Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,863
KUMRUHUSU BINTI AONDEKE NYUMBANI AKAJITAFUTIE MAISHA NI KUMFANYA AWE MALAYA!
Anaandika, Robert Heriel.
Mwanamke hatafuti maisha Ila anatafutiwa, maisha ya mwanamke yapo Kwa mume wake au Mzazi wake. Ni hatari na kosa kubwa kumruhusu binti yako akatafute maisha. Mwanaume ndiye anayekula Kwa jasho, neno Kula Kwa jasho linamaanisha "kutafuta" ili utafute basi itakupasa usijue kitu unachokitafuta kipo wapi na utakipata lini.
Mzazi unaanzaje kumruhusu Binti yako umpendaye akatafute maisha ambayo hajui yako wapi na atayapata lini, huo ni upumbavu, na kutokumpenda binti yako.
Binti anapaswa akishakua anaandaliwa mazingira ya kuolewa, Kama atakuwa amebahatika kupata kazi basi Alhamdulullah!
Kumruhusu binti akatafute maisha inamaanisha umeruhusu binti yako afanye umalaya,
1. Binti aombe kazi akiwa nyumbani kwako au nyumbani Kwa Ndugu yako unayemuamini bila kujali umri wa binti yako.
2. Usimruhusu binti kupanga chumba na kujitegemea ikiwa hana kazi maalumu, hajaajiriwa.
Mzazi ni Bora umuajiri binti yako mwenyewe ikiwa Ajira zinasumbua kuliko binti ajiajiri mwenyewe akiwa mbali na hapo nyumbani.
3. Binti akifikia umri wa kuolewa, hakikisheni anaolewa iwe Kwa Kupenda mwenyewe au kutokupenda.
Mwambieni umri wa kuolewa umefika, Kama anamchumba amlete nyumbani. Kama hana mwambie mnampa muda Fulani amlete mchumba akishindwa mwambieni mtamtafutia ninyi wenyewe.
4. Ni marufuku binti kufanya kazi za kujidhalilisha utu wake, au zenye mazingira ya kuudhalilisha utu wake. Kama Muziki wa kidunia. Sio binti anafanya vitu vya kipuuzi puuzi na kuanika uchi wake kwenye majukwaa Kama mwendawazimu.
5. Kama binti atapata kazi ya kuajiriwa mbali na nyumbani, akapanga nyumba basi muambieni mtampatia ndugu mdogo WA kuishi naye na kumsaidia kazi.
6. Ni vizuri umuozeshe binti yako Kwa kijana mnayeheshimiana hii itapunguza uonevu, unyanyasaji na hata kutalakiana kusiko Kwa muhimu.
Sio binti aokote wahuni wahuni wa uko mjini wasio ijua hata Imani na maana ya ndoa.
7. Mfanye binti yako akuelewe unataka nini kwake. Hii itapunguza mifarakano baina yako na yeye. Binti Yako asipokuelewa atakuwa mbaya zaidi.
8. Mtiishe mama yake na kumfanya mama yake awe Mke Bora ili aige kutoka Kwa Mama yake.
Mke wako akikushinda basi hata watoto wako watakushinda, hakikisha mkeo umemshepu vile unavyotaka ili isikusumbue katika malezi ya binti zako.
Madhara ya kushindwa kumtiiisha Mkeo utayaona Kwa watoto wako.
9. Usikubali mtu amchezee Binti Yako ungali upo hai.
Hakikisha Jambo hilo binti yako analifahamu. Hiyo itamfanya hata yeye asikubali mtu yeyote amchezee.
Ikiwa utashindwa kumlinda binti yako na kumpigania Kwa nguvu zote basi hata yeye atashindwa kujilinda na kujipigania.
Kitu chochote kisicholindwa kamwe hakiwezi ijua thamani yake. Hivyo hata chenyewe hakitaweza kujilinda.
10. Mfanye binti yako asiwe na Shaka juu ya Maisha. Mwambie hapo nyumbani ni kwao. Asiwe na presha ya kujitegemea kwani mwanamke hapaswi kuwa na fikra hizo. Mwambie, mwanamke ananyumba mbili, Kwao na Kwa mume wake.
Wakati mwanaume hana nyumba hata moja. Hata alizojenga sio zake.
Kuruhusu mwanamke kutafuta maisha NI Kumtupa kwenye shimo lenye nyoka wakali.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Safarini kuelekea Arusha,