Kumpiga mama yako mzazi na kumtukana kisa visa vya uzee imekaaje hii?

Mpige tu

Mitoto mingine ingefia tu tumboni au ingezibwa na nyonyo uchangani ikafia mbali huko.

Huo ujasiri hata wa kuandika hivo umeupata wapi.

Mungu mtetee mama mwenzetu.
 
Mzazi wako fanya ufanyavyo asije akakunenea maneno mabaya,epuka sana hilo na kaa nae kwa akili awe baba au mama.

Nina shuhuda mbili,moja ni ya binamu yangu yeye aliowa mke wakashirikiana kumtesa mama yake kuna siku mama yake akamtamkia laana (kwa mujibu wa waliokuwa karibu) alimwambia maisha yake atatanga tanga na mwisho ataishia pabaya na akamsisitiza hayo yatamkuta kabla hajafa,alianza na kufukuzwa kazi serikalini (ninavyoandika hapa yupo jela maisha kwa case ya mauaji na yenyewe ni jumba bovu sababu marehemu siku anauawa siku tatu nyuma alikuwa amegombana nae),mwezi mmoja baada ya hukumu kweli mama yake alifariki.

Nyengine ni hawa wanaojiita watoto wa Kariakoo,huyu alimtukana mama yake matusi ya nguoni mchana wa saa saba jua kali mbele ya kadamnasi akigombea urithi wa nyumba ya baba yake yule mama (sasa nae marehemu) akamtolea maneno huku akionyesha kwa ishara ya kidole na akimtaja jina “wewe kama hukutoka ktk uchi huu hutokaa uufurahie urithi wa baba yako”,nyumba yao sasa pamejengwa ghorofa kwa mkataba familia walipewa floor moja wakagawana watatu na chini walipewa frame moja kila mtoto ya biashara huyu jamaa alianza kuuza upande wake ghorofani kisha akauza ile frame sasa ni homeless yupo mtaani anauza maboksi na analala nje.
 
Jitaidi kuwa mshauri mzuri tu. Wewe ni wa kwanza kufanya haya ulipokuwa mtoto ila ulivumiliwa, kwann ushindwe wewe kumvumilia mtu ambaye kapewa zawadi ya maisha marefu na Mungu?
Ukweli Thread Ni Nzuri
Ila Avatar Yako Ndiyo Chanzo Cha Kuweka Comment
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Nani anaweza mpiga mzazi wake. Mimi bi mkubwa wangu nikiongea nae huwa sauti yangu kama naongea na MUNGU. Naongea nae kama naongea na raisi.
hahaha hata mimi asee kuna kipindi nilimuudhi bi mkubwa yani alikua ananigombeza namjibisha aloo akaanza kuongea huku analia yani nilijisikia vibaya sana yani mpaka leo sijawahi kukaa kubishana nae tena sitaki kuona yale machozi tena.
 
"Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.

Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni."

Qur'an 17: 23-24
 
Akili ya mlezi wako uzeeni ndio hiyoo uliyokuwa nayo wew utotoni hadi unaanza kukua kiutu uzima na kiakili..tofauti ya uzeeni inaongezeka usahaurifu unaongezeka na hasira pia...lea kama ulivyolelewa wew utotoni ila wew simpige kofi ata moja wala kumnyanyasa kwa chochote
 
Waqadhwaa Rabbuka al laata'buduuw il laa iy yahuu wabilwaalidayni ihsaana (Quran17:23)....Mkuu anayofanya mzazi wako uzeeni ndo uliyoyafanya ww utotoni..Usiku wa manane walikua hawatafuti mtoto mwengine kwa usumbufu wako ww bichwa lisilo na akili kama mimi.

USIMDHALILISHE MZAZI WAKO (X3)
 
Unampigaje kwanza? Yani unakunja kabisa ngumi au unamçhapa viboko! Mama yako kabisa aliekuzaa aisee kuna watu mna roho ngumu.

Kuna mmoja juzi kamuua baba'ake eti kisa mzee kagoma asiuze shamba kuna mitoto ni ya hovyo kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom