Kumlazimisha mjamzito kupima UKIMWI pamoja na aliyempa mimba ni kumuumiza kisaikolojia (Incase aliyempa amemkana)

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
Serikali iangalie hili suala la ulazima wa wajawazito kupima na waliowapa mimba.

Zahanati na kila sehemu inayotoa huduma ya wajawazito imekuwa ni lazima waende na waume zao kupima UKIMWI, hili sio suala baya kwa sababu ya mtoto atakayezaliwa.

Lakini nadhani ni muhimu kutoa ushauri kwa majmzito kuliko kulazimisha mama husika aje na mumewe, what if mwanamke amekataliwa na aliyempa mimba, inakuwaje kama alibakwa? Vipi kuhusu hawa wahudumu nk ambao hupata watoto kwa watu wasiowajua au hata kama wanawajua wanakuwa hawako tayari kuwapokea.

Je, sio kwamba tunawaumiza wanawake kwa kuwalazimisha kuja na wanaume, na wao wana maumivu ya kutelekezwa na waliowapa mimba, au maumivu ya lifestyle yao?

Sikatai kuona umuhimu wa swala la kumlinda mtoto, lakini tuwe na double standards ili tusije kumuumiza mama kisaikolojia. Kama wauguzi watakuwa makini wataona taarifa nyingi za wazazi wa kiume zinazojazwa huwa ni za uwongo, aidha wadanganye kazi za wazazi wenzao au kusema kuwa wamekufa.

Kama mtakuwa makini mtaona sura za wazazi hubadilika wanapojibu kuhusu waume zao, mara nyingi huwa ni maumivu kwao. Tupunguze uwongo! Tujue kabisa family planning kwetu bado ndogo sana hivyo ni ngumu kwa mtu kuwa na mume ambaye amempatia mimba bila mipango ya awali.

Wenyewe mnashuhudia idadi ya singe mothers, hii inaonyesha ukosefu wa ushirikiano baina ya wazazi na wao.

1573814232188.png

Nawasilisha!
 
Ni muhimu couple kupima lakini si lazima ,hakuna clinic inayokataa kumuhudumia mama kwa kuwa hajaja na mwenza, nimeona mara nyingi wanawake ndio wanaopima kuliko wanaume.
 
nikienda kuanza clinic Next month
ntawaeleza hali halisi imabidi tujikaze tu wakiniambia niwape No ya baba K ntawaambia Hata mimi binafsi sina maana baba K katorokea Thailand nikipata baba K Mlezi ntamuwasilisha..
wamuache baba K wangu mkataa mimba aenjoy bila kujali tunakaaje vikao

nacheka kama mazuri
 
Una utani mbaya. Aliyetorokwa anaandika Kama wewe ulivyoandika?
 
Una utani mbaya. Aliyetorokwa anaandika Kama wewe ulivyoandika?
unadhani natania mkuu
niko serious ndo mana nmesema nacheka kama mazuri.Moyo umekufa ganzi "Nmehangaika vya kutosha, Kama dunia imejaa singomaza's basi na mimi naelekea kuongeza hesabu yao" Hata nikilia haisaidii bora nicheke tu
 
Take a heart....hauko peke yako. Wanawake wengi nawajua tena wengine ni wana familia baada ya hawa mbuzi pori kukojoa na mkojo wao kujaa tumboni hawaonekani eti wako bize.
 
Back
Top Bottom