Kumradhi:Mh RAIS JK alitutakia mwaka mgumu/wa shida 2011 wakati wa hotuba 31/12/2010

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
9,281
7,126
SASA NAAMINI Mh.Dk,Luten Kanali KIKWETE tarehe 31/12/2010 kwenye hotuba yake aliwatakia wanainchi HEAVY NEW YEAR 2011 na sio happy new year

Bei za bidhaa hizi na nyinginezo zimepanda
sukari,mafuta ya kula ya taa,unga zote,
maji ya bakresa,chai kwa mamantilie,maharage
Umeme juu na haupatikani,migomo, polisi ua raia,KIBONDE wa Clouds kutukana studio wazazi na vijana masikini,Celina Kombani-wanaodai katiba ni watu wa barabarani tu

Wana JF hamuoni kuwa JK alichomeka neno HEAVY na kuondoa happy?
 
kwa hiyo unataka JK akutafutie chakula,akupikie na akulishe?

Acheni visingizio fanyeni kazi mungu atawabariki
 
kwa hiyo unataka JK akutafutie chakula,akupikie na akulishe?

Acheni visingizio fanyeni kazi mungu atawabariki

Wewe lazima utakuwa ni kilaza!inavyoonekana hujui kabisa kazi(wajibu) wa serikali kwa raia wake!kwa faida yako,kazi ya serikali kwa raia wake ni kutoa huduma za jamii,kuongeza nafasi za ajira kwa kubuni mipango mbalimbali,kupambana na maadui watatu wa maendeleo kama vile Ujinga(kama wewe ulivyo),maradhi na umaskini.Na uduma nyingine nyingi!kwa mfano kutoa ruzuku wa wakulima wa korosho,kutawasaidia wakulima kuuza bidhaa zao kwa wingi,pia kupanua uzalishaji wa mazao yao!!
 
kwa hiyo unataka JK akutafutie chakula,akupikie na akulishe?

Acheni visingizio fanyeni kazi mungu atawabariki
Kazi ziko wapi mkuu, tuonyeshe ziliko maana watoto wetu hawana kazi wamehitimu Chuo kikuu na wengine wengi wapo ghetho tu. Naona wewe wa kwako wanapata kazi kirahisi tu. Nipe contact zako utupe kazi za wanetu.
 
Wewe lazima utakuwa ni kilaza!inavyoonekana hujui kabisa kazi(wajibu) wa serikali kwa raia wake!kwa faida yako,kazi ya serikali kwa raia wake ni kutoa huduma za jamii,kuongeza nafasi za ajira kwa kubuni mipango mbalimbali,kupambana na maadui watatu wa maendeleo kama vile Ujinga(kama wewe ulivyo),maradhi na umaskini.Na uduma nyingine nyingi!kwa mfano kutoa ruzuku wa wakulima wa korosho,kutawasaidia wakulima kuuza bidhaa zao kwa wingi,pia kupanua uzalishaji wa mazao yao!!
hii nchi ina amani sasa mnachoshindwa kujiajiri ni nini?mabilionea wote duniani sio waajiriwa tena akili zenu zinatutia mashaka manake mumezoea kugoma huko vyuoni kazini ntakuwa wasumbufu

Endeleen na migomo muone kama inajenga nchi
 
Enzi zile tunapigania uhuru huwezi kusikia kila kitu tunaililia serikali, siku hizi kila jambo inalaumiwa serikali, ndoa zetu zikivunjika ....serikali. Kushindwa kwetu kutimiza tendo la ndoa kwa wake na waume zetu...serikali.

Wakati mwingine tuna nafasi ya kuzungumzia namna gani kila mmoja wetu kwa nafasi yake alivyochangia kutokomeza umasikini. Kwa mfano, ninapokwenda kijijini kwangu wakati wa likizo huwa najitolea kufundisha bure hivyo ningependa kuhamasisha na wengine wanaoweza kufanya hivyo ama kufanya jambo lingine la kujenga nchi kadri fursa yako inavyokuruhusu.
 
Kuna bwana mmoja ana fedha nyingi tu mama yake alikua anaumwa lakini hakumsaidia kupata matibabu na kumwacha kijiji bila msaada wa tiba, hata hivyo, wakati wa mazishi watu walikuwa wanailaumu serikali kushindwa kukidhi mahitaji ya wananchi wake na kudai mama yule kama angesaidiwa alikuwa na nafasi ya kupona. Mimi nikasema serikali ilimsomesha bure yule mtoto wa marehemu na hadi kafika hapo alipo. Elimu kwa huyo bwana ilikuwa ni msaada kwa njia nyingine kuboresha na kutatatua baadhi ya shida za familia yake kadri atakavyomudu kulingana na kipato chake. Familia bora huzaa taifa bora, huyo bwana hakusomeshwa ili kuwa mbinafsi kwani na serikali ingeamua kuwa mbinafsi asingepata elimu na maisha bora.
 
Wewe lazima utakuwa ni kilaza!inavyoonekana hujui kabisa kazi(wajibu) wa serikali kwa raia wake!kwa faida yako,kazi ya serikali kwa raia wake ni kutoa huduma za jamii,kuongeza nafasi za ajira kwa kubuni mipango mbalimbali,kupambana na maadui watatu wa maendeleo kama vile Ujinga(kama wewe ulivyo),maradhi na umaskini.Na uduma nyingine nyingi!kwa mfano kutoa ruzuku wa wakulima wa korosho,kutawasaidia wakulima kuuza bidhaa zao kwa wingi,pia kupanua uzalishaji wa mazao yao!!

safi mkuu illa nina was wasi kama huyu jamaa ataelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom