Kumiliki Gari ya usafiri binafsi

Dereva Suka

Senior Member
Sep 25, 2014
176
289
Habari zenu wakuu

Kumiliki gari Tanzania inabidi ujipange na uwe una biashara inayokuingizia pesa ya uhakika au mshahara mnono but kama unajua haupo vizuri sana basi tarajia kukutana na mambo haya.
1. Motor vehicle itaisha muda wake then hela ya kulipia utajikuta hauna sababu ya majukumu...Police hawatakuacha.

2. Insurance au bima itaisha nayo utatakiwa kuilipia...kama hujalipia utakutana na sheria na 30000 itakuhusu.

3. Over speeding kidogo tu utakamatwa na hela utatoa

4. Unatakiwa uwe na vifaa vya usalama vyote kuanzia triangles, fire extinguisher kama huna notification inakuhusu.

5. Gharama za parking mjini hasa hapa Dar

6. Gharama za mafuta....kwa gari ya kawaida kabisa ndogo kwa siku mafuta ya 10000 kwa ajili ya mzunguko lazima yakuhusu..kwa mwez inagonga kama 300000 hiv.

7. Bado gari hujaipeleka service, hujanunua oil, matairi hujabadili mara umepata pancha au kifaa cha gari kimeharibika au umegonga na unatakiwa ulipe ukatengeneze na show yako ya mbele.

8. Gari inahitaji kuoshwa..gharama za chin kabisa kuosha ni 5000...jiulize kwa mwezi gari unaosha mara ngapi.

9.ukizubaa ukapaki vibaya utaibiwa power window na taa itabidi ukanunue...mfano tu taa moja ya nyuma ya Toyota Progress ni 250000. Kwa kifupi..kumiliki gar inabidi uwe upo vizuri kweli....ukiona mtu anamiliki gari bongo halafu limekamilika kila kitu...tairi kaweka rim sport, gari safi, vibali vyote vipo up to date na kila siku ana drive jua huyo ana pesa..usiniulize kazitolea wapi ila jua tu yupo vizuri.
 
Habari zenu wakuu

Kumiliki gari Tanzania inabidi ujipange na uwe una biashara inayokuingizia pesa ya uhakika au mshahara mnono but kama unajua haupo vizuri sana basi tarajia kukutana na mambo haya....
Hahahahaha umeeleweka mkuu.
Heshima kwa wenye magari na ndio maana hata mabinti unachagua tu kama upo duka la nguo
 
Habari zenu wakuu

Kumiliki gari Tanzania inabidi ujipange na uwe una biashara inayokuingizia pesa ya uhakika au mshahara mnono but kama unajua haupo vizuri sana basi tarajia kukutana na mambo haya...
Nimecheka sana hy statment yako ya mwishon...et usiniulize hela katoa wap
 
Habari zenu wakuu

Kumiliki gari Tanzania inabidi ujipange na uwe una biashara inayokuingizia pesa ya uhakika au mshahara mnono but kama unajua haupo vizuri sana basi tarajia kukutana na mambo haya...
Wakati wako wa kumiliki Gari bado. Tulia
 
Back
Top Bottom