Kuminya uhuru wa mawazo ni kuminya ubunifu. Tusahau nchi ya Viwanda

ntemintale

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
952
1,871
Ubunifu huwa ni zao la uhuru wa mawazo. Ukibana uhuru wa mawazo umeua ubunifu. Na bila ubunifu tusahau kufikia nchi ya viwanda.

Cc: Wahusika wanajifahamu. Kama hawajifahamu wamuulize Mugabe.
 
Matajiri wataishi kama shetani! Hivyo viwanda vitajengwa na masikini? Hakuna cha viwanda labda visasi.
 
Wenye akili timamu ndiyo wanaona uhusiano wa maendeleo na uhuru wa mawazo au maoni ya watu.

JK tulimshutumu sana kuwa dhaifu na rushwa kwenye utawala wake. Lakini alikuwa vyema kwenye freedom ya press na watu.

Hakuna maendeleo bila ubunifu. Hakuna ubunifu bila freedom ya watu na press!
The choice is ours.
 
La

Labda mnataka mbinywe magolori yenu tu. Kungekuwa na kubinywa kwa uhuru wa mawazo mngekuwa mnajimwaga hivi humu JF? Tatizo la nyumbu wakikaririshwa kwamba sehemu ya kuvukia mto ni moja basi wote wataishia kutumbukia na kuliwa na mamba. Ziko forums na platforms nyingi za innovations hasa kwa vijana kuweza kutoa na kubadilishana mawazo yao juu ya teknolojia na matumizi yake katika kukabili changamoto za jamii zetu. Kama kuna kubinywa kwa uhuru mbona maxmalipo wanaendelea? Nyinyi mnakaririshwa kuviringisha mikono na kuhamasishwa kuuza figo badala ya nyumbu wenzenu wakubwa kuwaonesha njia za namna ya ku confront challenges za maisha yenu na mnafuata tu kama mazuzu vile. Hakuna uhuru usio na mipaka hata huko kunakosemekana demokrasia ndio ilizaliwa.
'Malaika' Wa kufunga mitandao kashindwa kazi, vinginevyi jf ingeshafungwa. Uhuru zaidi bila kuhafifisha uwajibikaji unatakiwa!
 
Matajiri wataishi kama shetani! Hivyo viwanda vitajengwa na masikini? Hakuna cha viwanda labda visasi.
Hakika, kama mkakati ni kuwafanya matajiri waliosota ili kutajirika na wakapata raha, waishi kama mashetani, Wa kujenga viwanda watatokea Jupiter au Mars!
 
La

Labda mnataka mbinywe magolori yenu tu. Kungekuwa na kubinywa kwa uhuru wa mawazo mngekuwa mnajimwaga hivi humu JF? Tatizo la nyumbu wakikaririshwa kwamba sehemu ya kuvukia mto ni moja basi wote wataishia kutumbukia na kuliwa na mamba. Ziko forums na platforms nyingi za innovations hasa kwa vijana kuweza kutoa na kubadilishana mawazo yao juu ya teknolojia na matumizi yake katika kukabili changamoto za jamii zetu. Kama kuna kubinywa kwa uhuru mbona maxmalipo wanaendelea? Nyinyi mnakaririshwa kuviringisha mikono na kuhamasishwa kuuza figo badala ya nyumbu wenzenu wakubwa kuwaonesha njia za namna ya ku confront challenges za maisha yenu na mnafuata tu kama mazuzu vile. Hakuna uhuru usio na mipaka hata huko kunakosemekana demokrasia ndio ilizaliwa.
Humu tunatumia fake ids. Kwa maana hiyo hatuko huru kutoa maoni hadharani.
 
Wenye akili timamu ndiyo wanaona uhusiano wa maendeleo na uhuru wa mawazo au maoni ya watu.
JK tulimshutumu sana kuwa dhaifu na rushwa kwenye utawala wake. Lakini alikuwa vyema kwenye freedom ya press na watu.
Hakuna maendeleo bila ubunifu. Hakuna ubunifu bila freedom ya watu na press!
The choice is ours.
Hata Mugabe alijiona think tank, lakini leo hii kawekwa chini ya Ulinzi. Sera zake za umimi na kujiona anajua kila kitu zimeharibu uchumi.
 
Tunaenda Zimbabwe na ccm.
Mungu wasaidie watanzania.

Watanzania daini katiba mpya ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana.
 
Back
Top Bottom