Kumiliki Shahada ya kupigia kura ambayo si yako, SI KOSA - Polisi.

dedam

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
845
165
Polisi wamesema ukikutwa na shahada za kupigia kura hata mia moja sio kosa. Je sheria za uchaguzi zinasemaje
 
Na mishangao inaendelea!
Polisi wilayani Igunga imesema si kosa kwa mtu mmoja kumiliki shahada ya kupigia kura ya mtu mwingine.

Akiongea kupitia TBC1 Afisa mmoja wa Polisi wilayani humo (jina halikuwekwa hewani) alisema kuwa wamewaachia wanachama wa CCM ambao walikamatwa wakiwa wanaorodhesha majina ya wananchi wa kijiji fulani pamoja na kadi zao za kupigia kura, huku Mwenyekiti wa kijiji hicho akikutwa na shahada ambayo/ambazo si zake.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, amedai kuwa wameamua kuwaachia watu hao kwani hilo si kosa, na kwamba Mwenyekiti huyo wa kijiji alikutwa na kadi ya mjomba wake hivyo si kosa.

My take:
Vyombo vya dola na serikali vinazidi kukumbatia chama tawala hata pale ukweli unapokuwa dhahiri shahiri. Vipi kama makosa ya aina hiyo wanapokutwa nayo wapinzani?
 
Wana JF jana nimeangalia vyombo vya habari Star Tv ITV na hata ile TBC ya mshana, amenukuliwa Kamanda Mngulu yule wa Igunga akisema kuwa kitendo cha viongozi wale wa CCM walikutwa na shahada za kupigia kura za watu wengine pamoja na kuandikisha majina si kosa kisheri,mimi sina uelewa mpana kisheria nisaidieni wana jamvi, sheria hasa zile za uchaguzi zinasemaje katika mazingira hayo?
binafsi niliona kama si kosa basi kuna hatari shahada zikanunuliwa kama njugu na watu kunyimwa haki yao ya kupiga kura, na kama ni kosa kisheria kuna umuhimu wa kamanda huyo kutakiwa kufuta kauli yake kwani inachochoea uchakachuaji wa uchaguzi.
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom