Kumsamehe aliye kusaliti

Ni vizuri uwe mwepesi kusamehe kwa sababu najua makosa hayakosekani, so ukiwa unaweka vitu moyoni huo moyo utakuza mzito kama sim tak mwisho wa siku kukosa furaha moyoni.

Ukisamehe unakua comfortable sana na unabarikiwa na Mungu, embu jiulize Mungu angekua hasamehi dhambi zako tungebaki wangapi hapa duniani? Kuna makosa mazito sana kusamehe ni ngumu ila ww ukiwa tayari vitu vinapita tu na love inakua mingi sana... ila kwenye mapenzi pagumu mno mkuu...
 
Ni kwel mkuu vp kwa mfano mwnamke akakussliti mara ya kwanza akakili na akaomba msamaha yakaisha alafu baada ya muda Tena karudia Yale Yale Tena vp unaweza msamehe

NB : bado anakujali na heshima iko pale pale yaan hajabadilika kitu
Anakuheshimu vipi wakati anakusaliti. Sijakuelewa
 
Ni vizuri uwe mwepesi kusamehe kwa sababu najua makosa hayakosekani, so ukiwa unaweka vitu moyoni huo moyo utakuza mzito kama sim tak mwisho wa siku kukosa furaha moyoni.

Ukisamehe unakua comfortable sana na unabarikiwa na Mungu, embu jiulize Mungu angekua hasamehi dhambi zako tungebaki wangapi hapa duniani? Kuna makosa mazito sana kusamehe ni ngumu ila ww ukiwa tayari vitu vinapita tu na love inakua mingi sana... ila kwenye mapenzi pagumu mno mkuu...
Mbona hakumsamehe lucipher alipoasi kule mbingini?
 
Kama simpendi namsamehe ......ila kama nampenda siwez aiseee naumia saana !!!!
Kuna ex alikuwa anawaambia wenzie huyu gf wangu ananivumilia,Kumbe mwenzie sijawah kumpenda moyo ni kiza kinene
 
Ngoja namm nisamehe tuuu basi hakuna namna Tena sjui nmpende zaidi ili aondoe Ile hulka yake ya kuzoea kusaliti
Kusamehe ni kukipigia magoti kifo kiingie katika nyumba yenu.
Kama umeingia kwenye mahusiano naye sababu ni mzuri,hata ukimfumania utamsamehe sababu uzuri wake bado upo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu ni msomi ,hata ukimfumania utamsamehe sababu vyeti vyake bado vipo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu anapesa hata ukimfumania utamsamehe sababu pesa bado zipo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu mpo dini moja utamsamehe sababu bado mpo dini moja.

Kama umeingia kwenye mahusiano unatafuta wa kuishi naye hata ukimfumania utamsamehe sababu unachotaka ni MTU wa kuishi naye.

KAMA umeingia kwenye mahusiano unaamisi sio msaliti ,hutoweza kuendelea naye sababu ni msaliti.Na wewe hukuwa unatafuta msaliti.
he/she is not your choice
Shikamoo!
 
Lazima ujifunze kusamehe kwasababu it is the right thing to do. Unasamehe kwa faida yako wewe sio kwa aliyekukosea. Unaposamehe unajiweka huru, unaondoa sumu moyoni ambayo yaweza kukudhuru siku za mbeleni. Usiposamehe maana yake unaweka visasi, majuto na hasira vitu ambavyo ni madhara kwa afya yako ya kimwili na kiakili. Usiposamehe, maana yake unaongeza tatizo kuwa kubwa wakati unaposamehe unaondoa uhasama na pia unatoa fursa kwako na kwa aliyekukosea kujifunza. Lakini muhimu zaidi hata ufanyeje, ulie, ulipize kisasi, umkomoe aliyekukosea HAIFUTI LILE KOSA LA MSINGI ALILOFANYA MWANZONI.

Kuna tofauti kati ya a) Kusamehe na b) Kuendelea na huyo aliyekukosea. Uamuzi ni wako unaweza kusamehe na kuamua kuendelea na uhusiano kama kawaida au unaweza kusamehe lakini ukaamua kusitisha uhusiano - nakusamehe lakini sitaweza kuendelea na uhusiano. Ni kosa kubwa sana kutosamehe kwasababu madhara yake ni makubwa hasa kwako wewe, maana yeye ameshafanya. Kwa kuwa unampenda mwenzako, hakuna atakayekuhukumu kwamba umesalitiwa na ukaamua kumsamehe mwenzako na kuendelea na maisha yako.

Ili uendelee na mahusiano ni muhimu kuzingatia kwamba aliyekukosea anaonekana kujutia na kutubu kosa lake, kwani unaweza kuamua kuendelea naye lakini yakatokea yale yale.

Kusamehe ni lazima kama unataka kuishi maisha marefu yenye afya
Maisha marefu?
 
Mwanamke ni mvumilivu sana ikifikia sehem akakusaliti basi hatoweza kuacha hiyo tabia maana wanayo point of no return .....inashauriwa usimsamehe piga chiniiiii
 
Nimekupata vizuri sana mkuu ushaur mzur saana kiukwel bado nampenda saana na yeye anaheshima saana hajawahi nionesha Ile dharau yaani Sasa sijajua huwa anapatwa nanini Paka anaamua kunisaliti

Kibaya zaidi Hua ananisaliti ambapo Hua hata hatupo katika conflict na waala nakua sijamkwaza

Inshort npo mkwel kwake 100% sijawahi mcheat muda wote na tuna five years

NB... Nampenda ila kila nkimuona na nkiifkilia yalotokea naumia sana
Kama uchawi upo umerogwa siyo bure kama uchawi haupo lazima unashida katika akili.
 
Mungu mwenyewe alisalitiwa na shetani akamfukuza kwenye ufalme wake sembuse wewe mwanadamu.
Kumsamehe msaliti ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe hata Mungu alishindwa, acheni kujitia wakomavu wa uvumilivu, mtaharibu maisha yenu.
 
Mimi mpenzi wangu akinisaliti anakutana na ngumi za kutosha halafu maisha yanaendelea akitaka kula kona kimpango wake sasa
 
yalinikuta nikaombwa msamaha nikasamehe kosa kubwa la hawa viumbe kama ana marafiki wanaokujua na kesi pia wanaijua jiandae maumivu

Baada ya msamaha tulienda vizuri tu adabu kama zamani kadri siku zinapozidi kwenda dharau zikaanza ukiongea nae basi lazima mashoga zake wajue na mambo ya mitandao haya

siku moja kama Mungu tu akaniongoza hebu mtafute muulize mustakabali wenu ndani ya huu mwaka mpya nikaambiwa baaadae tutaongea nikanyuti baadae kupiga simu naqmbiwa nacheki tamthilia nikapga usingizi
kesho yake night nikamjia hewani nikakuta yuko kwenye jam asubuhi kuuliza imekuwa kesi kwamba complaining nyingi na vitu ambavyo havieleweki
Nikapiga goti chini Mungu akasikiliza kilio changu nikamuacha alikuwa ni mtu amabae sio rahisi kumuacha

suala la kurudiana na mtu aliekusaliti ni kama kujiua mwenyewe samehe na move on
Mungu husikia kilio cha kila mja wake
mkuu Hapo umefunuliwa tu huyo mwenzako ni mtu wa aina gani usipoteze muda kumrekebisha utakwama kila wakati fanya maendeleo
 
Back
Top Bottom