Uchaguzi 2020 Kumkata Paul Makonda kwenye Kura za Maoni CCM, siyo maamuzi yenye akili

Bashite keshajichagulia wizara za kupewa endapo ataukosa unaibu spika 1-waziri wa Nchi ofisi ya Rais utawala bora 2- waziri wa mambo ya ndani 3-waziri wa Ulinzi hataki wizara isiyo na chombo cha Dola anataka awe juu ya vyombo vya dola, akikosa hizo wizara nyeti angalau apewe wizara zenye Ulaji kama wizara ya madini

Utalii, viwanda, ujenzi, kule wizara ya fedha anajua hawezi kupewa yupo mzee Mpango mpaka mwaka 2026 huko wizara ya michezo akipewa atapokea uteuzi tu lakini chaguo lake binafsi kwa mujibu wa mshauri na msiri wake Le mutuz ni hizo wizara.
 
Umeongea kimahaba Sana, Mtu akishatoa taarifa halafu akatia chumvi ikazidi inapoteza kabisa ladha hata ya habari yenyewe. Makonda Ni mtu anayefanya kazi kweli lakini matatizo yake Ni makubwa kuliko kazi anazozifanya.Kama humjui makonda Ni mbinafsi kuliko unavyoweza kufikiri, mtu ambaye anaweza kua tayari kupitisha bidhaa kinyemela kupitia cheo chake kidogo tu Cha RC akipewa wizara atafanya mangapi? Atuambie Mali alizozipata akiwa Rc tu tukimpa wizara itakuaje? Ni mtu hatari Sana Sana wakuogopwa hafai hata kwa kukopea sema ndio hivyo tu kipenzi Cha baba.

Unazifahamu mali zake Mkuu?
Au umesikia maneno ya kuambiwa?
 
Chama kikimpitisha hakuna mpinzani wa kumshinda Mkuu
20200719_220056.jpg

Ridhaa ya kuwa mbunge inatokana na kura. Kila la heri kwake Paul na wagombea wengine wote
 
Kama mtu anajipendekeza kwako kwa nini usimpendelee?
Mtu anatukanwa kwa kazi uliyompa kwa nini usimlinde?
Mtu ananidhamu ya kazi uliyompa bado usimbebe?
Labda Kama amekutuma, Ila Bashite Hana hizo sifa unazompa ....yote aliyoyafanya alifanya kwaajili ya tumbo lake . Magufuli Ni mzalendo naweza hata kubishana na mtu hadhari lakini kwa makonda nashangaa hata ujasiri unautoa wapi!
 
Wakifuata ushauri wako CCM watalipoteza jimbo la Kigamboni asubuhi kweupe.Makonda ni kijana mzuri lakini alikuwa bado anahitaji kujifunza kwanza

Makonda ajifunze lipi tena ikiwa kuna vijana wamechukua majimbo wakiwa chini ya miaka 25.
 
Sikubaliani na makonda katika mambo mengi nina admire ujasiri wake. Akiweza kuuchannel katika positive na kupunguza kiki, anaweza kuja kuwa kiongoz bora kwa taifa hapo mbeleni.
 
Unazifahamu mali zake Mkuu?
Au umesikia maneno ya kuambiwa?
Nilijua tu utawahi hapo, Mali Ni kweli anazo nyingi Sana hata yeye mwenyewe akiongea tu amekua akijitanabaisha ,na mbona husemi Mambo ya kupitisha fenicha bila Kodi? Yupo na makando kando mengi kuliko kazi alizofanya!
 
KUMKATA MAKONDA SI MAAMUZI YENYE AKILI

Na, Robert Heriel

Ikiwa CCM itaamua kumkata Mhe. Paul Makonda itakuwa imefanya maamuzi yasiyo na busara. Yatakuwa ni maamuzi yasiyo na akili. Makonda ni moja vijana wachache muhimu kwa zama hizi katika taifa hili. Taifa la Tanzania linahitaji vijana mia moja mfano wa Makonda ambao watakuwa nchi nzima kwa ajili ya kuleta mabadiliko ndani ya nchi hii.

Ni muhimu Makonda akipitishwa na CCM katika nafasi ya ubunge kisha baadaye apewe nafasi ya uwaziri katika wizara zinazowahusu vijana, burudani na michezo.

Kwa nini Makonda ni kete muhimu kwa siasa za sasa hapa nchini?
Hoja zifuatazi zitahusika;

1. UJASIRI
Makonda ni kijana jasiri asiye mwoga. Ni moja ya vijana wachache hapa nchini ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika uongozi, Makonda matukio aliyojiingiza yanambeba licha ya kuwa hajafanikiwa sana lakini angalau tuliona nia yake. Kuna mambo kuyafuatilia lazima uwe na roho ya kikulungwa, roho ya simba. Kufuatilia Wauza Madawa ya kulevya ni moja ya mambo ambayo ni magumu sio hapa nchini hata duniani kwa ujumla.

Makonda ni jasiri kwani haogopi kusimamia kile anachokiamini. Watu waoga huwa hawana Msimamo. Kilichomwangusha Makonda ni mipaka ya mamlaka katika kazi yake.

2. MWANAJAMII
Makonda ni moja ya viongozi wasiojifungia ndani. Huchangamana na jamii. Sio wale viongozi ambao wakipewa nafasi hujifungia ndani muda wote maofisini, kumuona tuu utahangaika mpaka ukate tamaa. Hii ni tofauti na Makonda, yeye anapatikana muda wowote, ukifika ofisini kwake hakuna milolongo ya ajabu ajabu. Makonda ni kawaida kumuona kwenye matukio ya kijamii mathalani matamasha ya vijana ya burudani na michezo, matukio ya misiba, n.k. Hii ni tofauti na viongozi wengine. Kiongozi lazima achangamane na jamii.

3. USTAHIMILIVU
Kama kuna vijana wavumilivu kwenye hili taifa ni pamoja na Makonda. Moja ya vijana walioonja joto la jiwe awamu hii mitandaoni na kwenye vyombo vya habari ni pamoja na Makonda. Licha ya kashfa kibao kama vile Kufoji vyeti, ambapo mahasimu wake walidai alicharaza mswaki kidato cha nne kwa majina yake halisi Daudi Albert Bashite. Hilo akalivumilia, kashfa za kuwa anatabia za kishoga, nalo akavumilia, kashfa za kuwa hana uwezo wa kuzaa mtoto, yote alistahimili.

Pengine aliniudhi siku moja aliyolia kanisani, ile siku alijishushia credit. Mwanaume kulia lia mbele za watu sio jambo jema hasa wanaume shupavu. Hata hivyo halimuondolei sifa zingine lakini namuasa, siku nyingine asilie lie mbele za watu. Mwanaume kulia lia ni dalili ya udhaifu.

4. DHAMIRI YA DHATI YA KUISAIDIA JAMII
Makonda ni moja ya viongozi waliojipambanua katika kuisaidia jamii yake hasa kwenye Mkoa aliopewa auongoze. Makonda amesaidia vikundi vingi vya kina mama na vijana. Makonda ameonyesha nia za kuwasaidia watoto na kinamama waliotelekezwa na waume zao. Makonda ameonyesha nia ya kuwasaidia wale walioonewa kisheria kwa kuwawekea wanasheria, Makonda kajitahidi kupunguza uchafu wa jiji la Dar es Salaam, Makonda kajitahidi kurejesha usalama jijini Dsm kwa kupunguza vikundi vya Panya Road, sijui watoto wa Mbwa n.k.

Makonda anaweza asionekane ni kijana bora labda kutokana na tabia yake ya kujitukuza, na kutoa maneno ya shombo ambayo kwa sehemu kubwa nafahamu analenga kujifariji na kuwaumiza adui zake. Kwa kawaida kisaikolojia watu wanaotoa maneno ya shombo huyatamka kama njia ya kujifariji na kuondoa sonona, na kuwaumiza adui zao.

Wapo wakuu wa Mikoa wengi lakini waliofanya kama makonda hawafiki kumi. Hii ni dalili kuwa Makonda anafaa kupewa nafasi zaidi ya ukuu wa Mkoa.

5. MSAADA MKUBWA KWA MAGUFULI
Kama kuna watu waliomsaidia Mhe. Magufuli katika uongozi wake basi ni pamoja na Makonda. Imekuwa ngumu kumtenganisha Magufuli na Makonda katika siasa za awamu ya tano. Makonda amekuwa moja ya wabadilisha upepo katika masuala yanayotokea hapa nchini. Kwa namna hii amekuwa msaada mkubwa katika siasa za awamu hii. Makonda haoni shida kusemwa yeye kwa kupoteza mada fulani iliyokuwa inavuma ikiisakama serikali.

Pengine Makonda asiwe na ushauri wa maana kwa Magufuli lakini kiukweli anamchango mkubwa katika kubadili upepo wa mambo yanayovuma hapa nchini. Hili pekee linatosha kwa Magufuli kumkubali Makonda. Kumzima Makonda kwa wakati huu sio uamuzi wa akili. Nyota yake inang'aa lazima itumiwe kwa maslahi ya nchi.

6. KAFANIKIWA KULETA UTISHO
Makonda ni moja ya viongozi wachache waliofanikiwa kuleta utisho kwa watu wengi hapa nchini. Watu wa kawaida na viongozi wengi wanamuogopa Makonda. Kujenga hofu ni moja ya mambo ya muhimu katika utawala. Hofu hufanya utekelezaji uende kwa haraka. Makonda kwa cheo alichokuwa nacho cha ukuu wa Mkoa hakilingani na hofu aliyoijenga ndani ya jamii yake. Wengi humheshimu kupita cheo alichonacho.

7. BINGWA WA UHAMASISHAJI NA UCHANGISHAJI
Kiongozi sharti awe amebobea katika kuhamasisha watu. Makonda anajua kuhamasisha watu. Makonda anauwezo wa kuwachangisha matajiri, Akawaweka pamoja wafanyabiashara, wasanii na watu maarufu. Makonda anauwezo wa kuhamasisha vyombo vya habari vizungumzie jambo fulani. Tumeona mara kadhaa Makonda akikodisha kumbi za gharama kwa ajili ya tukio fulani mpaka wengine wanasema huyu Makonda anatoa pesa wapi. Makonda ni mhamasishaji na mchangishaji kwa wale atakaowaona wadau wa maendeleo.

Matajiri watachanga iwe kwa kumuogopa au kwa upendo. Hiyo haitamhusu Makonda ilimradi lengo limefikiwa.

Viongozi wengine katika hili walishindwa kabisa.

Magufuli anahitaji vijana kama hawa, watu kama Makonda, Tundu Lisu, Jokate, Anthony Mtaka, Prof jay, Ally Hapi, GJ Malisa, Ole Mushi, Ole Sebaya, Sugu, Profesa Mkandara, Ummy Mwalimu, Joyce Ndalichako, Suleiman Jafo, Bashe, Kassim Majaliwa, Bashiru, Ester Bulaya, miongoni mwa viongozi wengine wenye sifa.

Nafahamu kila mmoja ana mapungufu lakini kwenye mizani; ubora uzidi mapungufu.

Makonda apewe nafasi kwani ni mtu anayejirekebisha kila uchwao, sio mtu wa kutoa boko tena kama zamani alipokuwa mgeni wa kazi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300.
Wakala wa makonda unaongea nin
 
Sikubaliani na makonda katika mambo mengi nina admire ujasiri wake. Akiweza kuuchannel katika positive na kupunguza kiki, anaweza kuja kuwa kiongoz bora kwa taifa hapo mbeleni.
Sio kwa makonda, labda tuko na macho tofauti ya kutizama Hawa viongozi. Makonda sio mtu muadilifu hata kidogo na ukikosa uadilifu huna sifa ya kua kiongozi labda wa family yako.
 
Labda Kama amekutuma, Ila Bashite Hana hizo sifa unazompa ....yote aliyoyafanya alifanya kwaajili ya tumbo lake . Magufuli Ni mzalendo naweza hata kubishana na mtu hadhari lakini kwa makonda nashangaa hata ujasiri unautoa wapi!

Mimi nimeeleza kwa uchache walau aliyoyafanya, kama hayo hayatoshi kuitwa mzalendo, basi nieleze ni yapi yamfaayo mtu kuyafanya ili aitwe mzalendo kwa nafasi kama ya ukuu wa Mkoa?

Ndio maana nikasema kwa hapa Tz, wakuu wa mikoa waliofanya vizuri Makonda yupo Top 3. kisiasa anashikilia nafasi ya kwanza
 
KUMKATA MAKONDA SI MAAMUZI YENYE AKILI

Na, Robert Heriel

Ikiwa CCM itaamua kumkata Mhe. Paul Makonda itakuwa imefanya maamuzi yasiyo na busara. Yatakuwa ni maamuzi yasiyo na akili. Makonda ni moja vijana wachache muhimu kwa zama hizi katika taifa hili. Taifa la Tanzania linahitaji vijana mia moja mfano wa Makonda ambao watakuwa nchi nzima kwa ajili ya kuleta mabadiliko ndani ya nchi hii.

Ni muhimu Makonda akipitishwa na CCM katika nafasi ya ubunge kisha baadaye apewe nafasi ya uwaziri katika wizara zinazowahusu vijana, burudani na michezo.

Kwa nini Makonda ni kete muhimu kwa siasa za sasa hapa nchini?
Hoja zifuatazi zitahusika;

1. UJASIRI
Makonda ni kijana jasiri asiye mwoga. Ni moja ya vijana wachache hapa nchini ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika uongozi, Makonda matukio aliyojiingiza yanambeba licha ya kuwa hajafanikiwa sana lakini angalau tuliona nia yake. Kuna mambo kuyafuatilia lazima uwe na roho ya kikulungwa, roho ya simba. Kufuatilia Wauza Madawa ya kulevya ni moja ya mambo ambayo ni magumu sio hapa nchini hata duniani kwa ujumla.

Makonda ni jasiri kwani haogopi kusimamia kile anachokiamini. Watu waoga huwa hawana Msimamo. Kilichomwangusha Makonda ni mipaka ya mamlaka katika kazi yake.

2. MWANAJAMII
Makonda ni moja ya viongozi wasiojifungia ndani. Huchangamana na jamii. Sio wale viongozi ambao wakipewa nafasi hujifungia ndani muda wote maofisini, kumuona tuu utahangaika mpaka ukate tamaa. Hii ni tofauti na Makonda, yeye anapatikana muda wowote, ukifika ofisini kwake hakuna milolongo ya ajabu ajabu. Makonda ni kawaida kumuona kwenye matukio ya kijamii mathalani matamasha ya vijana ya burudani na michezo, matukio ya misiba, n.k. Hii ni tofauti na viongozi wengine. Kiongozi lazima achangamane na jamii.

3. USTAHIMILIVU
Kama kuna vijana wavumilivu kwenye hili taifa ni pamoja na Makonda. Moja ya vijana walioonja joto la jiwe awamu hii mitandaoni na kwenye vyombo vya habari ni pamoja na Makonda. Licha ya kashfa kibao kama vile Kufoji vyeti, ambapo mahasimu wake walidai alicharaza mswaki kidato cha nne kwa majina yake halisi Daudi Albert Bashite. Hilo akalivumilia, kashfa za kuwa anatabia za kishoga, nalo akavumilia, kashfa za kuwa hana uwezo wa kuzaa mtoto, yote alistahimili.

Pengine aliniudhi siku moja aliyolia kanisani, ile siku alijishushia credit. Mwanaume kulia lia mbele za watu sio jambo jema hasa wanaume shupavu. Hata hivyo halimuondolei sifa zingine lakini namuasa, siku nyingine asilie lie mbele za watu. Mwanaume kulia lia ni dalili ya udhaifu.

4. DHAMIRI YA DHATI YA KUISAIDIA JAMII

Makonda ni moja ya viongozi waliojipambanua katika kuisaidia jamii yake hasa kwenye Mkoa aliopewa auongoze. Makonda amesaidia vikundi vingi vya kina mama na vijana. Makonda ameonyesha nia za kuwasaidia watoto na kinamama waliotelekezwa na waume zao. Makonda ameonyesha nia ya kuwasaidia wale walioonewa kisheria kwa kuwawekea wanasheria, Makonda kajitahidi kupunguza uchafu wa jiji la Dar es Salaam, Makonda kajitahidi kurejesha usalama jijini Dsm kwa kupunguza vikundi vya Panya Road, sijui watoto wa Mbwa n.k.

Makonda anaweza asionekane ni kijana bora labda kutokana na tabia yake ya kujitukuza, na kutoa maneno ya shombo ambayo kwa sehemu kubwa nafahamu analenga kujifariji na kuwaumiza adui zake. Kwa kawaida kisaikolojia watu wanaotoa maneno ya shombo huyatamka kama njia ya kujifariji na kuondoa sonona, na kuwaumiza adui zao.

Wapo wakuu wa Mikoa wengi lakini waliofanya kama makonda hawafiki kumi. Hii ni dalili kuwa Makonda anafaa kupewa nafasi zaidi ya ukuu wa Mkoa.

5. MSAADA MKUBWA KWA MAGUFULI

Kama kuna watu waliomsaidia Mhe. Magufuli katika uongozi wake basi ni pamoja na Makonda. Imekuwa ngumu kumtenganisha Magufuli na Makonda katika siasa za awamu ya tano. Makonda amekuwa moja ya wabadilisha upepo katika masuala yanayotokea hapa nchini. Kwa namna hii amekuwa msaada mkubwa katika siasa za awamu hii. Makonda haoni shida kusemwa yeye kwa kupoteza mada fulani iliyokuwa inavuma ikiisakama serikali.

Pengine Makonda asiwe na ushauri wa maana kwa Magufuli lakini kiukweli anamchango mkubwa katika kubadili upepo wa mambo yanayovuma hapa nchini. Hili pekee linatosha kwa Magufuli kumkubali Makonda. Kumzima Makonda kwa wakati huu sio uamuzi wa akili. Nyota yake inang'aa lazima itumiwe kwa maslahi ya nchi.

6. KAFANIKIWA KULETA UTISHO

Makonda ni moja ya viongozi wachache waliofanikiwa kuleta utisho kwa watu wengi hapa nchini. Watu wa kawaida na viongozi wengi wanamuogopa Makonda. Kujenga hofu ni moja ya mambo ya muhimu katika utawala. Hofu hufanya utekelezaji uende kwa haraka. Makonda kwa cheo alichokuwa nacho cha ukuu wa Mkoa hakilingani na hofu aliyoijenga ndani ya jamii yake. Wengi humheshimu kupita cheo alichonacho.

7. BINGWA WA UHAMASISHAJI NA UCHANGISHAJI

Kiongozi sharti awe amebobea katika kuhamasisha watu. Makonda anajua kuhamasisha watu. Makonda anauwezo wa kuwachangisha matajiri, Akawaweka pamoja wafanyabiashara, wasanii na watu maarufu. Makonda anauwezo wa kuhamasisha vyombo vya habari vizungumzie jambo fulani. Tumeona mara kadhaa Makonda akikodisha kumbi za gharama kwa ajili ya tukio fulani mpaka wengine wanasema huyu Makonda anatoa pesa wapi. Makonda ni mhamasishaji na mchangishaji kwa wale atakaowaona wadau wa maendeleo.

Matajiri watachanga iwe kwa kumuogopa au kwa upendo. Hiyo haitamhusu Makonda ilimradi lengo limefikiwa.

Viongozi wengine katika hili walishindwa kabisa.

Magufuli anahitaji vijana kama hawa, watu kama Makonda, Tundu Lisu, Jokate, Anthony Mtaka, Prof jay, Ally Hapi, GJ Malisa, Ole Mushi, Ole Sebaya, Sugu, Profesa Mkandara, Ummy Mwalimu, Joyce Ndalichako, Suleiman Jafo, Bashe, Kassim Majaliwa, Bashiru, Ester Bulaya, miongoni mwa viongozi wengine wenye sifa.

Nafahamu kila mmoja ana mapungufu lakini kwenye mizani; ubora uzidi mapungufu.

Makonda apewe nafasi kwani ni mtu anayejirekebisha kila uchwao, sio mtu wa kutoa boko tena kama zamani alipokuwa mgeni wa kazi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300.
Unamaanisha chama la wana lisifate taratibu zake za kupata mgombea na apewe konda boy?
 
hakuna mwenye uwezo wa kumkata Makonda huko CCM, sio tu Makonda hata Mnyeti pia hakuna mwenye uwezo wa kumkata..

Makonda ndie mgombea ubunge jimbo la Kigamboni hilo halina ubishi na hayupo wakumkata..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom