Kumetokea nini Mwanza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumetokea nini Mwanza?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Plato, Sep 13, 2010.

 1. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Wakuu nimesikia habari kwamba jana kulikuwa na vurugu mwz, eti kidogo mabomu yapigwe na dr.slaa ndiye ameepusha ghasia.magazeti hayafunguki humu na jf sioni chochote.nijuzeni tafadhali wenye hizo habari.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  tupeni data tafadhari..
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  I too have heard it in Newspapers summary this morning!, but for sure i hav'nt got any detailed substance of the commotion!..Bt we got lots of pals from Mwanza, do the needful plz!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wananchi wa Mwanza pale Milongo (karibu na Community Center)... ni uwanja wa shule ya Msingi.. Dr.Slaa alipomaliza kuhutubia walitaka walisukume gari lake.. lakini Polisi hawakutaka hilo na mji wa mwanza ulikuwa umesimama kwa muda... ndipo nusura itokee vurugu lakini Polisi waliweza kumudu kuidhibiti.
   
 5. p

  pierre JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kawmba wadau waliofika kumsikiliza dr.slaa waliamua kutumia nguvu zao kwa kusukuma gari alilokuwa amepanda dr.slaa kama mchango wao wa mafuta.Polisi kuona hivyo ndio wakawa wanatishia kuwapiga mabomu,ndipo dr. alipotumia busara zake kuwanyamazisha polisi.
   
 6. b

  bobishimkali Member

  #6
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moja ya kazi ya polisi katika kipindi hiki cha kampeni ni kulinda usalama wa wagombea akiwemo DR SLAA ili wasiweze kudhurika na jambo lolote.Hivyo kitendo kilichofanywa na polisi cha kuwazuia watu kusukuma gari la SLAA,mimi nakiunga mkono kwa asimia100,kwa sababu ni vigumu kujua kama watu wote wanaotaka kusukuma gari la mgombea fulani wana nia njema naye. JE?KAMA SLAA ANGEDHURIKA KUTOKANA NA WATU KUSUKUMA GARI LAKE NA POLISI HAWAKUCHUKUA HATUA YEYOTE YA KUWAZUIA,NANI ANGELAUMIWA KAMA SIYO POLISI. Polisi walitekeleza wajibu wao ipasavyo na ndivyo wanavyopaswa kufanya ili kulinda usalama wa viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea siku ya uchaguzi 31 oktoba 2010
   
 7. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Soma Mwananchi kaka Wameeleza vizuriii...!
   
 8. MasterMind

  MasterMind Senior Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema wapata msukosuko Mwanza

  Monday, 13 September 2010 08:20
  Boniface Meena, Ilemela

  UMATI wa wafuasi wa Chadema uliokuwa ukisukuma gari la mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Dk Willibrod Slaa nusura wapigwe mabomu ya machozi, lakini katibu huyo mkuu wa chama hicho akafanikiwa kutuliza askari waliotaka kuvuruga hali ya hewa.Wafuasi hao wa Chadema walikuwa wamekaidi amri ya polisi ya kuwataka waachane na kitendo hicho cha kulisukuma gari la mgombea huyo wa uraiskutoka uwanja wa Shule ya Msingi ya Mirongo hadi katikati ya jiji la Mwanza.

  Uamuzi huo wa kulisukuma gari lililombeba Dk Slaa ulisababisha barabara alizokuwa akipitia kwenda katikati ya jiji kupitika kwa shida ama kusababisha zisipitike kabisa, kiasi cha polisi kuamua kutaka kutumia nguvu za ziada kuwatawanya.

  Kabla ya polisi kuchukua hatua hiyo, Dk Slaa aliibuka na kuwakemea akiowataka wasitumie nguvu kubwa kutuliza shauku ya wananchi.

  Akizugumza jana kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Igombe wilayani Ilemela, Dk Slaa alilaani kitendo cha polisi kutaka kutumia mabomu ya machozi kuutawanya umati wa wananchi uliokuwa ukisukuma gari lake.
  Alisema kitendo cha polisi kutaka kuwarushia wananchi mabomu ya machovu hakikubaliki na kingevuruga uchaguzi na kuonekana kuwa si huru.

  "alichotakiwa kufanya (kamanda wa polisi wa wilaya) OCD ni kuwapanga askari wake ili waangalie wananchi wasipate madhara na msafara uende kwa amani... lakini alishindwa kudhibiti na ninalaani kitendo hicho cha kutaka kutumia mabomu ya machozi," alisema Slaa.

  Alisema kuwa OCD wa Nyamagana hakutimiza wajibu wake na kushangaa kwamba Jeshi la Polisi liliahidi kutopendelea upande wowote wakati wa uchaguzi, lakini anaona hali tofauti na na akamtaka OCD wa Ilemela amfikishie ujumbe huo OCD mwenzake.

  "Mfikishie ujumbe huo mwenzako na sisi tutaufikisha kwa wakubwa zenu," alisema Dk Slaa.
  Dk Slaa, ambaye alikuwa mbunge wa jimbo la Karatu kwa takriban miaka 15 na sasa ameamua kugombea urais, alisema ni muhimu kwa wananchi kufanya mabadiliko kwa kuiweka Chadema madarakani.  Source: Mwananchi
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Slaa aepusha shari wananchi na polisi

  Na Restuta James

  13th September 2010


  [​IMG]
  Busara zake zawabadili Polisi nia
  [​IMG]
  Washuhudia gari yake ikisukumwa


  [​IMG]
  Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Willibroad Slaa


  Busara ya mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Willibroad Slaa, juzi iliepusha shari mjini Mwanza, baada ya kuwataka polisi waliokuwa wamejiweka tayari kumwaga maji ya kuwasha na mabomu ya machozi dhidi ya wananchi, kuacha kufanya hivyo.

