Kumpeleka mtoto shule yenye ada kubwa ni kupoteza tu hela

Wakuu kuna shule moja inaitwa St Joseph ipo maeneo ya Mbezi nasikia na yenyewe inafundisha hatari na ina malezi mazuri kwa wanafunzi, hata mwanafunzi awe mtukutu vipi akienda pale siku akirudi nyumbani unaweza kumkataa kwa kudhani labda umebadilishiwa mtoto. Nani anaifahamu vizuri shule hii wandugu? Nataka nimpeleke dogo akapige interview pale.
 
Wakuu kuna shule moja inaitwa St Joseph ipo maeneo ya Mbezi nasikia na yenyewe inafundisha hatari na ina malezi mazuri kwa wanafunzi, hata mwanafunzi awe mtukutu vipi akienda pale siku akirudi nyumbani unaweza kumkataa kwa kudhani labda umebadilishiwa mtoto. Nani anaifahamu vizuri shule hii wandugu? Nataka nimpeleke dogo akapige interview pale.
mbezi ya morogoro road au mbezi beach?
 
Kipaumbele changu ni mwanangu/wanangu waishi maisha bora kuanzia elimu na makazi km hela ninayo nitamsomesha shule ya gharama yoyote na hata akikaa nyumbani nitamuhudumia mpaka atakapo pata maisha yake
 
Me nadhani kuna haja ya kubadilisha mitazamo yetu juu ya suala zima la kusoma.

Sio Lazima Kila mtu asome mpaka chuo kikuu au kwa matarajio ya moja kwa moja kuwa atapata kazi mambo yamebadilika.

Japo ni muhimu Kila mtu kusoma mpaka kiwango fulani ili kuondoa ujinga.

Hivyo ukiona kuna haja ya kumsomesha mwanao mpaka elimu ya juu ili afike sehamu fulani Fanya hivyo, na ukiona hakuna haja basi tafuta namna nyingine.

Mwisho wa siku la muhimu ni kuweza kayamudu maisha.
 
Hizi sarakasi zote zitaisha serikali ikiamua na kusimamia shule zote zitumie kiingereza kama lugha ya kufundishia ( shule zote za serikali ziwe English medium). Tutapata shida kidogo mwanzoni lakini huko mbele ya safari, tutatoa vijana wanaojiamini na kupunguzia wazazi gharama zisizo na msingi. Kuna watu wanaingia kwenye lindi la umasikini kisa kusomesha watoto English Medium.
 
Sawa wangu ntampeleka buza sec hili hiyo hela ya kumpeleka marian nimtengenezee mazingira akimaliza awe na kitu chake
Sioni haja ya kumnyima mwanao elimu bora eti kwa sababu hakuna ajira

Kwa sababu kwa hilohilo unalosema la kumtengenezea mazingira, laiti kama ungekuwa na pesa za kutosha, ungempeleka Marian na still ungemtengenezea mazingira baada ya kumaliza.
 
Mzee sjaongelea hela nimeongelea mwanafunz anapomalza shule anakuwa hana cha kufanya si bora hiyo hela umtengenezee mazngra ya baadae

Hoja ni kwamba akilipa hiyo 15M

Mtoto akimaliza chuo asikae nyumbani mzazi awe amemwandalia cha kufanya.

Sio wote wanaokosa kitu cha kufanya, na reality ni kwamba hao wanaoenda hizo shule za gharama ndio wanopata connection za maana, ni % ndogo ndio utakuta wapo tu bila hili wala lile

Wengi wao ndio hao wanapata scholarships na kwenda kujisomea nje ya nchi na kupata kazi huko huko. Wengine utakuta wazazi wao ndio wana uwezo wa kuwapatia michongo ya maana ni kiasi cha kupiga simu moja tu.

Jaribu kufuatilia kwa umakini alumni wa hizo shule labda kuanzia graduates wa 2000s mpaka 2010s sasa hivi wapo wapi,(under the assumption wapo around 25-40 years old, umri ambao ni prime kwa kuchapa kazi/kujiajiri) utakuta % kubwa wamefika sehemu za maana...ukweli ni kwamba mwenye nacho huongezewa na maskini huporwa hata kidogo alichonacho.
 
Mtoa mada fungua akili yako mkuu. Mwanao haendi shule kusoma tu. Kuna exposure na watu tofauti na mambo tofauti.

Nilibahatika kusoma shule ya Feza O - level na A- level. Kiukweli nilivyoexperience pale vimenishape na kunisaidia katika mafanikio hadi leo hii.

Tulijengwa kwa spirit ya brotherhood na kusaidiana. Tulipewa fursa nyingi za kuwa bora zaidi mara kwa mara. Shule ilikuwa haiishi competition za mambo ya kompyuta, music, lugha ya kituruki, hesabu na mengine mengi. Na ulikuwa ukichaguliwa mnapewa free trip kwenda nje kwa ajili ya hiyo competition. Hata kama haushindi but kwa kuparticipate tu unakuwa unajijenga katika sekta flani na motivation zipo kila siku. Nakumbuka kuna dogo alikuwa anapiga gitaa flani la kituruki vizuri akawa anapiga safari Uturuki kila mwaka na alikuwa analipwa. By estimation mpaka anamaliza form 6 alikuwa ashalipwa yeye kama yeye zaidi ya 10m bila kuhesabu trip ambazo ni free.

Ukiachana na the fact kuwa tulisoma na watoto wa who is who pale ambapo unajenga fursa ya kuonana na wazee wao na kujenga urafiki wa baadae, bado hata after kugraduate unapata msaada. Ishu za kazi, biashara, na kujuliana hali ni nyingi sana kiasi cha kwamba graduates wa Feza hawahangaiki katika kazi kwa sababu ukiinform alumni na una vyeti vyako unapata connection chap. Can you imagine kuna ofisi ya alumni ambayo ina kila kitu na kama wewe ni alumni wa Feza unaweza kwenda hapo na kuitumia kama workspace yako bila charges zozote kwa muda wowote utakao? Totally free. Scholarship opportunities ndio usiseme.

Pia mahusiano ya uongozi na wanafunzi ni smooth sana. Walimu ni washkaji na ni approachable. Wanakujenga kama sibling ili ufanikiwe mbeleni. Hata baada ya kugraduate mambo ni mazuri sana.

Personal stori moja ni nilishawahi kupewa dili la 16 mil na mwalimu pale shule katika mwaka wangu wa kwanza wa chuo. Imagine 19 years old unaaminiwa na 16 mil. Kibongobongo ni ngumu sana ila mwalimu akanipa pande na hakutaka chochote.

Tafadhali sana kama una uwezo usichezee elimu ya mwanao. Shule si kwa ajili ya madaftari ila kunamshape yeye kama yeye na network yake kwa maisha yake yote.
 
Shida ni pale ambapo mzazi anajinyima hadi hatua ya mwisho plus vikoba ili mwanae asome private na akimaliza mtoto anabaki mzigo kwa mzazi na mzazi anakuwa mzigo kwa mtoto wanabaki wnaangaliana tu

Hilo ni tatizo sana
 
Back
Top Bottom