Kumng'oa Lowasa si tiba ya CCM, tiba yake ni kukaa pembeni mwa mchezo wa uongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumng'oa Lowasa si tiba ya CCM, tiba yake ni kukaa pembeni mwa mchezo wa uongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kinyamagala, Nov 23, 2011.

 1. Kinyamagala

  Kinyamagala Senior Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kimsingi nimekuwa nikifuatilia kwa kina hoja ya CCM ya kujitakasa kwa njia ya kujivua gamba.Dhana iliyomaanisha kuwaengua baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo LOWASA.Nawaita kwa jina zuri la viongozi na si MAFISADI kama mlivyozoea kwani jina hilo si la lazima ulitumie unapomtaja kiongozi yeyote sasa wa CCM kwani hiyo ni sifa ya msingi inayomwezesha mtu kushika nafasi ya juu ktk chama hicho.Ndo maana hata Igunga Dr Kafumu ndo alikuwa na sifa ya kuwa mgombea akiwa ametokea wizara kinara kwa rushwa naye akiwa mtuhumiwa wakati wapinzani wao wakuu ktk uchaguzi huo walimpata mwalimu KASHINDYE kuwa mgombea wao.Hakuwa na kashfa huyu.Tatizo la CCM si watu watatu,danganya watoto,tatizo ni mfumo mzima ulojengwa na kuimarishwa na awamu tofauti za uongozi ndani ya chama baada ya MWALIMU.Mzee Mwinyi alisimamia kuua Miiko ya uongozi kupitia Azimio la Zanzibar,Akaruhusu viongozi kutotenganisha wajibu wao kwa jamii ilowapa dhamana na matumizi ya dhamana hizo kwa maslahi yao binafsi.Mzee Mkapa akaimarisha mfumo wa uongozifisadi kwa kuhalalisha uongozi wenyewe kuwekwa mnadani[TAKRIMA]iba upate mtaji wa kuongoza,au kopa upate mtaji wa kununua uongozi ili baada ya kuupata uutumie kulipa na kujitajirisha,yeye mwenyewe akajimegea Net group solution,Kiwila colmine,na ndiye aloshadadia utandawizi.KIKWETE ni matunda ya mfumo ulobuniwa na awamu za nyuma hususani Mkapa kununua uongozi[TAKRIMA].Kazi hiyo ilifanywa kwa mafanikio makubwa chini ya kamanda wake wa kutekeleza mfumo nunua uongozi kama ilivyoasisiwa na Mkapa akishangiliwa na akina Mangula.Timu ya Lowasa ikashinda Kikwete Rais mpaka leo.Ukweli ni kwamba Lowasa,Chenge,Rostam ni moja ya wachezaji wazuri sana wa ngoma inayopigwa na CCM.Hiyo ni ngoma yao.Kilichopo ni wachezaji kuoneana wivu yaani fulani anacheza zaidi tumtoe tucheze sisi.Nani atweza kumtenga KWA MFANO Sitta na ufisadi?Je nyumba anayoishi sasa hivi ya uspika DAR kwa gharama kubwa anastahili?Mwakyembe hakuwa na mgongano wa kimaslahi ktk TANESCO akiwa mmoja wa wANAHISA ktk kuanzisha mradi wa kuzalisha umeme wa upepo SINGIDA?nani msafi?We need to overwhole the system[CCM].Na njia sahihi ya kuisafisha CCM ni kuiweka kando ya UTAWALA.Wakisafishika waweza kurudishwa madarakani
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwa afya ya taifa hili huyu anatakiwa ang`oke mapema mno!
  Hafai hata robo
   
 3. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2015
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Wacha tuchokonoe yaliyopita na wengine wasema wenzao nao wasomwe madhambi yao... yalipita vipi hadi na wao wawanyoshee wenzao vidole vya Macho.
   
Loading...