekana ikawa sababu kubwa zaidi ya hiyo inayotajwa! Muujiza huu wa Lissu unatafakarisha, Huu ni muujiza hakika! Ni muujiza wa aina yake na wenye makusudi ndani yake! Lissu ilikuwa afe kama walivyokufa wengine katika mazingira yanayofanana na ya kifo cha Lissu kilichoshindikana! Malango ya mauti yalifunguliwa wazi mbele yake yammeze, lakini Mungu aliizuia mauti ya Lissu kwa sababu kulitokea Dharula Duniani ya kufanywa na Lissu kabla kifo chake hakijaruhusiwa! Mambo ya kiroho yanalitanabaisha hili, Lipo jambo Lissu alibaki ili alifanye!

Kwa sababu hizo kuna haja ya wanaompuuza Lissu kulitazama jambo hili upya kwa jicho la Kiroho na kidadisi zaidi!! Kwa mazingira ya kupona kwake, Lissu anabaki kwenye Kundi la watu waliowahi kukutana na muujiza mkubwa hapa Duniani!

Kumtazama Lissu kwa jicho la dharau kunakofanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali, ni kufanya kosa kubwa sana la kiufundi! Dunia inaendelea kumuamini Lissu kuwa serikali ya nchi yake ndiyo iliyompiga risasi zote hizo kwa lengo la kumuua! Ushahidi pekee wa kimazingira anaoutoa unaonekana kuwa na nguvu ukizingatia kuwa Serikali mpaka sasa bado haijatoa ushahidi wowote kupinga madai ya Lissu hata kujishughulisha na raia wake huyu! Suala la kutaka kumzuilia stahiki zake za kibunge ni mtego mwingine kwa serikali ambao nafikiri Lissu anatamani jambo hili lifanyike ili kuongezea nguvu ushahidi wake! Jambo hili la Lissu kuzunguka huku na kule kuielezea Dunia kilichomtokea na kuituhumu serikali ya nchi yake! Watendaji wengi wa serikali wanamuona kama kichaa anayedhurula kama wanavyomuita! Lakini wanakosea sana kwa sababu madhara kwa serikali ya anachokifanya Lissu sasa yatakuja kuonekana mbele tuendako.

Wengi wanashindwa kujua kuwa, kama kifo kimeshindwa kumnyamazisha Lissu' hatanyamazishwa kwa kumnyang'anya mshahara wake, hatanyamazishwa na maneno makali ya akina Makonda wala hatanyamazishwa na kejeli za akina Msukuma!

Dawa pekee ya kumnyamazisha Lissu huko Duniani aliko ili aachane na kuituhumu serikali yake, dawa hiyo aliyenayo ni serikali yenyewe kujishughulisha na suala la Lissu ikiwa ni pamoja na ;

1.Serikali kutoa ushahidi usio na shaka wa mtu halisi aliyehusika kumshambulia Lissu

2. Serikali kuieleza Dunia walikokuwa walinzi waliokuwa zamu kulinda nyumba za serikali wakati Lissu anashambuliwa.

3. Serikali kuieleza Dunia zilikokwenda CCTV camera baada ya Lissu kushambuliwa.

Kwa nini serikali ndo inapaswa kuwa na majibu haya? Kwa sababu ndo pekee ina mamlaka ya kutoa majibu hayo na si mwingine!!! Hayo ndiyo maswali pekee ambayo Lissu amekuwa akiyauliza kila kwenye chombo cha habari cha kimataifa anachoalikwa!!

Serikali isipoamua kujishughulisha na suala hili la Lissu! Udharula wa kifo chake utaisumbua sana serikali.

Wasalaam!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4.Pia serikali ieleze kwanini haikumpatia haki ya matibabu kama ilivyofanya kwa wengine mfano Job Ndugai,Sitta nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni utani, kuna watu wanadhani ni sinema ambalo limechezwa na lissu mwenyewe?? Hebu wacheze la kwao watumie tu hata kisu tuone!!
Sioni jambo ambalo linaweza kufanyika kati ya hayo matatu
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom