Kumpeleka mtoto shule yenye ada kubwa ni kupoteza tu hela

Kuna watu wanashindwa kukuelewa mkuu, Yaani mtu anayeingiza labda milioni 20 kwa mwezi anampeleka mtoto shule ya million 5 kwa mwaka kwake anaona amempeleka shule ya gharama ndo maana wanaropoka tu, ila wanatakiwa kuelewa mlengwa wa maada ni nani? Kwa ufafanuzi ni yule mzazi ambaye anapambana anateseka yaani anakaa njaa kabisa et anasomesha mtoto private then huyo mtoto akimaliza chuo aje akae nyumbani ateseke, kumbe bora angempeleka shule za kawaida tu akapata elimu aje mtaani kupambana na changamoto za maisha au kama mzazi amejaliwa basi yale mapambano ya kusomesha shule za gharama angepambana kumuandalia mtoto cha kuanzia pindi atakapomaliza elimu yake,

Asante
 
Wakuu kuna shule moja inaitwa St Joseph ipo maeneo ya Mbezi nasikia na yenyewe inafundisha hatari na ina malezi mazuri kwa wanafunzi, hata mwanafunzi awe mtukutu vipi akienda pale siku akirudi nyumbani unaweza kumkataa kwa kudhani labda umebadilishiwa mtoto. Nani anaifahamu vizuri shule hii wandugu? Nataka nimpeleke dogo akapige interview pale.

Mpeleke nilishawai kusikia
 
Kumpeleka Mtoto shule yenye Ada kubwa au Shule ya Garama ni kupoteza tu hela, cz mtoto atasoma atafika hadi Chuo then atamaliza Vizuri chuo, baada ya kumaliza chuo anakuwa mzigo wako tena anashinda tu nyumbani hana cha kufanya Ajira hamna unaanza kuangaika upya, Wakati Umetumia gharama nyingi hadi kumfikisha Chuo
poverty mentality at its core. akili za watu mafukara.
 
Mtoa mada fungua akili yako mkuu. Mwanao haendi shule kusoma tu. Kuna exposure na watu tofauti na mambo tofauti.

Nilibahatika kusoma shule ya Feza O - level na A- level. Kiukweli nilivyoexperience pale vimenishape na kunisaidia katika mafanikio hadi leo hii.

Tulijengwa kwa spirit ya brotherhood na kusaidiana. Tulipewa fursa nyingi za kuwa bora zaidi mara kwa mara. Shule ilikuwa haiishi competition za mambo ya kompyuta, music, lugha ya kituruki, hesabu na mengine mengi. Na ulikuwa ukichaguliwa mnapewa free trip kwenda nje kwa ajili ya hiyo competition. Hata kama haushindi but kwa kuparticipate tu unakuwa unajijenga katika sekta flani na motivation zipo kila siku. Nakumbuka kuna dogo alikuwa anapiga gitaa flani la kituruki vizuri akawa anapiga safari Uturuki kila mwaka na alikuwa analipwa. By estimation mpaka anamaliza form 6 alikuwa ashalipwa yeye kama yeye zaidi ya 10m bila kuhesabu trip ambazo ni free.

Ukiachana na the fact kuwa tulisoma na watoto wa who is who pale ambapo unajenga fursa ya kuonana na wazee wao na kujenga urafiki wa baadae, bado hata after kugraduate unapata msaada. Ishu za kazi, biashara, na kujuliana hali ni nyingi sana kiasi cha kwamba graduates wa Feza hawahangaiki katika kazi kwa sababu ukiinform alumni na una vyeti vyako unapata connection chap. Can you imagine kuna ofisi ya alumni ambayo ina kila kitu na kama wewe ni alumni wa Feza unaweza kwenda hapo na kuitumia kama workspace yako bila charges zozote kwa muda wowote utakao? Totally free. Scholarship opportunities ndio usiseme.

Pia mahusiano ya uongozi na wanafunzi ni smooth sana. Walimu ni washkaji na ni approachable. Wanakujenga kama sibling ili ufanikiwe mbeleni. Hata baada ya kugraduate mambo ni mazuri sana.

Personal stori moja ni nilishawahi kupewa dili la 16 mil na mwalimu pale shule katika mwaka wangu wa kwanza wa chuo. Imagine 19 years old unaaminiwa na 16 mil. Kibongobongo ni ngumu sana ila mwalimu akanipa pande na hakutaka chochote.

Tafadhali sana kama una uwezo usichezee elimu ya mwanao. Shule si kwa ajili ya madaftari ila kunamshape yeye kama yeye na network yake kwa maisha yake yote.
çok güzel👍
 
Kipaumbele changu ni mwanangu/wanangu waishi maisha bora kuanzia elimu na makazi km hela ninayo nitamsomesha shule ya gharama yoyote na hata akikaa nyumbani nitamuhudumia mpaka atakapo pata maisha yake

Hongera
 
Ni umasikini tu mkuu, sidhani kama kuna mzazi mwenye pesa asiyependa mtoto/watoto wake kusoma katika mazingira mazuri na rafiki kwa taaluma. Hasa kwa kipindi hiki cha sasa.
 
Tuendelee kutafuta hela ndugu zangu mimi mwenyewe ni muhitimu wa chuo ambaye sikupata kazi niliyosomea, lakini hii haiondoi ukweli kwamba natamani nipate pesa Mwanangu asome shule yenye mazingira mazuri na malezi bora. Kuhusu watoto kumaliza na kukaa tu hii pia inachangiwa na uwezo wa wazazi, mzazi kama uwezo unao utakuwa umetengeneza miradi ya kutosha ambayo hata wanao wakikosa ajira serikalini waitaisimamia.# Kinacho tutesa wengi ni umasikini tu
 
Back
Top Bottom