Kumlinganisha Mrema wa 1995 na Dr Slaa wa 2010 ni sawa na nuru ya mwezi vs ya jua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumlinganisha Mrema wa 1995 na Dr Slaa wa 2010 ni sawa na nuru ya mwezi vs ya jua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Oct 4, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Makamba na wanapropaganda wengine wa CCM wamekuwa wakitaka tulinganishe umaarufu aliokuwa nao Augustin L Mrema na ule anaopata mgombea urais kwa tiketi ya Chadema mwaka huu, Dr W Slaa kuwa unafanana na utakuwa na matokeo yanayofanana.

  Kuna tofauti kubwa nyingi na kubwa kati ya wagombea hawa wawili, pia kuna tofauti ya kimazingira ambayo inawatofautisha pia. Nitajaribu kuzijadili kwa uchache.

  Mrema (Mzee wa Kilalacha) pamoja na kuwa alikuwa na ufuasi mkubwa, uadilifu wake ulikuwa na maswali mengi ambayo hakuweza kuyajibu mpaka sasa ambapo ameyajibu katika vitendo vyake. Mrema alipigana vilivyo na uozo mwingi uliokuwepo wakati ule, lakini pia aliitumia nafasi hiyo kujinufaisha binafsi kwa kuchukua mgawo kutoka kwa wale aliowakamata au kuwatuhumu kuhujumu nji hii.

  Tangu kampeni zianze hatujasikia uadilifu wa Dr Slaa ukiwekewa mashaka tofauti na ile ya yeye kuwa na uchumba na mke wa mtu, katika utendaji wake wa umma hakuna popote ambapo tumesikia uwajibikaji na uadilifu wa mgombea huyu wa Chadema ukitiliwa mawaa.

  Wote wawili wanafanana katika ujasiri wao wa kufichua ufisadi uliokuwa unaofanywa na watawala, Mrema kwa wakati ule akiwa waziri katika serikali ya A H Mwinyiki alitaja waziwazi bila kificho uovu uliokuwa ukifanywa na wanafamilia na watu waliokuwa karibu na bosi wake na alidiriki hata kuwaamuru watendaji wa wizara yake kuwakamata. Dr Slaa ameonyesha ujasiri unaofanana na wa Mrema pale aliposimama hadharani kumtaja rais aliyeko madarakani miongoni mwa mafisadi wakubwa wa nchi hii (The First 11 in the List of SHAME), huu ni ujasiri unaotakiwa kwa kiongozi yeyote. Amekuwa mwiba kwa serikali katika ufisadi kupitia makampuni ya Meremeta, Tangold, MwananchiGold, Richmond, EPA, n.k.

  Hata hivyo watu hawa wawili wanatofautiana sana katika uwezo wao wa kuchanganua na kujadili mambo, jambo moja liliomwangusha Mrema katika uchaguzi wa 1995 ni uwezo mdogo aliouonyesha kwenye mdahalo wa marais wakati ule, alishindwa kabisa kujadili hoja zilizowekwa mbele yake na badala yake akaendelea kutaja tu vitu alivyofanya tofauti na maswali yaliyowekwa mbele yake yaliyomtaka ajadili na achanganue hoja.

  Dr Slaa kwa upande mwingine ameonyesha weledi wa hali juu inapokuja kwenye mijadala mbali mbali, uwezo huu ndio uliowafanya CCM wakatae kuwaruhusu wagombea wao wakiogopa kumkuta yaliyomkuta Mrema 1995, ya kushindwa kujadili hoja kwa weledi. Katika nyakati tofauti, Kikwete ameonyesha uwezo mdogo sana inapokuja kwenye mijadala ya wazi ambapo anakuwa hana hotuba iliyotayarishwa.

  Tukija kwenye upande wa mazingira, Mrema wa 1995 aliangushwa kwa kiasi kikubwa na uwezo wa kujenga hoja wa mgombe wa CCM wa wakati ule lakini Mkapa alikuwa na turufu ya Mwl J K Nyerere, wote tunakumbuka jinsi Mwalimu alivyobadilisha upepo baada ya kuamua kumuunga mkono Mkapa, kuanzia kwenye siasa za ndani za CCM, Mkapa alibebwa na uwepo wa Mwalimu nyuma yake. Ilipokuja kwenye kampeni na vyama vya upinzani, Mkapa alipata nguvu kubwa baada ya Nyerere kumpigia kampeni na hii ni TOFAUTI kubwa kati ya mazingira ya CCM na Mkapa mwaka 1995 na mazingira ya CCM na Kikwete mwaka 2010.

  Nyuma ya CCM na Kikwete wa 2010 wapo Mama Salma Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Abdulhaman Kinana, na wengine ambao uwezo wao wa kujenga hoja ni mdogo. Na kikubwa kabisa uadilifu wao ni wa mashaka, tofauti na uadilifu uliotukuka wa Mwalimu aliyemuunga mkono Mkapa.

  Mkapa/CCM ya 1995 walikuwa na turufu nyingine ya mhimu ya ugeni wa Mkapa katika siasa za Tanzania, Kikwete wa 2010 ni rais anayemaliza mda wake na wote tunaujua uwezo na udhaifu wake, ni tofauti kubwa na ahadi zisizotekelezeka za Mkapa za 1995 na ahadi za namna hiyo za Kikwete za 2010. Wakati tulikuwa na mashaka na uwezo wa kuzitekeleza zile ahadi tata za Mkapa 1995, tuna uhakika na kutotekelezwa kwa ahadi za ajabu za Kikwete za mwaka 2010.

  Tofauti hii kubwa wanaijua kwa ufasaha CCM na wanajua kuwa umati ulioko nyuma ya Dr Slaa kwenye mikutano yake ni habari mbaya wasiyoitaka CCM na kwa sababu hiyo wanajaribu kila mbinu bila mafanikio kumdhoofisha Dr Slaa kwa kumfananisha na Mrema (Nji hii).
   
 2. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  2010 kuna tofauti kubwa hasa katika uchambuzi wa mambo kwa wananchi walio wengi...
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  uelewa wa wananchi ni mkubwa sana kipindi hichi, Mrema alikuwa na nguvu sana mijini ambapo ni tofauti na sasa kwa Slaa ambaye mpaka kijijini ana nguvu
   
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kUNA TOFAUTI KUBWA KWENYE WAFUASI JAPO VYAMA WANAVYOTOKA VYOTE VINA USHAWISHI MKUBWA MAENEO YA KASKAZINI HUSUSAN KILIMANJARO..... MREMA ALIKUWA ANA USHAWISHI NA WAFUASI WENGI ILIFIKIA MAHALI POLISI WALIKUWA HAWANYWI MAJI NA NAKUMBUKA KWENYE MOJA YA MKUTANO WA MREMA ULIPIGWA MABOMU YA MACHOZI HADI MREMA MWENYEWE ALINYESHEWA MVUA YA MABOMU. MREMA ALISUKUMWA KWENYE GARI NA WAFUASI.... MREMA ALILIPUA BOMU LA HONGO YA MIL 900, MREMA, MREMA WELL MREMA NADHANI NI ZAIDI YA DR SLAA KWASABABU KWA KIPINDI KILE ANAGOMBEA URAIS ALIKUWA KESHASHIKA NAFASI NYINGI ZA JUU NA ALIFANYA MAMBO MENGI MAKUBWA.

  AWE NI SHUSHUSHU AU MSALITI LAKINI NI HUYU HUYU MREMA ALIEKUWA CHACHU YA VITUO VIDOGO VYA POLISI. KUNA MAMBO MENGI MAZURI MIMI HUWA NAMPA MTU HAKI YAKE INAPOBIDI SINACHUKI NA MTU UBAYA WAKE NI WAKE YAFAA TUCHUKUE MAZURI YAKE AS WELL KWANI HAKUNA BINADAMU ALIE KAMILIKA. HATA HUYO DR WATU WANAMSEMA SIJUI ETI KACHAKACHUA MKE WA MTU MIE NAONA HIZO NI NEGATIVES TU KUNA MAMBO MAZURI KAYAFANYA ALIPOKUWA MMOJA WA VIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI....NA HAYAPINGIKI JAPO KUWA SWALA LA KUSIMAMA KIDETE KUHUSU UFISADI CHADEMA WALILIBINAFSISHA ILA KWA UKWELI SIO CHADEMA TU HATA BAADHI YA WABUNGE NDANI YA CHAMA CHA CCM WALISIMAMA KIDETE LAKINI......KUSIMAMA KIDETE BUNGENI KUZUNGUMZA SANAAAA HAIAMANISHI MTU ANAWEZA KUONGOZA NCHI TAFAKARINI ENYI WAPENDA MAENDELEO NA MUSTAKABALI WA HII NCHI.
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  tatizo la wabunge wa ccm kuzungumzia ufisadi sawa lakini raisi Wao anawanadi mafisadi kuwa wamesingiziwa unataka nini wananchi wanaona kama chadema ndo nguzo iliyobaki kuupinga ufisadi.
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hoja zako Mtemi zimetulia sana, ila hiyo jezi yako inayofanana na Arsenal ndo imeharibu mambo. Nataka kuongezea vitu vya kimazingira kati ya zama za Mrema na Slaa (PhD)
  1. Mwaka 1995 mfumo wa vyama vingi ulikuwa ni mgeni kwa watanzania kwa hiyo wapigakura wengi kwao sisiemu ilikuwa ndo baba ndo mama, mwaka huu wale vijana waliozaliwa 1992 wkt mfumo unaanza wana haki ya kupiga kura na kwao ccm ni chama kama vingine kwakuwa vyote wamevikuta.
  2. Mwaka 1995 mbinu za kulinda kura hazikuwepo kwa hiyo Mrema aliishia kuibiwa kura nyingi sana kutokana na ulinzi feki na pia matokeo yalikuwa hayabandikwi vituoni kama ilivyo sasa, mwaka huu matokeo yanabandikwa vituoni na pia kuna pipoooooooooooz pawa ya kulinda kura. Nakushauri ukishapiga kura sogea mbali kdg na kituo, tulia linda kura yako usiende nyumbani. Huenda hata ulinganifu huu wa ccm unaletwa kuweka mazingira ya kuiba kura na kusema hata mrema ilikuwa hivihivi.
  3. Muamko mdogo wa kidemokrasia kwa watanzania mwaka 95 ulisababisha watu wengi wasijiandikishe kupiga kura kwa kutoelewa na wakawa ndio mashabiki wa mrema ktk mikutano. Mwaka huu ccm wamefanya kosa la karne na ndio linalompeleka Slaa (PhD) ikulu, nalo ni kusajili simu za mkononi huku kitambulisho cha mpigakura kikiwa ndio standard ya kila mtanzania wa kijiweni na vijijina kusiko na ajira. Ukiangalia takwimu za tcra watanzania wenye simu za mkononi wanazidi milioni 15 na karibu wote wana vitambulisho vitakavyowawezesha kupiga kura walivyovitumia kusajiri simu. Mfano halisi ni foleni iliyokuwepo dar siku za mwisho za uandikishaji, kulikuwa na bonge la nyomi hd JK akawaambia jamaa waongeze siku akidhania atakuwa na mpinzani dhaifu aweke rekodi ya kura nyingi. Hawawezi kuviuza kwakuwa vinatumika ktk mambo yao mengi. Karibu wote hawa ni kizazi kipya ambacho kiko very well informed na wanajua dhambi zote za JK na watampa kura Slaa (PhD)
   
 7. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Nimezaliwa 82. Mi naijua CHADEMA NA DR. Wa ukweli tu. Hawa sijui ccm sijui nini huwa nawaona uchuro tu kwangu. Chadema kuna siasa ya kisasa na hai.
   
 8. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  naichukia ccm kutoka rohoni kabisaa
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni ukweli usiopingika kwamba Dr. Slaa amezitikisa "establishments" za CCM na mashabiki wake vilivyo.Wengi wa hizo "establishments" wanajiuliza kulikoni? Inakuwaje Mgombea wetu mwenye nyota ya mng'ao na aliyependwa sana mwaka 2005 anakuwa mzigo na ngumu kumuuza?

  Hata hivyo kuna wanaoliwazana kwamba ah! Hii ni sawa na 1995, mara ya kwanza Tanzania ilipoendesha uchaguzi wa vyama vingi. Wakati ule Mkapa na Mrema waliakamiana vilivyo na CCM ilitikisika , mwisho wake Mkapa akaibuka mshindi kwa ushindi mwembamba kama ilivyoainishwa hapa chini

  Tanzania: October 29, 1995 Presidential Election
  Registered Voters: 8,929,969
  Votes Cast: 6,846,681 (76.67% of Registered Voters)
  Valid Votes: 6,512,745 (95.12% of votes cast)
  Null Votes: 333,936 (4.88% of votes cast)

  CANDIDATE - PARTY/VOTES (% of valid)

  Benjamin William Mkapa - Revolutionary Party of Tanzania 4,026,422 (61.82%)
  Augustino Lyatonga Mrema - National Committee for Constitutional Reform 1,808,616 (27.77%)

  Matokeo hayo finyu hapo juu yanayoaminiwa kuchakachuliwa kwa sana ndiyo yanayoipa japo pumzi CCM kwa sasa kwamba bado itaibuka mshindi kwenye uchaguzi wa Oktoba 31 mwaka huu. Lakini je 1995 ni sawa na 2010????????? Ufuatao ni muanisho wa tofauti kubwa zinazoakisi uwezekano mkubwa wa matokeo ya uchaguzi mwaka huu kuwa tofauti kabisa na yale ya 1995. My analysis is only biased in the two candidates, JMK na Dr. Slaa.

  1. Aina ya wagombea
  Mwaka 1995 wagombea wote walikuwa wapya na hakuna aliyekuwa raisi kabla. 2010 kuna mgombea mpya na raisi wa awamu ya nne. Mgombea mpya anapimwa zaidi kwa umakini na ahadi zake wakati "incumbent" pamoja na ahadi pia ana mapungufu anayotembea nayo yaliyojitokeza wakati wa utawala wake.  2. Uandikishaji wapiga kura.
  Zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura mwaka huu ni vijana (kihistoria huwa hawaogopi mabadiliko). Hawa sit u kwamba ni "potential" voters bali pia wamejiandikisha. Ikumbukwe kuwa mojawapo ya tambo kuu za CCM mwaka 1995 ilikuwa kwamba washabiki wa Mrema ni wahuni na hawajajiandikisha kupiga kura (ukweli kiasi). Tofauti na mwaka huu 2010. Kitambulisho cha kura ni mojawapo ya ID's muhimu kwa mtanzania hivyo zaidi ya 85% wamejiandikisha.  3. Mapokeo ya mabadiliko Vijijini
  Tofauti na ilivyokuwa 1995 ambapo mashabiki wa upinzani walikuwa ni kwenye miji tena ile mikubwa mikubwa tu. 2010 Tunashuhudia vijijini kukiwa na mwamko zaidi wa mageuzi pengine kuliko hata mijini. Bukombe, Busanda, Mbarali, Njombe, Mbozi mashariki ni mifano tosha.  4. Mtandao wa intaneti pamoja na vyombo vya habari
  Sio siri 2010 mtandao wa intaneti umechukua nafasi kubwa sana katika upashaji habari za uchaguzi wakati mwingine haraka zaidi kuliko vyombo vya habari (main stream media). Hii haikuwepo 1995. Lakini pia vyombo vya habari (sio habari leo, daily news, rai etc) vinaripoti matukio kwa uhuru zaidi kuliko 1995.

  5. Uelewa kuhusu vyama vingi

  Mwaka 1995 upinzani ulitafsirishwa na CCM kama vita na ukizingatia uchaguzi ulifanyika mwaka mmmoja tu baada ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda. Well "boy" hii ni 2010 tumeona mpaka wakuu wa wilaya kwenye kampeni za vyama vya upinzani. Wafanyakazi wa serikali walio wengi hawaogopi kusema hisia zao hadharani kuhusu upinzani na pia vijijini watu wameelewa kwamba upinzani unaleta chachu ya maendeleo. Walikuwa wanawasikiliza wapinzani kwenye bunge lilopita mfano Slaa, Zitto, Mdee etc.


  6. Oganaizesheni mbovu ya CCM
  Ni ukweli ulio wazi kwamaba CCM sasa haiko sawa kimpangilio. Ndiyo maana ya vurugu kwenye kura za maoni, makundi na maagizo tata kama kukimbia midahalo. CCM ya leo 2010 si ile ya 1995 ambayo mambo yalikuwa yanaendeshwa kwa vikao na kampeni kwa kamati za chama. Kampeni za sasa ni familia na marafiki zaidi. Nguvu yote ya CCM sasa iko mikononi mwa mwenyekiti ambaye naonekana kuyumba kifikra na kimwili.  7. Mashabiki damu wa CCM.
  Ikumbukwe kwamba CCM kama chma kikongwe nchini na chenye historia ndefu kina mashabiki "loyal" kulingana na mguso wake katika jamii. Hawa huwa hawasikii, hawaambiwi wala hawafundishiki wao ni CCM tu. Mwaka 1995 ni hawa ndiyo walioibeba CCM. Lakini kadri siku zinavyoenda MPAKA SASA 2010 na CCM yenyewe kujipambanua kwamba imekaa kimaslahi zaidi na ni ya wafanyabishara kundi hili linapotea kwa kasi. Na hapa ndipo JK aidha makusudi au kwa kutojua anaonekana kupotea mwelekeo kabisa ameshindwa kulikumbatia kundi hili kimatendo zaidi ya ulaghai wa kwenye majukwaa na kupiga picha na walemavu (kumradhi). Hii ndiyo base ya chama lakini sasa hivi wanaonekana kama "intruders" Umuhimu wanapewa kwenye uchaguzi tu. Pia ikumbukwe mwaka huu kuna wapiga kura "born in the 1990's" hawa CCM kwao is just like any party.  8. Agenda na ilani za uchaguzi.
  Wakati mwaka 1995 wote Mrema na Mkapa walikuwa wakisisitiza kupambana na rushwa na ufisadi kutoka kwenye ilani za vyama vyao JK anaonekana kuogopa hata kutamka tu neno ufisadi.Ilikuwa rahihsi kuiamini CCM mwaka 1995 kwani walikuwa wananadi mtu mpya lakini kwa sasa 2010 JK ataaminikaje wakati 2005 alitueleza hayahaya anayotwambia sasa. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?  9. Nyerere "effect"
  Ni ukweli ulio wazi kwamba Nyerere ndiye mwanasiasa aliyekuwa na uwezo wa kujenga hoja ikaeleweka nchi nzima na hata kukubalika. Aliaminika na kupendwa na watanzania walio wengi kwa sababu ya historia na uadilifu wake. Hivyo basi aliposimama 1995 kumkampenia Mkapa alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kumuongezea kura na hatimaye kumfanya shinde uchaguzi ule. Lakini je 2010 nani "Nyerere" wa CCM? Mkapa , nope? Mwinyi kidogo lakini bado hawezi kuvutia wananchi wakaamini JK will be different.

  10. 2010 ni Dr. Slaa.
  1995 alikuwa Mrema aliyehama kutoka CCM na kuingia NCCR mageuzi in just 3 months akatangazwa kuwa mgombea urais. 2010 nni Dr. Slaa mgombea makini mwenye CV inayouzika ndani yah chama kilichojijenga taratibu mpaka kufika hapo kilipo.

  Hivyo basi 2010 siyo 1995. Get it??????
   
 10. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Imetulia mkuu, tathmini nzuri!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Umesahau moja kuwa kuna wapiga kura wengi mwaka huu ambao walikuwa watoto wadogo sana mwaka 1995 na hadi leo hii wamekuwa wakiona watoto wa viongozi wa CCM pamoja na wapambe wao wafanyabisahara ndio wakipata tenda nzuri za serikali, elimu nzuri na kuandaliwa kuchukua madaraka ya nchi, lakini wao wenyewe wakijengewa shule zisizo na waalimu na mwishowe kuishia kuwa machinga, ambapo serikali hiyo ya CCM inahamasisha wawe machinga zaidi kwa kuahidi kuwajengea machinga complex nyingine nyingi badala ya kujenga shule nzuri nyingi. Kundi hili lina hasiara sana na CCM kuliko CCM inavyojijua, na hao ndio watakaoiadhibu sana CCM.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yea mkuu this is a good one ngoja ntaiongeza!
   
 13. Mubezi

  Mubezi Member

  #13
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  unajua CHICHIEM wanajua kuwa watu ni walewale wa mwaka 1995,wanafikiri kuwa bado DHAMBI yao kubwa ya kuwapotosha wananchi kifikra kuwa HAIWEZEKANIKI bado inafanya kazi,wamekuwa wakipotosha jamii,kuwa kila jambo haliwezekani,hawajui kuwa kila kitu duniani kimedungulika kwa majaribio.Wao wana sera HAIWEZEKANINIKI,je utafanikiwaje bila ya kujaribu.Mtu hakibuni kitu anakamatwa,ukisema utafanya ili bure wao HAIWEZEKANI,wanachojua wao ni BARABARA ndio maendeleo,Kaka mwaka huu hatudanganyiki,watu wameelimika wanauchungu kwa kumuona rith1 anabadilisha magari kila siku wakati tumesoma nae chuo,na sasa sisi tupo mtaani,yeye anatesa.
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  tumekuelewa subiri maamuzi ya watanzania wengi october 31st
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Ccm wamefulia kweupeeee............mbona kila mtu anaipinga ccm?...huo ushindi wa kimbunga utatokana na nini?.....tumeichoka ccm na kikwete dhaifu na fisadi
   
 16. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  CCM wanafikiri mazingira ya Augustino Lyatonga Mrema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 ni sawa na Dr. Wilbroad Peter Slaa katika uchaguzi mkuu wa 2010. Hivi hizi tofauti hawazioni? Endeleza tofauti hapo chini za chaguzi hizi mbili

  Tofauti
  1. Dr. Slaa ana CV kali kuliko ile ya Mrema ikiwemo degree ya juu, yaani PhD wakati Mrema alikuwa na ka-diploma tu; ni hvi juzi ndio amenunua ka-bachelor!!!

  2. Dr. Slaa amekuwa mbunge kwa muda wa miaka 15 kwenye upinzani na kuonesha maendeleo makubwa jimboni kwake na hivyo ni mtu sawia ku-emulate hayo maendeleo kwa nchi nzima, mfano sekondari ya kwanza kuingi kwenye mtandao wa internet iko Karatu

  3. Kwenye kampeni zao wote wanavutia umati mkubwa, wote wana mabomu/ makombora ya kuelekea kwa CCM na serikali yake, lakini tofauti ni kuwa Makombora ya Mrema yalikuwa machache na wala hayakuwa na impact nzuri kwa maisha ya kila mtanzania kama yalivyo ya Dr. Slaa (ya Dr. Slaa ni laser guided, long range with a huge impact),

  4. Makombora ya Dr. Slaa yana ushahidi na anayatengeneza mwenyewe kwa kutumia utafiti na yanagusa kila nyanja, ya Mrema kwenye nyanja chache na short lived na hakuna utafiti wa kugundua mabomu mengine,

  5. Mrema alikuwa anaongelea makombora yake ambayo yalikuwa yanapoteza nguvu zake jinsi siku zinavyokwenda bila kutoa VISION na MISSION ya kulikomboa taifa letu; Dr. Slaa ana laser guided missiles ambazo hazikosi target, na yana-huge impact nzuri kwenye ubora wa maisha ya watanzania wote wakiwemo vitukuu vya ndungu zao mafisadi, makombora haya yamekuwa yakiboreshwa (update and upgrade) kwa kufanya utafiti wa kina wenye ubora,

  6. Makombora ya Mrema yalikuwa yanarushwa kwa rocket launcher lakini ya Dr. Slaa yanarushwa kwa kutumia dege aina ya B52,

  7. Mrema alikuwa ni silaha aina ya RPG/ AK-47 na Dr. Slaa ni silaha mathubuti aina ya super missile launched from the B52, the bomber!

  8. Wakati wa Mrema demokrasia ya vyama vingi ilikuwa changa, kwa Dr. Slaa imekomaa; pia 1995 watanzania walikuwa na single party hangover, 2010 hang over imekwisha ikichangiwa na ujio wa kizazi kipya,

  9. Dr. Slaa anaongea lugha nane (8), Mrema anaongea lugha mbili (3) ambazo ni Kiswahili, Kichagga na poor English!!!!!! Hivyo Dr. Slaa atakuwa mzuri katika ushirikiano wa kimataifa na wala hatakuwa na makaratasi wakati atakapoongea na marais wa nje

  10. Dr. Slaa amesoma nje ya nchi na kutembelea nchi nyingi, Mrema alisomea nje ya nchi ushushu tu kwa muda mfupi na kutunukiwa diploma.

  11. Mrema ni kigeugeu na ana jazba na kwa sasa yuko na CCM, Dr. Slaa sio kigeugeu, ana uthubutu, mtaratibu.

  12. Jimboni kwa Dr. Slaa, Karatu, miaka yote CCM ni chama pinzani katika baraza la la madiwani katika halmashauri, lakini Mrema amewahi kuwa mbunge lakini katika majimbo hayo chama chake hakijawahi kuifanya CCM kuwa mpinzani katika baraza la madiwani.

  13. Dr. Slaa is a leader, Mrema is a lapdog!!

  14.

  Kwa kifupi kila zama ina historia yake, na ya mwaka huu ni kubwa kwa maana ukombozi umefika.
   
 17. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Lingine kubwa litakaloiondoa CCM, tofauti na 1995, ni kuwa watu tumepigika hasa. Mchele 1500, Sukari 1600, Diesel 1700, mkate 800...watu wako hoi. Watu wanakula mlo mmoja tu.

  Halafu safari hii, wale vijana waliozaliwa mwaka 1992, mwaka ambao vyama vingi vilirejea tena, ni wapiga kura. Hakuna cha CCM imewalea, imewasomesha....Hakuna ilichokifanya kwao, na wana hasira.

  Vile vile, kuongezeka kwa vyuo vya elimu ya juu na idadi ya wanafunzi katika vyou hivyo ni mwiba kwa CCM. Chagua CHADEMA, Chagua Dr. Wilbroad Slaa.
   
 18. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Unjua mambo mengine ndugu zangu watanzania sio lazima kufikiri ila hata tahaaira ataona tu.we jk anahaidi ahadi mpaka sasa ni 70 halafu idadi ya siku anazoomba ni 1875 yaani miaka 5.ukigawanya kwa idadi ya ahadi ni kwamba kila ahadi inatakiwa ikamilike ndani ya siku 26.sasa basi je jk ataweza kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa vitatu kwa siku 26?je ataweza kununua meli 3 kwa siku 26 kama alivyoahid?nijuavyo na nipo tayari kurekebishwa,gari tu kutoka japani ukiagiza linachukua zaidi ya mwezi.itakuwa meli 3?barabara za flyovers kwa dsm zitawezekana kwa huo mda wakati mandela road imeanza kujengwa tangu anaingia madarakani mpaka sasa anatoka?eti tegeta mpaka ubungo watatumia treni.ye na waindi wake si ndo wamelifisadi trl?sas treni gani tena?du mi nimechoka bana mnisamehe.shame on you mtu mzima unakuwa tapeli.sidanganyiki.tutakutana 31 october.
   
 19. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  15. 2010 Watu wengi wanaokwenda kwenye campaign wamejiandikisha.
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  1. Mreama ni Mrema na Dr Slaa ni Dr Slaa
  2. 1995 sio 2010
   
Loading...