Kumsamehe aliye kusaliti

Ni kwel mkuu vp kwa mfano mwnamke akakussliti mara ya kwanza akakili na akaomba msamaha yakaisha alafu baada ya muda Tena karudia Yale Yale Tena vp unaweza msamehe

NB : bado anakujali na heshima iko pale pale yaan hajabadilika kitu
Heshima gani iliyo palepale.......Mi nilisalitiwa na mke wa ndoa nikamsamehe....akarudia. nikaingia mahakamani nikadaka gamba muda huu kila mtu kimpango wake. Usicheze hicho kidonda hakipinagi ni kama kansa hivi. Ushauri wangu ukisalitiwa katika uchumba hiyo ni alam kiwa hicho kimeo.....unasamehe ili iwaje sasa
 
Mi sijawahi aisee! wenza wangu wote nimewaacha ingawa wengine walithubutu kuniambia hawatorudia
 
Naomba niongelee kidogo ili suala kwa mapana

Kusalitiana kupo duniani na akuta kwisha mpk mwisho wa dunia hii kwa sababu uletrwa na matamanio ambayo ni madhaifu ya kibinadamu. Kumbuka kuwa kila mtu ana mtu wake awe m/ume au m/mke na unapotoka nje ya ndoa au mahusiano ni mtu mwingine wa nje ni kwamba nae anamsaliti mtu wake hivyo ndivyo circle ilivyo.

Wanaume uwa tunaumia sana kusalitiwa na hii imekaa kibaiolojia Zaidi maana wanaume tumeumbwa kama mashujaa na viongozi na wamiliki wa wanawake hivyo kusalitiwa ni kwamba unajihisi kama umevuliwa hivyo vyeo vyote. Ila tukubali kabisa kuwa kusalitiana kupo na ni jambo la jinsia zote mbili kwa kuwa tendo ufanywa na jinsia mbili tofauti kwa hiyo level ya usaliti ni 50/50

Kuhusu msamaha hapa ndio kuna mtihani mkubwa sana ambao bila ya Imani ya dini unaweza kushindwa kusamehe maana msamaha kibinadamu ni kitu kigumu sana. Biblia kwa wakristo inasema samehe saba mara sabini yaani hata mtu akifanya kosa na kurudia tena na tena na akaomba msamaha anapaswa kusamehewa (dhana ya saba mara sabini). Kwa wanandoa kusameheana ndio msingi mkubwa wa ndoa pamoja na kupendana na kuvumiliana ukiyawezxa haya utaishi vizuri katika ndoa na ukishindwa mojawapo bado ndoa uwa ICU.

Kwa kuwa binadamu tumeumbwa na mapungufu na pia kukosea ni ubinadamu basi mtu au mwenza akikuomba msamaha msamehe kwani hakuna bnadamu mkamilifu bora zimwi likujualo kuliko kuvunja ndoa na kuanza mahusiano mapya ambayo baadae nayo yatakuja kuwa kama hayo ya mwanzo au kuwa mabaya Zaidi kwa kuwa hakuna mkamilifu chini ya jua. Tuvumiliane na kusameheana

Ni ngumu sana ila hamna namna duniani hamna mkamilifu tuachane na kulipiza kisasi tutajiangamiza Zaidi maana unapomchikia mtu sumu ya chuki na hasira inakuumiza wewe Zaidi kuliko unayemchukua

ASANTENI
Hakika umenena ukwel mtupu mkuu
 
Heshima gani iliyo palepale.......Mi nilisalitiwa na mke wa ndoa nikamsamehe....akarudia. nikaingia mahakamani nikadaka gamba muda huu kila mtu kimpango wake. Usicheze hicho kidonda hakipinagi ni kama kansa hivi. Ushauri wangu ukisalitiwa katika uchumba hiyo ni alam kiwa hicho kimeo.....unasamehe ili iwaje sasa
Daah aisee Sina cha kusema
 
mkuu...unaweza kusamehe ila kusahau ni ngumu
mie nakumbuka nilivo oa..wife baada ya miezi tu enzi izo ndoani..akaanza kuchat na ex wake, kutumiana vipicha half naked kumtamanisha sijui kawa mke wa mtu...uwezi amini niligundua..niliumia..niliumia aliona machoni mwake kaniumiza mme wake...alipagawa..maana nilipiga kimya baada ya ye kujua nimeona ule upupu..alinyooka..alitubu..ila mpaka kesho haamini sikumbutua sikumkwida wala sikumfanya chochote il hali kipindi cha uchumba ndo zilikua zangu ..

wanawake hawajui wanachotaka mostly, so ukishindwa kumsamehe jua ndo basi... na mimi nilimsamehe kwasababu alizingua na bila sababu..nikasema nisimbane sana maana hajijui alichofanya
pole sana
 
olver, post: 25267764, member: 415752"]Mfano hakuna sababu mkuu yaan mko Safi tuu hamjagombana wala nini[/QUOTE]
Nimesafiri mda,nimepata ulemavu wa mda kidogo km zaidi ya miaka miwili kutokana na maradhi labda sina namna.zipo nyingi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom