Kumkataza Magufuli kubomoa majengo yaliyojengwa kwenye hifadhi za barabara ni ujinga mkubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumkataza Magufuli kubomoa majengo yaliyojengwa kwenye hifadhi za barabara ni ujinga mkubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hakikwanza, Mar 25, 2011.

 1. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Mimi binafsi na muunga mkono Mheshimiwa waziri kwa kubomoa majumba yaliyojengwa kwenye hifadhi za barabara na yote yanayoendelea kujengwa.Unajua kuna watu hadi sasa wanaendelea kujenga majumba ktk hifadhi za barabara ukimuuliza anakwambia kwani zitajengwa leo hizo barabara? Halafu ikibomolewa anataka fidia,pia nyumba hizi zinaleta ajali,unakuta saa nyingine gari limekata breki dreva inatakiwa atafute eneo la usalama wa kujiokoa,sasa eneo la usalama ni hifadhi ya barabara nahapo unakuta nyumba zimejengwa,Dreva anagonga hizo nyumba kujiokoa au anabaki barabarani kuhofia kugonga watu wengi na baadae ni maafa makubwa yanatokea.Halafu watu wanakurupuka kumkataza bila vigezo huu ni upuuzi.Pia mpangilio wa makazi umekuwa mbovu kwa kuwa karibu na barabara kwani barabara ni nyembamba halafu majumba yamezikaribia hivyo hata ukiharibikiwa na gari hakuna sehemu ya dharura ya kuegesha gari hasa mijini,hivyo gari unakuta limeegeshwa barabarani na kuwa chanzo cha ajali.PIA WATANZANIA HATUJAMBO KWA KUVUNJA SHERIA UKIANZA NA VIONGOZI WETU NA BAADAE MWANANCHI WA KAWAIDA sasa mheshimiwa anakomesha wengine wanakuja na matamko ya kumpinga huu ni ujuha haswa.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hapo ni sawa na kuahirisha msiba ila kufa mtu kesha kufa kuna siku tutazika.
  Hayo majengo yatajabomolewa iwe leo au kesho tena kwa aibu kubwa.

  Hifadhi ya barabara inatumika kwa mambo mengi ya kimaendeleo mfano kupitisha mabomba ya maji taka/safi,umeme,simu,gesi na yanatakiwa yapishane kwa distance flani flani.
  pia ni njia ya dharura in case things go wrong.(HAPA JK anatuamianisha hayo matumizi yatafanyika huku nyumba zikiwepoo kama si ujinga)?
  Pili Magufuli hajavunja sheria wajenzi ndio waliovunja sheria sasa JK anasupport wavunja sheria
   
 3. m

  mbinayamaswa Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uifikilie kubomoa tu, hawa watu waliojenga kwenye maeneo hayo wamepewa viwanja na halmashauri za miji na majiji, hivyo uamzi wa kubomoa bila kufuata utaratibu siyo haki ya msingi, wakulaumiwa ni watu wa mipango miji na idara ya ardhi ya eneo husika , vilevile serikari hawaweki vigingi vya kuonyesha mipaka kwa mda muafaka, unapimiwa kiwanja inachukua miaka 10 kuweka vielelezo vya eneo , lakini yote haya ni kutokana na kutokuwa makini kwa serikali yetu, na ufisadi ndiyo chimbuko la hayo yote
  hivyo waliomkataza magufuri wako sahihi . unadhamini ghari kuliko binadamu????????????
   
 4. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wanamzuia Magufuli kwa kuogopa kukosa KURA miaka ijayo... Vile vile wanafikiri wanampunguzia UMAARUFU,.Akili zao hazijajua watu walishachoka nao.. Eti kutetea wananchi ni kuacha kubomoa nyumba zao walizozijenga barabarani... Hapo hakuna kitu..
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hapo red sasa kama kosa sio la Magufuli ya nini kumdhalilisha?kwa nini serikali isiwachukulie hatua kali hao maofisa uliowajata?
  DECI mchezo mchafu na haramu naunga mkono serikali kuufuta manake lilikuwa janga ILA kwa nini serikali ISIWACHUKULIE HATUA MAOFISA WAKE WALIOWAACHA DECI WAFANYE UPUPU WAO WA KUWALAGHAI WANAINCHI?
  JK aliogopa pale Magufuli aliposema 'hata majengo ya CCM napomoa"
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  haa haaaaaaaaa haaaaaaaaaaa ... mkuu punguza hasira...!
   
 7. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ukifanya kazi na ****** halafu aone au ahisi unapata sifa nzuri kumzidi lazima aweke mizengwe tuu!!
   
 8. n

  ngoko JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanamwekea kidhibiti mwendo asije akamaliza mtaji wa CCM wa 2015
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  waziri ngwini.

  rais ngwini.

  ndiyo maana hata wakikatazana hawawezi kujenga hoja kihandisi.
   
 10. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Duuh, mmezugwa mkazugika!! bado mnawaza CCM inaowachapa kazi, Magufuli,jk,Pinda lao moja wanatucheza shere! kajifunze Polituical game uone sio kukumbilia kushika mwenge wa upambe!!
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  jk si bingwa wa kusahahu!?

  nakumbuka ajali moja ilishawahi kutokea eneo la Kimara ambapo gari iliacha njia na kugonga nyumba iliyokuwa kandokando ya barabara na kuserereka mpaka chumbani na kuuwa watu wawili waliokuwa wamelala.

  kikwete is no serious.
   
 12. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Huyu JK na watendaji wake hasa PM wote ni wa ajabu, ikiwa watamzuia J P Maghufuli kubomoa na wanataka barabara za flyover wanategemea zitajengwa vipi mijini bila kubomoa??????? Vitu vingine lazima uvitoe sadaka kupisha vitu vingine!!!! Kama ujenzi wa nyumba mpya lazima ubomoe ya zamani pamoja na kukata miti ingawa vyote ni muhumu. Maghufuli anafanya kazi yake yuko sahihi ni bora kumuacha ili nchi ipate maendeleo!!!!!!!! Kumzuia ni kudumaza maendeleo!!! Mwenye akili ataona ujinga unaofanywa na hao viongozi!!!
   
 13. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35


  Hapo kwenye red.

  Mimi sijajua kama mtu akivunja sheria inahitaji huruma! Vile vile sina hakika kwenye hili kuna haja ya kumwambia Magufuri awache kubomoa. Endapo watu walijenga bila utaratibu NYUMBA na vingine vibomolewe iwekwe miundombinu. Haya mambo ya kuwambia watu wasubiri wawe na utu ndo yalisababisha rais kuwambia wezi wa EPA warudishe hela ikiwezekana wasamehewe, kana kwamba mwizi anaweza kuiba na kukwepa mkono wa sheria. Endapo matatizo yako kwenye halmashauri za wilaya, basi hizo ndo zibanwe na wamiliki wa nyumba na kuwafidia wala si kumzuia Dr Maguifuri kufanya kazi yake
   
Loading...