Kumpiga kibuti mume mkorofi! Muendelezo…….

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Kuna wale ambao hawako tayari kutoka kwenye uhusiano mgumu kwa sababu ya mali. Wanaogopa watagawana mali na wenzao, jambo ambalo hawako tayari kulifanya na mara nyingi hawa ni wanaume. Wapo pia wanawake ambao wao ndio waliokuwa watafutaji wakuu. Swali la kujiuliza ni hili. ‘Ni kipi bora, ni mali au ni amani na utulivu na uhai wako?' kama ni mali, basi hakuna anayeweza kukuingilia kwenye uamuzi wako.

Lakini, kwa ufahamu tu, ni kwamba, pasipo na amani, mali haina maana na pasipo na amani uhai ni wa kubahatisha pia.Wengine wanashindwa kutoka kwenye husiano kwa sababu wazazi wa mume na ndugu wanampenda sana.

Anaogopa kuwaudhi kwa kuondoka kwenye ndoa ya mateso ya mtoto wao na ndugu yao. Anataka wafurahi, hivyo hawezi kuondoka. Huu nao ni upungufu.Hivi unakuwa umeolewa na ndugu na wazazi au na mume? Lakini, kwani ukiondoka utashindwa kuwa karibu na watu hawa? Hutashindwa na pengine urafiki wenu utakuwa wa kudumu. Ukiendelea kukaa kwenye ndoa ya mateso kuna siku utakosana hata na hawa, maana unaweza ukalipukwa ukamuuwa mtoto au ndugu yao.

Kuna wale wanaoshindwa kutoka kwenye uhusiano mgumu kwa sababu wana watoto na wanaogopa kwamba, watoto wao watateseka.Hivi ni kuteseka kupi kubaya, kule kwa utotoni au ukubwani? Mtoto anayeishi kwenye ndoa yenye vurugu, anaharibikiwa kuanzia utotoni hadi ukubwani.

Lakini, hata hivyo kuachana kwa wazazi, sio lazima kuwe na maana ya watoto kuteseka.Kuna wakati hata watoto wanamwambia mama atoke kwenye ndoa, halafu mama huyo huyo anadai anakaa kwenye ndoa hiyo kwa sababu ya watoto! Kuna haja ya kujiuliza maswali kwa upana zaidi.Ukitaka kutoka kwenye ndoa ngumu jiulize maswali haya.

Je, ndoa hii ni kwa faida ya nani? Je, niliolewa au kuoa ili kupata shida au amani na upendo? Je, bila ndoa,nisingeweza kuishi mwenyewe? Tafuta mifano ya wasio na ndoa ambao wanafurahia maisha.

Jiulize ni kwa kiasi gani wengine wanasaidia kukusukuma zaidi kwenye ndoa hiyo? Jiulize ukamilifu wako. Je, wewe ni nusu mtu au mtu kamili? Kama ni mtu kamili , basi ishi kama mtu kamili.
 
mtambuzi mimi ni miongoni mwa hao wa2 unaowasema.nilipost thread hapa wadau wakanishauri sana na nkaamua

ku follow my heart. lakini huyu baba mtoto ni mkorofi hataki kabisa kuniacha na kuheshim hisia zangu. ni mateso kwa kweli.
 
ni bora kuishi peke yako kuliko kuishi na mtu ambaye aman hakuna siku zote, na mwingine anakunyanyasa tu kisa una mtoto naye au watoto akijua huna pakwenda kwa ajili ya watoto na siku zote mwanamke anavumilia kwa ajili ya watoto .....
 
Huu ushauri ni mzuri ila naomba msije mkauleta huku kwetu Tarime na Rorya maana sisi kwetu ni mwendo wa KUTEMA na KUGECHA tu. Na hii ndiyo treatment ambayo wake zetu wanaifurahia.
 
mtambuzi mimi ni miongoni mwa hao wa2 unaowasema.nilipost thread hapa wadau wakanishauri sana na nkaamua

ku follow my heart. lakini huyu baba mtoto ni mkorofi hataki kabisa kuniacha na kuheshim hisia zangu. ni mateso kwa kweli.

Naweza kukusaidia kama ukini-PM
 
ushauri mzuri sana, ndoa ni furaha mateso yaje mengine lakini sio kukoseshana amani kwa kujitakia, bora kuishi pekee kuliko ndoa yenye mateso kutoka kwa binadamu mwenzio,, life it too short to spend it making others happy while u are not.
 
Back
Top Bottom