Kumkopesha mtu zama hizi ni kutafuta uadui

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,509
8,823
Wakuu,
Kusaidizana ni kitu cha kawaida kwa binadamu, ni ishara ya utu na upendo, pia huongeza mshikamano na kuaminiana.

Nilimkopesha mjomba wangu laki mbili akidai atanirudishia baada ya mwezi mmoja, ilipofika Kati kati ya mwezi wa makubaliano akakopa tena Tsh laki moja na nusu kwa miadi ya kurejesha kiasi chote, wakuu huu ni mwezi wa tatu hakuna pesa iliyorudi wala dalili za kulipwa deni langu hamna, nimeamua kumpotezea tu.

Juzi kuna rafiki yangu wa karibu yupo mkoa mwingine na yeye alinipigia simu akitaka nimkopeshe elfu ishirini atarudisha baada ya siku tatu, nikamuamini nikamtumia leo hii ni wiki ya nne kimyaaaaa hakuna dalili ya kulipwa deni langu,

Wakuu hivi nakosea kuwakopesha watu?? Je roho mbaya inalipa?? Je ninyi mnakabiliana vipi na hii hali?
 
Wote walikuja na gia ya kuniuliza kama nimelipwa au sijalipwa maana wanajua shughuli yangu nikawaambia ndio, ndio wakaanza swaga za kukopa, niliogopa kuwanyima sababu ningeonekana mbinafsi lakini mwisho wa siku hawalipi.

Na kakibarua kangu kalikuwa ka muda mfupi
Hapa nawaza kuwa na roho ya korosho wema haulipi
 
Uaminifu zama hizi haupo. Nilimkopea jamaa angu laki tisa kwa makubaliano kuwa atazirekesha ndani ya wiki mbili, mwezi 10 mwishoni, baada ya kumtumia akawa hapokei simu wala SMS hajibu. Nikafika kwake hakuja kunipokea akazima simu mpaka jioni akaja na mimi nilifika SAA tatu asubuhi.

Nikamwambia anipe pesa yangu, hakuwa nayo, akaniacha home kwake na familia yake kama siku mbili hivi nikaona nirudi tu kwangu maana mwenye mji kakimbia kwake. Nikawasiliana nae kwenye simu nikamwomba anisaidie laki na nusu kwanza, kumbe alisema sawa ili niondoke tu kwake.

Niliporudi zangu mjini hapokei simu wala nini na wala hataki kujua nini kinaendelea kwangu. Juzi Jumatano niliwekwa ndani na jamaa yangu maana nilimkopa laki nne kuongezea na yangu iliitimie tisa, anaona namzungusha. Ni kweli namzungusha kwasababu ya MTU mwingine. Hili linaniuma sana sana, kwanini nijitoe kwenye shida ya MTU halafu anilipe hivi. Leo amepokea simu ananiambia "hela sina kwahiyo nifanyeje sasa kama umewekwa ndani" akakata simu. Inauma sana, kuna mambo kwenye maisha yanauma mno.
 
Uaminifu zama hizi haupo. Nilimkopea jamaa angu laki tisa kwa makubaliano kuwa atazirekesha ndan ya wiki mbili ,mwezi 10 mwishoni , baada ya kumtumia akawa hapokei simu wala SMS hajibu. Nikafika kwake hakuja kunipokea akazima simu mpaka jioni akaja na Mimi nilifika SAA tatu asubuhi .

Nikamwambia anipe pesa yangu ,hakuwa nayo ,akaniacha home kwake na familia yake kama siku mbili hivi nikaona nirudi tu kwangu maana mwenye mji kakimbia kwake. Nikawasiliana nae kwenye simu nikamwomba anisaidie laki na nusu kwanza ,kumbe alisema sawa ,ili niondoke tu kwake.

,nilipo rudi zangu mjin hapokei simu wala nn na wala hataki kujua nini kinaendelea kwangu. Juzi jumatano niliwekwa ndani na jamaa angu maana nilimkopa laki nne kuongezea na yangu ili itimie tisa , anaona namzungusha. Ni kweli namzungusha kwasababu ya MTU mwingine. Hili linaniuma sana sana ,kwanini nijitoe kwenye shida ya MTU afu anilipe hivi. Leo amepokea simu ananiambia "hela sina kwahiyo nifanyeje sasa kama umewekwa ndan" akakata simu. Inauma sana . kuna mambo kwenye maisha yanauma mno
Muwe mnasoma nyakati za kumdhamini mtu kifedha. Halafu unapomdhamini hakikisha kile kiasi cha pesa unakimudu hata yakitokea ya kutokea.
 
Uaminifu zama hizi haupo. Nilimkopea jamaa angu laki tisa kwa makubaliano kuwa atazirekesha ndan ya wiki mbili ,mwezi 10 mwishoni , baada ya kumtumia akawa hapokei simu wala SMS hajibu. Nikafika kwake hakuja kunipokea akazima simu mpaka jioni akaja na Mimi nilifika SAA tatu asubuhi .

Nikamwambia anipe pesa yangu ,hakuwa nayo ,akaniacha home kwake na familia yake kama siku mbili hivi nikaona nirudi tu kwangu maana mwenye mji kakimbia kwake. Nikawasiliana nae kwenye simu nikamwomba anisaidie laki na nusu kwanza ,kumbe alisema sawa ,ili niondoke tu kwake.

,nilipo rudi zangu mjin hapokei simu wala nn na wala hataki kujua nini kinaendelea kwangu. Juzi jumatano niliwekwa ndani na jamaa angu maana nilimkopa laki nne kuongezea na yangu ili itimie tisa , anaona namzungusha. Ni kweli namzungusha kwasababu ya MTU mwingine. Hili linaniuma sana sana ,kwanini nijitoe kwenye shida ya MTU afu anilipe hivi. Leo amepokea simu ananiambia "hela sina kwahiyo nifanyeje sasa kama umewekwa ndan" akakata simu. Inauma sana . kuna mambo kwenye maisha yanauma mno
Pole sana lakini angalau umepata funzo
 
Wakuu,
Kusaidizana ni kitu cha kawaida kwa binadamu, ni ishara ya utu na upendo, pia huongeza mshikamano na kuaminiana,

Nilimkopesha mjomba wangu laki mbili akidai atanirudishia baada ya mwezi mmoja, ilipofika Kati kati ya mwezi wa makubaliano akakopa tena Tsh laki moja na nusu kwa miadi ya kurejesha kiasi chote, wakuu huu ni mwezi wa tatu hakuna pesa iliyorudi wala dalili za kulipwa deni langu hamna, nimeamua kumpotezea tu,

Juzi kuna rafiki yangu wa karibu yupo mkoa mwingine nayeye alinipigia simu akitaka nimkopeshe elfu ishirini atarudisha baada ya siku tatu, nikamuamini nikamtumia leo hii ni wiki ya nne kimyaaaaa hakuna dalili ya kulipwa deni langu

Wakuu hivi nakosea kuwakopesha watu?? Je roho mbaya inalipa?? Je ninyi mnakabiliana vipi na hii hali?
Mi laki mbli saizi sijibiwi txt Wala Simu hapokei yaani Nina mpango nkamfungulie kesi aiseeh
 
Juzi kuna rafiki yangu wa karibu yupo mkoa mwingine nayeye alinipigia simu akitaka nimkopeshe elfu ishirini atarudisha baada ya siku tatu, nikamuamini nikamtumia leo hii ni wiki ya nne kimyaaaaa hakuna dalili ya kulipwa deni langu,

Aiseeeeee
 
Uaminifu zama hizi haupo. Nilimkopea jamaa angu laki tisa kwa makubaliano kuwa atazirekesha ndan ya wiki mbili ,mwezi 10 mwishoni , baada ya kumtumia akawa hapokei simu wala SMS hajibu. Nikafika kwake hakuja kunipokea akazima simu mpaka jioni akaja na Mimi nilifika SAA tatu asubuhi .

Nikamwambia anipe pesa yangu ,hakuwa nayo ,akaniacha home kwake na familia yake kama siku mbili hivi nikaona nirudi tu kwangu maana mwenye mji kakimbia kwake. Nikawasiliana nae kwenye simu nikamwomba anisaidie laki na nusu kwanza ,kumbe alisema sawa ,ili niondoke tu kwake.

,nilipo rudi zangu mjin hapokei simu wala nn na wala hataki kujua nini kinaendelea kwangu. Juzi jumatano niliwekwa ndani na jamaa angu maana nilimkopa laki nne kuongezea na yangu ili itimie tisa , anaona namzungusha. Ni kweli namzungusha kwasababu ya MTU mwingine. Hili linaniuma sana sana ,kwanini nijitoe kwenye shida ya MTU afu anilipe hivi. Leo amepokea simu ananiambia "hela sina kwahiyo nifanyeje sasa kama umewekwa ndan" akakata simu. Inauma sana . kuna mambo kwenye maisha yanauma mno
Nadhani pesa ya kukopeshwa na mtu huwa inaleta kama laana hivi. Yaani kuna wakati mtu uliyemkopesha baadae anavyo-behave hadi unajiuliza ni yeye kweli!?
 
Dah nilijua ni mimi tu naumia kumbe tuko wengi, sasa hivi nimejifunza ni bora mtu aniambie nimsaidie amekwama anahitaji kiasi fulani cha pesa kuliko neno nikopeshe
 
Wakuu,
Kusaidizana ni kitu cha kawaida kwa binadamu, ni ishara ya utu na upendo, pia huongeza mshikamano na kuaminiana,

Nilimkopesha mjomba wangu laki mbili akidai atanirudishia baada ya mwezi mmoja, ilipofika Kati kati ya mwezi wa makubaliano akakopa tena Tsh laki moja na nusu kwa miadi ya kurejesha kiasi chote, wakuu huu ni mwezi wa tatu hakuna pesa iliyorudi wala dalili za kulipwa deni langu hamna, nimeamua kumpotezea tu,

Juzi kuna rafiki yangu wa karibu yupo mkoa mwingine nayeye alinipigia simu akitaka nimkopeshe elfu ishirini atarudisha baada ya siku tatu, nikamuamini nikamtumia leo hii ni wiki ya nne kimyaaaaa hakuna dalili ya kulipwa deni langu,

Wakuu hivi nakosea kuwakopesha watu?? Je roho mbaya inalipa?? Je ninyi mnakabiliana vipi na hii hali?
Wewe unasema miezi mitatu. Mimi ni mwaka sasa na jamaa kila siku namuona baa ananunulia wanawake bia tanotano. Acha kabisaa
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom