Kumtaja Rais kila mara hata kwa vitu vya ovyo ni aibu, tujirekebishe

Mkuu natunga na wimbo wa Kumsifia Rais wetu we mleta mada njoo tuimbe huku!

Tunajivuna tunaye Samia wa Tanzania!×2

Tunajivuna tunaye Samia wa Tanzania!×2

Ooh Samia aah Ooo Samia wa Tanzania×3
 
Namshukuru sana aliyeleta mada hii leo! Imenikera sana kwa miaka sita na bado wameendeleza katika awamu hii!
Je makampuni yakijenga daraja ama barabara tunataja jina la mkurugenzi???
Mbona tunasema Azam, CRDB, EXIM! ASAS na kadhalika!
Awamu zote isipokuwa ya mwendazake na hii ya sita tulizoea kusikia “serikali imeagiza ama imefanya hiki na kile””
Kwa mfano wakati wa Mlm Nyerere sikuwahi kusikia Nyerere kajenga daraja. Ilikuwa ni serikali na ni vema iwe serikali kwani neno serikalili linajumuisha wananchi!!
Ninasikitika kuona wanataka kuendeleza mambo mabaya ya awamu iliyopita!!
Please stop it inawaaibisha!! Inatuaibisha wote!!
Tunakuwa kama watoto wadogo!!
Baba amenunua shati, baba amenunua nyumba lakini hapa ikiwa na maana afadhali ijapo mama hatajwi!!
Lakni kodi zetu anapewaje Rais halafu useme ni ya rais na ndiye kajenga??????
Ndiyo maana hakuna maendeleo ta watu binafsi Tanzania. Wananchi wameaminishwa kuwa ni rais anaywrakiwa kuwalisha, kuwabeba, kuwapa dawa, nk.
Tuwe wakweli tuwaambie wananchi kuwa serikali imehenga kwa kodi zao na imeshindwa kujengakwa sababu kodi zao hazikutisha!!

Hapo watu watajua faida ya kodi na watahenga ownership na kutunza raslimalu yao!!


Please stop it!!!
Hii tunaita 'unyumbu' ambapo tunaodhani wanauwezo mzuri wa kufikiri wanapo acha kutumia akili zao wenyewe, badala yake kufwata mkumbo 'kutumia akili za wengine'
 
Wanaoongoza katika hilo ni Majaliwa, Msigwa (wa habari) na Ummy!! Hadi wanakera sometimes, kila kitu Mama Samia kasema hivi, katoa hela hii, kaagiza hili, kajenga kile!! Kujipendekeza kulikopitiliza
 
Hakuna serikali ya rais fulani hapa.
Serikali ni ya wananchi.Sijui watu wanajipendekeza ili wapate nini!Tuache ujinga na woga uliopitiliza.
Basi Baki na ujinga wako,subiria chadema waingie ikulu ndio uje useme serikali ya wananchi
 
Umaskini wetu uko kila mahali hadi kwenye akili..Tuna umaskini wa fikra,elimu na kipato alafu matajiri wa unafiki,majungu,tamaa na mengine yafananayo.Kwahiyo usishangae hayo.Ni matokeo ya jinsi tulivyo.
 
Umaskini wetu uko kila mahali hadi kwenye akili..Tuna umaskini wa fikra,elimu na kipato alafu matajiri wa unafiki,majungu,tamaa na mengine yafananayo.Kwahiyo usishangae hayo.Ni matokeo ya jinsi tulivyo.
Na kuchukia wenye mawazo chanya yanayoijenga jamii
 
Basi Baki na ujinga wako,subiria chadema waingie ikulu ndio uje useme serikali ya wananchi
Acha upumbavu.
Mimi sishabikii chama chochote cha siasa kwa sababu hakuna hata kimoja kinachonisaidia chochote kwenye maisha yangu.Wote wanapigania matumbo yao tu.
Kama hiyo chadema yako inakuletea unga ndani endelea kuwapigia debe.
 
Kuna baadhi ya vitu yani kama ni binadamu wa kawaida kabisa vinatia kichefuchefu sana.

Hivi ni kweli kwamba kila kitu kinachofanyika katika nchi hii na vingine ni vya aibu na vingine wala Rais hauhusiki ktk kuvifanya , Je ni lazima kumtaja. 'Rais anakwenda kufanya. Rais anakwenda kufanya..'

Hivi ni kweli kwamba Marais wa nchi hii wanataka kuwa acknowledged namna hiyo hata kwa vitu ambavyo vinatia aibu. Hii si sawa kabisa na huu ni utopolo na umakolo wa hali ya juu kabisa.

Sidhani kama Rais Samia anahitaji sifa za hovyo namna hiyo na nyingine za aibu. Nafikiri Viongozi na Watumishi serikalini muache kujipendekeza.

Kuna habari moja ya aibu nimeitizama TBC muda si mrefu. Kuna shule huko Morogoro , Matombo sekondari. Tangu uhuru hakuna muundo mbinu wowote ambao Serikali imewahi ongeza..shule hiyo ilijengwa na mkoloni. Sasa kuna madarasa ma nne tu nasisitiza Ma NNE TU..serikali ya CCM ndo imeona iyajenge leo, 60 years later since colonial era anatajwa Rais Samia... "Rais Samia anakwenda kujenga vyumba vinne...'' what in the hell is this?

Embu Rais atajwe katika mambo ya msingi.. Mambo mengine kumtaja Rais ni kumtukana. Ifike mahala tuache potosha wananchi. Miradi mingine ni ya Wananchi.. Aibu.

Mambo kama haya ndio yanawapa watu hawa utukufu na kujikuta wao ni Miungu hapa duniani. Na ndio maana mtu anaweza simama mbele za watu na kusema 'nitaenda kuwa viongozi wa malaika...' ujinga kabisa. Kumbe sisi wenyewe ndo tumewajaza Ufalme Juha... Ukuu uliopitiliza na Utakatifu.

Tuache Ujinga huu.

AIONE SSH.
Duuuuh
 
Awamu ya jiwe hili jambo ndipo lilishika hatamu, hii ni legacy mojawapo ya mwendazake
Na ndio tatizo la kumwabudu Jiwe lilikoanzia likiongozwa na Prince Bashite.
Kila wakati kutajataja majina yake yote na kumsifu muda wote kwa mambo yote hata akinywa maji. Hiyo ndio personality cult.
Ni ibada inayoendelezwa na waliojaa unafiki unaotokana na njaa endelevu au uoga, na kwa sehemu nyingi, VYOTE.
Lakini, huyo huyo Rais mfanya kilakitu hapa Tz akitajwa kuhusishwa na matukio mabaya, ya uovu, uonezi au karaha kwa wananchi, hao hao wanaojivunia kuimba mapambio wanaanza kudai ANATUKANWA.
 
Back
Top Bottom