Kumlinganisha Mrema wa 1995 na Dr Slaa wa 2010 ni sawa na nuru ya Mwezi vs ya Jua

Ndugu, usivuke mipaka Mrema ni Mtanzania, Mume wa mtu, baba wa wanae anasthili heshima kama wewe mheshimiwa. He is not a lapdog.
 
Ccm wamefulia kweupeeee............mbona kila mtu anaipinga ccm?...huo ushindi wa kimbunga utatokana na nini?.....tumeichoka ccm na kikwete dhaifu na fisadi

Wanasema eti sisi si wapiga kura, tehe tehe tehe!!!!!!!!!!!
 
16 watu miaka hii wameaka, na hwadanganyiki tena, wamejua umuhimu wa kupiga kura.
 
14. Mrema hakuthubutu kutaja majina kwenye mabomu yake, lakini dr. Slaa amewataja wahusika kwenye mabomu yake
15.


ccm wanafikiri mazingira ya augustino lyatonga mrema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 ni sawa na dr. Wilbroad peter slaa katika uchaguzi mkuu wa 2010. Hivi hizi tofauti hawazioni? Endeleza tofauti hapo chini za chaguzi hizi mbili

tofauti
1. Dr. Slaa ana cv kali kuliko ile ya mrema ikiwemo degree ya juu, yaani phd wakati mrema alikuwa na ka-diploma tu; ni hvi juzi ndio amenunua ka-bachelor!!!

2. Dr. Slaa amekuwa mbunge kwa muda wa miaka 15 kwenye upinzani na kuonesha maendeleo makubwa jimboni kwake na hivyo ni mtu sawia ku-emulate hayo maendeleo kwa nchi nzima, mfano sekondari ya kwanza kuingi kwenye mtandao wa internet iko karatu

3. Kwenye kampeni zao wote wanavutia umati mkubwa, wote wana mabomu/ makombora ya kuelekea kwa ccm na serikali yake, lakini tofauti ni kuwa makombora ya mrema yalikuwa machache na wala hayakuwa na impact nzuri kwa maisha ya kila mtanzania kama yalivyo ya dr. Slaa (ya dr. Slaa ni laser guided, long range with a huge impact),

4. Makombora ya dr. Slaa yana ushahidi na anayatengeneza mwenyewe kwa kutumia utafiti na yanagusa kila nyanja, ya mrema kwenye nyanja chache na short lived na hakuna utafiti wa kugundua mabomu mengine,

5. Mrema alikuwa anaongelea makombora yake ambayo yalikuwa yanapoteza nguvu zake jinsi siku zinavyokwenda bila kutoa vision na mission ya kulikomboa taifa letu; dr. Slaa ana laser guided missiles ambazo hazikosi target, na yana-huge impact nzuri kwenye ubora wa maisha ya watanzania wote wakiwemo vitukuu vya ndungu zao mafisadi, makombora haya yamekuwa yakiboreshwa (update and upgrade) kwa kufanya utafiti wa kina wenye ubora,

6. Makombora ya mrema yalikuwa yanarushwa kwa rocket launcher lakini ya dr. Slaa yanarushwa kwa kutumia dege aina ya b52,

7. Mrema alikuwa ni silaha aina ya rpg/ ak-47 na dr. Slaa ni silaha mathubuti aina ya super missile launched from the b52, the bomber!

8. Wakati wa mrema demokrasia ya vyama vingi ilikuwa changa, kwa dr. Slaa imekomaa; pia 1995 watanzania walikuwa na single party hangover, 2010 hang over imekwisha ikichangiwa na ujio wa kizazi kipya,

9. Dr. Slaa anaongea lugha nane (8), mrema anaongea lugha mbili (3) ambazo ni kiswahili, kichagga na poor english!!!!!! Hivyo dr. Slaa atakuwa mzuri katika ushirikiano wa kimataifa na wala hatakuwa na makaratasi wakati atakapoongea na marais wa nje

10. Dr. Slaa amesoma nje ya nchi na kutembelea nchi nyingi, mrema alisomea nje ya nchi ushushu tu kwa muda mfupi na kutunukiwa diploma.

11. Mrema ni kigeugeu na ana jazba na kwa sasa yuko na ccm, dr. Slaa sio kigeugeu, ana uthubutu, mtaratibu.

12. Jimboni kwa dr. Slaa, karatu, miaka yote ccm ni chama pinzani katika baraza la la madiwani katika halmashauri, lakini mrema amewahi kuwa mbunge lakini katika majimbo hayo chama chake hakijawahi kuifanya ccm kuwa mpinzani katika baraza la madiwani.

13. Dr. Slaa is a leader, mrema is a lapdog!!

14.

Kwa kifupi kila zama ina historia yake, na ya mwaka huu ni kubwa kwa maana ukombozi umefika.
 
1995 masanduku ya kura yalikuwa yanakusanywa ofisi ya Halmashauri kisha kuhesabiwa, wizi ulikuwa ukifanyika njiani kwa kutumia polisi, this time kura zinahesabiwa kituoni palepale

1995 watu wengi waliomuunga mkono Mrema nikiwemo mimi hatukujiandikisha kupiga kura, tulibaki kutamani, this time kwa sababu ya kusajiri namba ya simu na kwa sababu ya kutafuta vitambulisho, wengi wetu tumejiandikisha....

1995 mrema aliishia kufanya mikutano 40 tuu kutokana na matatizo ya usafiri na kutumia mfumo wa CCM wa kufanya mkutano mmoja kwa siku ukitanguliwa na kwaya, ngonjera , muziki nk, this time, Dr Slaa anafanya mikutano hadi nane kwa siku kutumia helcopter, patamu hapa

1995 CCM ilikuwa taasisi na walifanya kazi kama timu hivyo waliweza hata kuiba kura, kufanya kampeni na kuhakikisha Ushindi, safari hii kuna mpasuko mkubwa CCM huku wenye cham wakiwa wamepokwa mamlaka na pesa za Kampeni ambazo anazo Ridhiwani, Ni mpasuko huu ndiyo silaha itakayoiua CCM kwani Makada wa CCM sasa hivi wanafanya kazi kinafiki wakijisemea pembeni, WANAJIFANYA KUJUA KAMPENI TUONE ITAKAVYOKUWA
 
Nyambala, you have had a good analysis! Huu ni mwaka wa Dr Slaa na CCM waache maji yafuate mkondo wake.
 
Miaka 15 iliyopita huwezi kulinganisha na sasa
Vijana waliokuwa na umri wa miaka mmitatu minne ndio wapiga kura wa mwaka huu hamjui mrema wa 1995 wanamjua mrema anayejikomba kwa KIKWETE na CCM kwa maana hiyo anayetumia hoja hizo kuwabadilisha mawazo watanzania anajidhihaki mwenyewe kwani hakuna tija hapo

Mengi wakati ule kwa kutmia TV yake aliwatiisha wananchi kwamba nchi itaingia kwenye umwagaji wa damu kama upinzani utachaguliwa leo vijana na wazee wa sasa wanajua Wabunge wa upinzani ndio waliiongoza kwa kuuliza maswali bungeni na kuiwajibisha serikali kwa mantiki hiyo wanaimani kwamba lazima watoe Raisi kutoka upinzani ili kuzidisha maendeleo ya nchii

Mwaka 1995 Nyerere alimnadi Ben Mkapa na sauti ya zege ikasaidia kubadilisha maono ya wananchi leo KIKWETE ananadiwa na Salma,Ridhiwani,Miraji,Beno Malisa,Januari na Yusuphu Makamba,Batlida na KInana ,kwa mantiki hiyo wanachi wanajua KIKWETE anataka kurudi madarakani ili familia yake ambayo inaendesha ufalme na usultani irudi madarakani kwa maana hiyo nguvu yake ni zero
Wananchi wenyewe wamechoka na CCM kwa hiyo hata ulinganishe na nini hata utoe ahadi gani hata Tambwe Hiza na Msabaha wafanye propaganda za mbinguni hakuna takaye badirika
Jinsi wanavyomlinganisha Mrema aliyechakachuliwa bora angekuwa amekufa lakini kwa jinsi alivyo hai na anavyojidhalilisha na alivyofilisika kisiasa ndipo wananchi wanavyoona DR Slaa ndio tunu ya taifa na ndio raisi wetu wa wa awamu ya tano
 


8. Agenda na ilani za uchaguzi.
Wakati mwaka 1995 wote Mrema na Mkapa walikuwa wakisisitiza kupambana na rushwa na ufisadi kutoka kwenye ilani za vyama vyao JK anaonekana kuogopa hata kutamka tu neno ufisadi.Ilikuwa rahihsi kuiamini CCM mwaka 1995 kwani walikuwa wananadi mtu mpya lakini kwa sasa 2010 JK ataaminikaje wakati 2005 alitueleza hayahaya anayotwambia sasa. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?



9. Nyerere “effect”
Ni ukweli ulio wazi kwamba Nyerere ndiye mwanasiasa aliyekuwa na uwezo wa kujenga hoja ikaeleweka nchi nzima na hata kukubalika. Aliaminika na kupendwa na watanzania walio wengi kwa sababu ya historia na uadilifu wake. Hivyo basi aliposimama 1995 kumkampenia Mkapa alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kumuongezea kura na hatimaye kumfanya shinde uchaguzi ule. Lakini je 2010 nani “Nyerere” wa CCM? Mkapa , nope? Mwinyi kidogo lakini bado hawezi kuvutia wananchi wakaamini JK will be different.


Hivyo basi 2010 siyo 1995. Get it??????


  1. Ni vigumu sana leo hii kuwadanganya watu kuliko ilivyokuwa mwaka 1995, kutokana na tekinohama ni rahisi zaidi kupata habari hivyo kuziba mianya ya uongo...
  2. Ukweli huvunja milima. Mtu anayesimamia ukweli ana nguvu zaidi kuliko yule anayeamini ghiliba. Kikwete hawezi kutumia mapambano dhidi ya rushwa kama mojawapo ya mambo anayotarajia kuyafanya, kwa sababu ameshindwa na hawezi kwa sababu adui anayetakiwa kupambana naye yuko nyumbani mwake na anaishi naye kwa mapenzi ya dhati. Akitumia turufu hii atashindwa kwa sababu atakuwa hasemi ukweli, nafsi yake itamsuta na atavuruga zaidi kuliko kukaa kimya. HANA MPANGO WA KUPAMBANA NA RUSHWA kwa sababu hili siyo tatizo kwake, UFISADI na RUSHWA ndizo zimemfanya afike hapo.
  3. Kutokana na ukweli kuwa wengi wanaosimamia haki na ukweli ama wamejitoa au kuenguliwa katika nafasi za maamuzi ya chama inakuwa ni vigumu kumpata "Nyerere wa CCM 2010" kwa sababu waliopo hawayaenzi ya mwalimu na kwa bahati mbaya wanamtumia kama njia nyingine ya kuwaghilibu wapiga kura.... pasipo kuwa na ukweli ni vigumu kujenga hoja ukaeleweka hasa hasa kama unaotaka kuwadanganya wanauwezo wa kuwa na taarifa sahihi
 
Kulikuwa na NCCR-MAGEUZI ya Mrema imepita, ikafata CUF ya Lipumba nayo ikapita hivyohivyo, wanachadema kaeni chonjo huu tunaouona sasa sio upinzani wa chadema bali mwanzo wa mwisho wa CHADEMA ya Dr slaa, mambo kujirudia ni kanuni ya historia huwa haikwepeki hata siku moja.




If not me who? and if not now when?
 
Katika mazingira gani ???? Hao wapiga kura wa enzi hizo hawakuwa wamepigika kama wa sasa.1995-2005 uchumi wa nchi ulikuwa imara, leo wapiga kura wanashinda kwa mlo mmoja, umaskini umezidi kukua, watu wanataka mabadiliko kuliko kipindi chochote kilichopita.USIJIDANGANYE KWA HOJA DHAIFU
 
Kweli CCM wanatakiwa kuelewa wakati huu ni mgumu sana!hii ngoma lazima waicheze kwa uangalifu mkubwa,vingine hali inaweza kuwa mbaya sana kwao!
 
Wahenga walisema giza linapozidi sio tu kwamba kunakaribia kukucha bali nyota huonekana vizuri zaidi. Watatapatapa sana, tutasikia mengi ila double p au p square nikiwa na maana PEOPLES' POWER itatufikisha tunapotaka kwenda!
 
mrema huwezi kumlinganisha na dr slaa, vitu vingi vime change kwenye game la politics in 15 years but all in all mrema is a living legend in tanzania politics. kwakuwa dr slaa amewataja mafisadi doesnt make him a good politition. huyo dr slaa amefanya nini kwa ajili ya mslahi ya wananchi hususani huko karatu. mpaka leo hakuna mpinzani aliefikia kura za mrema 1995, awe mbowe, lipumba na hato huyo dr slaa. chadema mnazunguka na helicopter huko vijijini watu wanakuja kushangaa helicopter umnadhni wapiga kura. ccm nao wanatumia fuso na daladala kubeba na kupeleka watu kwenye mikutano. chadema na dr slaa mtaanguka vibaya kwenye uchanguzi.

dr slaa atakosa uraisi na ubunge wa karatu ndio umeshapotea. mbowe alimdanganya agombee uraisi akijua tu atashindwa. ATABAKI KATIBU MKUU. then atadissapear kwenye politics za tanzania. chadema mnakelele sana kama washabiki wa man u na yanga
 
Wadau wamejitahidi sana kutoa analysis zao. Nyingi nakubaliana nazo, lakini pia zipo ambazo nazipinga. Kwa mfano wapo walisema kuwa Slaa ana Ph.D, Mrema hakuwa nayo. Japokuwa kiwango cha elimu ni muhimu sana kwa kiongozi, lakini sidhani kama itamfanya awe kiongozi bora. The fact that you posses a Ph.D does not make you a good leader. Mrema hakuwa na elimu kama ya Slaa lakini kwa maoni yangu alikuwa na leadership qualities.

Suala nyingine wakati Mrema akigombea urais tayari alikuwa ameshashika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ile ya Waziri wa Mambo ya Ndani. Nyadhifa za Slaa ninazozijua ni ubunge. Hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa Chadema. Ninachojaribu kusema ni kuwa he has never been tested kwenye nyadhifa za juu kabisa za uongozi. Of course, hili haliwezi kumzuia kuwa kiongozi mzuri, lakini experience kutoka sehemu mbali mbali za dunia zinaonyesha kuwa wapiga kura wako very caution na mgombea ambaye hajawa tested kwenye nyadhifa za juu kabisa za uongozi.

Pia wadau wamejadili suala la kurusha makombora. But dont see how this can make someone a good leader. Nafikiri Mrema alikuwa na mvuto sana kwa wananchi probably because walikuwa tayari wameshaona mambo aliyoyafanya wakati bado akiwa CCM. Slaa anaweza kuwa na sera na nia nzuri lakini nahisi kama vile hatapata idadi ya kura alizopata mrema.
 
Binafsi nimefarijika sana na haya matokeo ya wapinzani kuzoa majimbo. lakini wadau naomba mniondoe shaka yangu. historia ya huko tutokako inaonyesha ccm wanapoona mambo magumu huwa wanaamua kuwarubuni wapinzani na kuwaingiza kundini mwao (ccm). Inawezekana hawa jamaa wakatugeuka kama kina Lamwai? na je tuwafanyaje kama hii trust tuliowapa wataifisidi 2015? Mwenzenu nna wasiwasi
 
wewe ni MWEHU kwa kufananisha uchaguzi wa 2010 na 1995. Uwezo wako wa kufikiria na kupambanua mambo ni mdogo.MWAKA 95 ULIKUWA NI USHABIKI 2010 NI MABADILIKO ASILIA. sasa wewe nasikitika kwa kufananisha ushabiki na Uchungu!!! kuhusu wao kurudi kundini sio tatizo maana nguvu ya CHADEMA imeanzia kwa WANACHADEMA VIJANA ambao hata hao wazee walioingia wakiondoka SIO ISHU!! Weka hofu kwa vVIJANA WA CHADEMA KURUBUNIWA sio mtu kurudi kundini weweeeee:tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape::tape::A S angry::A S angry::A S angry:
 
Unaongelea mambo mawili tofauti sana, mambo ya Kizazi ambacho leo hakipo, hiki ni kizazi cha mabadiliko hasa, na hata kundi lilikokua nyumba ya washindi hawa wa chadema ni vijana wa miaka 25.
 
Back
Top Bottom