Kumpiga mtu picha akiwa eneo la kazi na kuzituma mtandaoni; taratibu za kisheria zinasemaje?

Kiongozi unataka ushitaki upate pesa? Si ulikuwa kazini lakini? Mkataba wako wa ajira wasemaje?
 
Ilikuaje hadi ukapigwa picha? Na mzungu alipost kwa lengo lipi. Je, umeongea nae mzungu kuuliza nn alikusudia? Anavokupiga ulimuona?
 
Habari wakuu

Naomba nipeni taratibu za kisheria endapo KIONGOZI wako wa kazi akikupiga picha na kutuma mtandaoni.

Natanguliza shukrani
 
Ilikuaje hadi ukapigwa picha..?? Na mzungu alipost kwa lengo lipi... Je umeongea nae mzungu kuuliza nn alikusudia? Anavokupiga ulimuona?
Nilikua ofisini kwangu nimekaa nikasinzia yeye aliingia kwa Siri akapiga picha bila hata kuniambia na akaanza kuwatumia viongozi wengine
 
Nilikua ofisini kwangu nimekaa nikasinzia yeye aliingia kwa Siri akapiga picha bila hata kuniambia na akaanza kuwatumia viongozi wengine

Mkataba na sheria zinasemaje kuhusu kusinzia kazini?
 
Umesinzia? Na shukuru huyo bosi wako aliekupiga picha sio kaburu. Nakushauri mpelekee zawadi hata laki moja cash anakupenda sana.

Weka agano na macho yako kwenye kazi za watu hakuna kusinzia. Ukitaka kusinzia sinzia ukiwa unaendesha gari lako main load majibu utayapata hapa utaleta mrejesho tu.

Asante
 
Kwenye mkataba hakuna Mambo ya kusinzia kazini. Bali Kuna kuhusu kulala kazi yaan kutokuja kazini. Karibu

Hapo kuwa mpole tu mfuate kama ni bosi wako mweleze kuhusu kupitiwa unaweza hata kusingizia ugonjwa ndio maana ulisinzia ila usilete mashindano ya kisheria kwa hayo mazingira.

Nilijua umetulia zako unapiga mzigo akakupiga picha, kumbe amekubabstiza ukiwa umesinzia? Yeye anaweza kuwajibika kwa kupiga picha (ikithibitika ana hatia) na wewe utawajibika kwa kusinzia kazini, na Je, mazingira ya kazi baada ya huo msuguano yatakuaje?
 
MKUU HUTAKI KUPOSTIWA NA BOSI WAKO? AU HUTAKI TUJUE KAZI UNAYOFANYA
 
Habari wakuu

Naomba nipeni taratibu za kisheria endapo KIONGOZI wako wa kazi akikupiga picha na kutuma mtandaoni.

Natanguliza shukrani
mkuu ukijibiwa naomba unitag! sio kazini tu hata kwenye maisha yetu ya kila siku.
 
Sina uhakika juu ya picha ila kipo kipengele cha sheria kinasema huwezi kufanya kitu bila ya ridha ya mhusika. Kule USA kuna mke alifungua email ya mumewe bila ya ridha yake alimpeleka mahakamani na alishinda kesi. Mke alitozwa faini na kifungo cha miezi 2


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom