OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 3,601
- 9,064
Wakuu,
Kusaidizana ni kitu cha kawaida kwa binadamu, ni ishara ya utu na upendo, pia huongeza mshikamano na kuaminiana.
Nilimkopesha mjomba wangu laki mbili akidai atanirudishia baada ya mwezi mmoja, ilipofika Kati kati ya mwezi wa makubaliano akakopa tena Tsh laki moja na nusu kwa miadi ya kurejesha kiasi chote, wakuu huu ni mwezi wa tatu hakuna pesa iliyorudi wala dalili za kulipwa deni langu hamna, nimeamua kumpotezea tu.
Juzi kuna rafiki yangu wa karibu yupo mkoa mwingine na yeye alinipigia simu akitaka nimkopeshe elfu ishirini atarudisha baada ya siku tatu, nikamuamini nikamtumia leo hii ni wiki ya nne kimyaaaaa hakuna dalili ya kulipwa deni langu,
Wakuu hivi nakosea kuwakopesha watu?? Je roho mbaya inalipa?? Je ninyi mnakabiliana vipi na hii hali?