  Dk. Slaa alifikia hatua hiyo mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Nyamagana ambako umati wa wananchi ulijitokeza na kuvamia gari lake na kuanza kulisukuma huku wakimshangilia.

  Kutokana na hali ya wananchi kuzingira gari lake na polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa wamejiweka tayari kuwatawanya wananchi hao, Dk. Slaa alishuka kwenye gari lake na kuwataka polisi kutimiza wajibu wao wa kulinda amani na si kuwafurumushia wananchi mabomu ya machozi.

  Pengine juzi linaweza kuonekana kuwa ni tukio la kwanza kwa askari polisi kutafakari kabla ya kutenda, kwani pamoja na kwamba walionekana kukereka kwa gari la Dk. Slaa kusukumwa, walibadili nia na badala yake waliamua kuendelea kuimarisha ulinzi huku gari la Dk. Slaa likisukumwa hadi hotelini kwake.

  Kutokana na wananchi kuhamasika huko, askari polisi waliongoza msafara huo kwa mbele huku wakiimarisha usalama pembeni na nyuma, na shughuli ya Chadema ilimalizika kwa amani bila virungu wala mabomu kutembea.

  “Sitaki polisi mtupendelee, lakini sitaki muibebe CCM, nimesikitishwa askari walipotaka kuwapiga wananchi waliokuwa wakinishangilia, OCD (Mkuu wa polisi wa wilaya) wa Nyamagana hakuwa anafanya kazi yake kwa makini,” alisema.

  Aliongeza: “Kitendo hicho hakikubaliki kamwe, ujumbe huu tutaupeleka kwa viongozi wa juu, mkianza leo sijui baadaye kwenye kura itakuwaje, hatutaki Tanzania tumwage damu.”

  Dk. Slaa alisema polisi wanalipwa mishahara kwa kodi za Watanzania, hivyo si vema kulipiza kwa kile alichokiita kuwa ni zawadi ya mabomu ya machozi. Naye mgombea ubunge katika jimbo la Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda, amemtaka mgombea urais kupitia CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuachana na harakati za kuwania nafasi hiyo na badala yake ampigie kura Dk. Slaa.

  Shibuda aliyekuwa mbunge kupitia CCM kati ya 2005 hadi 2010, alisema Rais Kikwete anapaswa kutumia nafasi yake ya uenyekiti wa CCM, kupambana na ufisadi ndani ya chama hicho badala ya kung’ang’ania urais.

  Shibuda alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Ilemela, uliohutubiwa na Dk. Slaa. Alisema amekuwa ndani ya CCM kwa miaka 43 (Tanu na baadaye CCM), hivyo anafahamu uchafu uliopo na namna chama hicho kinavyoshiriki kupora rasilimali za taifa.
  “Ndugu yangu Kikwete, kama kweli unamwogopa Mungu, basi mpigie kura Dk. Slaa ili awe Rais wa Tanzania …ikiwa unamuenzi Mwalimu Nyerere, achia ngazi, ukapambane na ufisadi ndani ya CCM,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.

  Shibuda ambaye amekuwa akizungumza kwa misemo na nahau za kuchekesha, aliifananisha CCM na chui aliyejivika ngozi ya kondoo.

  “CCM ni chui aliyevaa ngozi ya kondoo, anaingia zizini na kurarua ng’ombe na kondoo, kimekuwa chama cha mafisadi kwa kunadi yale ambayo hakitekelezi,” alisema.

  Baada ya Shibuda kuzungumza, Dk. Slaa aliwataka wananchi kumchagua na kuwapigia kura wabunge wa Chadema katika jimbo la Nyamagana, Wenje Ezekia na Highness Samson (Ilemela).  CHANZO: NIPASHE
   
 10. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nidhani ni vyema vyama vya upinzani wajitahidi mno kuwa japo na mpiga picha na mwandishi wa mgombea urais ambao watakuwa wakisambaza taarifa na picha kwa kutumia blog, tovuti na hata email za vyombo vya habari mbalimbali maana habari zao na picha halisi ya mikutano yao huwa zinafichwa na kuminywa na mfumo CCM. Matokeo yake ni maswali kama haya kwa wanaotaka kupata ukweli.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,870
  Trophy Points: 280
  Nadhani JK amepata huu ujumbe kutoka mwanza aliopewa na shibuda, ni ujumbe mzito sana na kama anaweza kusoma alama za nyakati itakuwa makini,JK sio wa kurudi tena Ikulu,kama akiridi huyu jamaa atakuwa mkali manake itakuwa lala salama yake na hatojali mtu. We fikiria tu first half yake imekuwa mabaya sana na isiyoridhisha na usanii mwingi sana kupita kiasi. Sasa je tukimpa tena lala salama si ndio kabisa kila kitu atahamishia chalinze kabisa. Na wapewa kofia na mat shirt watabakia kulalamika hadi kusaga meno.
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Lile linalotumia kodi zetu kujiendesha hamna kitu

  HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania
   
 13. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  paka jimmy uppooo!!
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Polisi wajue fika my PAYEE ndo inawaweka mjini hivyo busara ndo iwe inatumika badala ya Jazba.
  Huree Dr Slaa kwa kuwapa live hawa polisi wetu.
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160


  Just out of curiosity, hivyo kwenye mikutano ya CCM hili gari la upupu linakuwa deployed au linaletwa tu kwenye mikutano ya wapinzani?
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bila shaka umeyaona matangazo ya kuhamasisha wananchi kuchangia vyama vya upinzani. Moja ya shughuli zinazohitaji michango ya wananchi wenye mapenzi na wenye kutaka kujua na kuona picha za nini upinzani inafanya ni habari na picha unazozizungumzia. Changia ili uweze kupata unachotaka!
   
Loading...