Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,361
- 2,734
Hivi ulivyompigia kura kikwete na ccm umevuna mahindi au mabua?
Tumevua.............Mabua
Hivi ulivyompigia kura kikwete na ccm umevuna mahindi au mabua?
Mkuu, uwe unasoma makala kwanza basi kabla hujaanza kukurupuka. Anyway, uchaguzi uliopita wala kura sikupiga kwa sababu ambayo ipo nje ya uwezo wangu na hata kama ningelipiga wengi hapa wanajua ningelimchagua nani.
Soma vizuri, sikuanzisha mimi hiyo mada.
mabuha = mabua
Mkuu umemsoma vibaya Angel Msofe..swali hili lilikuwa linamwendea Faiza Foxy.....wewe umeleta habari ambayo baada ya kuona mwanzishaji faiza kidogo tuichunieeee kwa hiyo aliyeanzisha suala la mahindi na mabuha ni FF na mimi namjibu kuwa tulipomchagua kikwete tulivuna Mabuha................
By FaizaFoxy
Kususa inkwisha? mlipoteza muda mrefu sana kwa siasa za kususa susa, naona mmejifunza kuwa kususa inatumika kuwa "disadvantage" kwenu.
Nimekuwa najiuliza, hivi ukivamiwa na nchi fulani ya jirani au hata ya mbali, je kuna haja ya kusimama na kuitetea nchi yako? Hili swali ndiyo limenipa msukumo wa kuandika haya machache hapa.
German ikiongozwa na Adolf Hitler, walianza mchakato wa kuzishambulia nchi za jirani na lengo hasa likiwa kujipanua kiuchumi. Walijizatiti kivita na walipokuwa tayari, walianza mchakamchaka wa kuzichukua nchi moja baada ya nyingine. Nchi nyingi kama Waholanzi, Wapolish, Wafaransa, Warusi waliwapinga na hiyo ikapelekea nchi hizo kupigwa vibaya sana na kuharibiwa.
Mji kama Warsaw, waliuvunja zaidi ya asilimia 90. Russia walikuwa wakivunja kila kitu na kwa Moscow, Warusi waliamua na wao wenyewe kuuchoma mji wa Moscow na Wageruman walipokuwa wakifika, hawakuwa na maji, chakula wala sehemu ya kujisetiri.
Vita kali sana ilipiganwa huko Volgograd (zamani ikiitwa Stalingrad - Battle of Stalingrad - Wikipedia, the free encyclopedia ) na vita ilipoisha, kulikuwa na uharibifu mkubwa sana. Katika matukio ya kusikitisha, ni kikosi cha Warusi, askari 10,000 ambao walipelekwa kushambulia Wageruman na wote wakafa. Mengine mtu unaweza kusoma mwenyewe kuhusu vita na hilo si muhimu hapa.
Upande mwingine, kuna nchi ambazo wao walimkaribisha Hitler kwa mikono miwili ingawa kwa shigo upande na kumpa funguo na mji mkuu wao na hiyo ilipelekea nchi hizo zisipigwe hata risasi moja wakati wa vita ya pili ya dunia. Moja ya nchi hizo ni Czech na ukiona mji mkuu wao uitwao PRAGUE, utagundua tofauti yake na nchi nyingi. Pale kuna majengo ambayo mengine hata yana zaidi ya miaka 1,000. Old town ya Prague kwa ujumla ni kipande kizuri cha historia.
Hapa swali langu ndiyo linaanza, je kulikuwa na haja ya nchi kumpinga Hitler? Je walifanikiwa nini zaidi ya kusababisha nchi zao kuharibiwa tu na silaha kali za Hitler? Je hao waliokubali nchi zao kuchukuliwa kirahisi, leo wamefaidika vipi?
Nafikiri hapa jibu litategemea mtu umeamua kukalia kiti katika upande upi. Wengine wanaona kuwa nchi zilizomgomea Hitler, walao baada ya vita ya pili ya dunia, walianza kuipanga miji yao upya hasa ukichukulia kuwa, miaka ya zamani, mitaa ilikuwa myembamba sana na vitu kama mabomba ya maji, umeme, simu, gas nk ilikuwa kwenye mpangilio wa ovyo kutokana na mitaa kuwa myembamba sana na hatari kwa afya ya binadamu.
Kwa wale waliokataa vita, wamebaki na historia yao na huku dunia nzima ikienda kuangalia jinsi zamani nchi za Ulaya zamani zilivyokuwa.
Hata kwa Tanzania, kuna makabila yaliwakubali na kuwapokea Wakoloni bila upingamizi. Wanyamwezi, Wahehe, Wangoni, nk waliamua kula nao sahani moja na kufanya maisha ya jamaa kuwa magumu walau kwa siku za mwanzo. Hapa napo unarudi kwenye lilelile swali, je kulikuwa na haja ya kuwagomea na matokeo yake yakawa kifo cha Isike, Mkwawa, Kinjeketile Ngwale na wananchi wengi sana ambao kulikuwa hakuna haja/kulikuwa na haja?
Tukirudi kwenye kesi yetu hapa ambayo imeumiza sana watu kichwa, Chadema kulikuwa na haja ya kumsusia (PROTEST) Kikwete pale Bungeni? Kulikuwa na haja ya Dr. Slaa kutokufika sehemu ya kuapishwa Kikwete pale uwanjani?
Kwangu mie, miaka ya zamani ningelijibu kuwa ilikuwa ni ushamba wa hali ya juu. Utamsusiaje mtu ambaye kesho yake unaenda kwake kumuona? Hiii hali iliendelea kuwepo kichwani kwangu hadi wakati wa vita kati ya Iraq na Iran (Israel vs Palestine) ambapo kila wakati nilikuwa nashangaa jambo moja kuwa kila wakisema wiki lijalo, watakaa mezani kujadili kusimamisha vita, basi vita ilikuwa inazidi kuwa kali sana. Zinapigwa utafikiri wamesema mwisho wa dunia unakaribia.
Nilimuuliza kaka yangu nini kinasababisha hii kitu na yeye akanijibu kwa kiingereza "Bargaining power at the mediation table."
Sina uhakika kwa kiasi gani, Nguvu ya CHADEMA na Dr. Slaa kwa CCM na hata kwa IKULU kwa sasa imekuwa kiasi gani au kupungua kwa kitendo chao cha kumsusia Kikwete na tume yake ya Uchaguzi. Je kama wasingelifanya hivyo, CCM ambayo hata kwenye kampeni zao hawakuwa na ajenda ya katiba mpya, wangelianzisha mchakato huu?
Labda kuna vijimaswali kadhaa inabidi kujiuza na haswa watu kama Lady FF (ingawa nafikiri atakuwa anafahamu hata zaidi yetu wengi humu ndani ya JF) kuwa, msuso wa CHADEMA, umeipa Bargaining Power kiasi gani hapa Tanzania against CCM/Ikulu/Serikali ya TZ?
MAONI YANGU: Kuna dalili kubwa kuwa, kususa kwa CHADEMA kumeleta mchakato wa katiba mpya. Sidhani kama CCM wangelianzisha kitu kama hiki bila ya kusukumwa kutoka nje kama Newton's law of motion inavyosema "a body will remain at rest or will continue to move at a constant velocity, unless an external force is applied. "
Ni mtu ambaye hafikiri sana na hajui au anajua ila anajifanya hajui (FF) ndiye atakuja na maelezo kuwa CCM wenyewe wameamua tu kubadilisha katiba na Rais mwenye kaamua tu kwa HURUMA yake kuonana na Chadema.
AGAIN, remember "a body will remain at rest or will continue to move at a constant velocity, unless an external force is applied. " Ukiona VINAELEA, VIMEUNDWA.
Hizo zote pumba, huko ireland unakoongea ni vita vya kidini, nani asiyejuwa? hata sijui unaongea maajabu yepi?
Hayo unayosema ingekuwa Serikali imenyanyuwa bendera nyeupe na kusema haya jamani wacheni kususa na maandamano mje tuongee, hapo ningekuelewa. Lakini bendera nyeupe mmyenyanyuwa nyinyi na mliotaka kuonana na Raisa ambae mlikuwa hamumtambui ni nyinyi na si mwingine. Sasa ujanja uko wapi? Na Kikwete alisemaje siku mliomsusia bungeni? usiniambie hujui.
Tulikuwa tunawaambia hapa, wacheni hizo, maana ya siasa sio hiyo. Hamsikii. Tazama sasa, umewashuka shuu, mnatafuta pakutokea hampapati. Mmerudi kulekule kwa yuleyule aliyewaambia "Mimi ndio Rais..."
Nakwambia seminar za kile chama cha siasa cha Kikristo cha Ujerumani CDU zimewasaidia kwa kiasi fulani, maana inaonesha mlikuwa hamjui maana ya siasa ni nini.
Naomba itazame ile picha ya viwanja vya Ikulu kabla ya kuingia kumuona Rais. Uniambie unakiona nini hapo.
Na mwenyekiti wako juu huko kwenye post kishaanza kusema kuwa katiba sio mwisho wa matatizo. Anajihami kabisaaa, yeye ndio aliilia, halafu yeye ndio akawa hataki mswaada upitishwe haraka, halafu yeye huyo kasusa halafu yeye huko kaomba kuonana na Rais.
Nimefurahi sana kwa hilo, kuwa mmemjuwa Rais ni nani, na makamu wake ni nani na Rais wa Zanzibar ni nani na makamu zake ni nani, na mmerudi.
Kile cheo ndio the most powerful katika Tanzania, kisikie hivihivi. Waone pale mbele yake, wote heshima na adabu, Hakuna kwii wala kwaaa, Unafanya maskhara wewe!
Bibie,Si mlikuwepo mbona hamkujumlisha nyinyi matokeo na kutangazia yaliyo sahihi? ina maana hata hesabu za kujumlisha kura zinawashinda? Unanshangaza!
Usitake kuchakachuwa, ikiwa bungeni tu mnasusa ingekuwa mmeibiwa si ndio mnge zira kabisa.
Hata kama tungetangaza mngetuita wachochezi. We know the likes of you.Basi mmekatazwa kutangaza hata ushahidi wa kupeleka mahakamani umewashinda kuweka? hizo ni alinacha na habari za kusadikika, kwenye wengine haziingii akilini.
Hapo kwenye red umechapia, Hitler hakuwahifika Moscow, aliyefanyiwa hivyo anaitwa Napoleon
Tatizo la kijijini kwenu ni wavivu, sisi kijijini kwetu raha mustarehe, mtandao 24/7, mboga mboga mihogo tunaishusha kila siku sokoni, maziwa fresh, kuku wa kienyeji, umeme wa samadi, mlikuwa wapi nyinyi? nyie huko kijijini kwenu piganeni tu wenzenu kule mjini akina Slaa wameamuwa kumkubali Rais na kumuomba kukutana nae na wemetoka Ikulu wanacheka kwa furaha, ushahidi ni picha. Na Slaa kasemaa hiyo sio "isolated" case. Kalagabaho.
Basi mmekatazwa kutangaza hata ushahidi wa kupeleka mahakamani umewashinda kuweka? hizo ni alinacha na habari za kusadikika, kwenye wengine haziingii akilini.
Hiyo inaitwa "friendly fire" mnajichanganya mpaka mnaripuwana wenyewe kwa wenyewe. Kama hamjajuwa FF basi ndio mimi.
Mwenye "parochial" mind ni mimi au aliyesomea kanuni za kanisa?
Hilo la "isolated case" rudia posts na uone ni nani aliyelisema mwanzo, mimi nimelirudia tu. Usije ukakuta ni Katibu Mkuu wako ndiye aliyelisema hilo, utashushuka.
Ikiwa mtu aliyesusa Rais, aliyepinga kuwa si Rais, aliyeamrisha maandamano, aliyekuwa hajaeda kikao cha mwanzo, na sasa kasalim amri na kaenda na tumemuona, na anapotoka huko anasema "tutawaokoa", "katiba sio mwisho wa matatizo", kuwa hii sio "isolated case", anaeongea hayo unafikiri kaenda kwa kupenda kwake? nnakuhakikishia ni matakwa ya Mwenyekiti wake, aliyekwenda Ikulu mara ya kwanza na wenzake, mara ya pili peke yake (imeripotiwa humu) mara ya tatu kamlazimisha katibu Mkuu aende akitaka asitake. hakuna cha kupotosha hapo ni "common sense" ambayo kwako amma haipo amma ni finyu ndio iliyotumika.
Hilo swali lako la mwisho hiyo ndio reaction za action kama mleta mada alipoielezea theory moja maarufu, au bado hukubali kuwa kila action ina reaction? Unataka kuvamia kituo cha polisi, unaambiwa tawanyika wewe unakaidi, ulitegemea reaction ipi hapo? upigwe na chelewa?
Kama Urais ni taasisi basi Kikwete ndio Rais wa hiyo Taasisi.
FF, hapo utakuwa una invite wachangiaji wakujadili wewe personally, halafu wasipokujadili unavyotaka, then tatizo litaanzia hapo na mada kugeuka na matusi kuanza, nimejifunza kwenye hilo.Hiyo inaitwa "friendly fire" mnajichanganya mpaka mnaripuwana wenyewe kwa wenyewe. Kama hamjajuwa FF basi ndio mimi.
Kususa ni njia mojawapo ya kujiexpress nadhani ata wewe uliepost kwa namna moja au nyingine unasusa anapokua na dissatsification ili kufikisha ujumbe....CDM hawakulupuki thas y ata jamaa wa magamba kasoma mchezo na kua mpole ili nchi itawalike.....so nampongeza JK na viongozi wa CDM kwani KJ akiacha ushambenga wa uCCM nadhani nchi itaenda sawa..jamani cku hizi kuna facial transp..... huyo jamaa nyuma ya JK ananitisha wakati wa picha wawe wanamtoa yani...........[/QUOTE]
Mkuu hapo kwenye RED, yan jamaa ndo kaharibu mandhar ya hiyo picha kabisa
Kuwa na Wabunge/ Madiwani wengi siyo indication pekee ya kuwa Mkwer.re alishinda kwa 61%, unamaana kuwa tukichukua 5age ya wabunge/madiwani wa Magamba vesus wa upinzani tutapata idadi yao ni 61%???kama unaamini hivi basi we Mama utakuwa na very narow thinking capacity.Na hayo mlishinda? nani mwenye wabunge zaidi? nani mwenye madiwani zaidi? ukipata jibu utajuwa Rais wako ni nani kama walivyojuwa viongozi wa chama chako.
Na hayo mlishinda? nani mwenye wabunge zaidi? nani mwenye madiwani zaidi? ukipata jibu utajuwa Rais wako ni nani kama walivyojuwa viongozi wa chama chako.