Madimba jr
JF-Expert Member
- Aug 12, 2017
- 1,577
- 3,143
we jamaa nawe hueleweki siku hizi umekua POPO sanaWanabodi, kila nipatapo fursa, huwa nawaletea zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo huwa zinachapishwa katika gazeti la Habari Leo, kila siku za Jumatano.
Ili kuepuka kuitwa popote na kuhojiwa kuwa nimesema kitu fulani, yaani statements, makala hizi huja kwa mtindo wa maswali, yaani questions nikihoji, Jumatano ya leo, nazungumzia hiki tkinachoendelea huku Tanzania Bara, katika utoaji wa update ya ugonjwa wa Corona.
Declaration of Interest
Unapoibua hoja nzito za kitaifa kama hii yenye maslahi kwa taifa, wakati taifa lako liko vitani, na limeisha tangaza vita, kama hoja hiyo itakwenda kinyume cha status quo, unaweza kuonekana ni msaliti wa vita hii, hivyo ni muhimu ku decrare interest kuwa huu sio usaliti, bali ndiko kulisaidia taifa lako. Naomba kusisitiza mimi Paskali wa JF, naunga mkono msimamo wa rais Magufuli wa kutofanya lockdown na kuzuia Watanzania tusitishane kuhusu haka ka ugonjwa Kalona, ni ka ugonjwa kadogo, ila inapofikia hali ya kutisha kwa watu kufa, kwa Corona, the situation now bado sio ile ile ya Ka Corona, sio kaugonjwa ni janga, na sio tena tusitishane, bali tuambiane ukweli kuwa Corona ni ugonjwa hatari, unatisha!, na watu wanakufa kwa rate ya kutisha!.
Je kuna uwezekano sisi hapa nchini kwetu Tanzania, tumetangaziwa Hali ya Hatari kimya kimya bila Watanzania kutangaziwa rasmi?. Nimeuliza hivi kufuatia kutokuwepo kwa update yoyote ya hali ya ugonjwa wa Corona upande wa Tanzania bara, tangu baada ya Rais Magufuli kulihutubia Taifa akitokea Ikulu ya Chato!
Hiki kinachoendelea cha kutokutolewa kwa update yoyote, kingeweza kufanyika tuu endapo taifa liko kwenye hali ya hatari ambayo inao utaratibu wake kuitangaza, na haiwezi kutangazwa kimya kimya, tena kwa sababu janga hili ni la taifa zima, hali ya hatari haiwezi kutangazwa upande mmoja tuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku upande wa bara tuu pekee yake!, huu utoaji taarifa za Corona unaoendelea huku Tanzania Bara, wa kutotoa update yoyote tangu last Friday ni kinyume cha Sheria ya Haki ya Kupata Habari, The Right to Information, kupitia sheria hiyo, Watanzania tuna haki ya kupata habari sahihi na za kweli kuhusu hali ya maambukizi ya Corona, wangapi wameambukizwa, wangapi wamepona, wangapi wamekufa, wangapi bado wako quarantine, wangapi walikuwa quarantine na wamemaliza.
Mpaka ninapoandika hapa, kwa Tanzania idadi ya waliokufa kwa Corona tangu janga hili lilipoanza kwa mujibu wa taarifa rasmi ni watu 10 tuu!. Kwa sasa tunaishi kwenye the age of information world, tuko kwenye dunia ya utandawazi, information zina flows from every corner, watu tunaona kila kitu, hadi video za mazishi ya usiku usiku, miili inetelekezwa mabarani for days!, watu wanawapoteza wapendwa wao na kutoruhusiwa kuwazika, tangu hiyo Ijumaa tuu mpaka jana, kuna visa zaidi ya 10 vimeripotiwa kwenye media tena wengine ni vigogo wakubwa kabisa, haiwezekani hadi leo Jumatano m, idadi ni ile ile ya vifo 10 toka Alhamisi iliyopita!
This is not right, kama Tanzania tuna sheria ya haki ya kupata habari, haiwezekani serikali yetu ikaendelea kukalia habari kama hizi katika mazingira kama haya, no matter how bad the situation is, Watanzania tuambiwe ukweli hata kama unauma vipi, ndio ukweli wa hali halisi ni haki yetu kujua na kuambiwa ukweli na serikali yetu.
Kwanza naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kutokana na bandiko la mwana jf huyu
Hivi kwanini wananchi tunanyimwa taarifa ya maambukizi mapya na ya wale wanaokufa kwa ugonjwa wa COVID-19? - JamiiForums na hapa ninaomba kunakili sehemu tuu ya bandiko hilo
Mkuu Mystery, naunga mkono hoja, enzi za zamani, mambo ya kutoa habari kwa upande wa serikali ilikuwa iko huru kutoa habari au kutotoa, ikijisikia kutoa habari, inatoa, ikijisikia kutotoa habari, haitoi na hakuna yoyote mwenye mamlaka ya kuiuliza.
Kupata Habari ni Haki sio Favour
Lakini kuanzia mwaka 2016, Tanzania tumepitisha sheria ya haki ya kupata habari, the right to information act, ambapo sasa kupata habari ni haki, sio favors, serikali inawajibika kutoa habari za kweli kwa wananchi, hiki kinachoendelea sasa kwenye utoaji wa habari za maendeleo ya ugonjwa wa Corona, ni kinyume cha sheria. Watanzania wana haki ya kupata habari, unless rais atangaze hali ya hatari, sheria zote na haki zote zinasimama!.
Kipengele cha Haki ya kupata habari ni hiki
View attachment 1434164
Lakini pamoja na haki hii, sheria hii pia inaipa serikali mamlala ya kuzuia habari andapo sarikali itakuwa na sababu za kuzuia habari fulani isitoke,
View attachment 1434165
kigezo pekee cha serikali kuzuia habari fulani isitoke ni endapo habari hizo zitakuwa na madhara kwa public interest, jee habari za vifo. vya Corona vina madhara kwa public interest?, jee jamii ya Watanzania wakiijua idadi kamili ya watu wanaokufa daily kwa Corona, tunapanic?. Mbona nchi za wenzetu wamekuwa wakitangaza daily na kuna nchi watu walikuwa wanakufa zaidi ya 1000 per day na wanatangaza, sisi tunaogopa nini?!.
Corona ni Janga Kweli, Jee Rais Atangaze Hali ya Hatari?.
Mamlaka ya rais kutangaza hali ya hatari ni haya
View attachment 1434166
Kwa hali ya Janga la Corona lilipofika, rais Magufuli anazo sababu zote za kweli na za kihali za kutangaza hali ya hatari kwa kutumia sababu hizi zilizoainishwa kwenye Katiba
View attachment 1434167
Kwa mujibu wa katiba yetu, rais Magufuli hawezi yeye tuu kuamua kujitangazia tuu hali ya hatari, tangazo la rais kutangaza hali ya hatari lazima liridhiwe na Bunge na kupigiwa kura ya ndio na theluthi mbili za wabunge wote wa Bunge la JMT,
View attachment 1434168
Sasa kwa vile hakuna kitu chochote kama hiki kimefanyika kwa Tanzania, hii withholding updates za Corona, inafanyika kwa sheria gani na mamlaka gani?
Leo Waziri Ummie Atatangaza Update.
Kuna kitu kinaniambia kuwa leo Waziri wa Afya, atatoa update, namuomba wazi Ummy wakati akitoa hiyo update ya leo, pia awe mkweli na muwazi kuhusu idadi halisi ya vifo vya Corona bila kusahau kuifafanua hii sintofahamu iliyotokea hapa katikati ya sababu ya kigugumizi cha ukmya wa siku 5 bila eny update.
Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali
Je kuna uwezekano sisi hapa nchini kwetu Tanzania, kuna Hali ya Hatari ya kisiri siri imetangazwa kimya kimya bila Watanzania kutangaziwa rasmi, hivyo huu ukimya wa kutotangaza update ya Corona ni utekelezaji tuu?, vinginevyo hiki kinachoendelea kwenye kutotoa update ya Corona ni kinyume cha sheria ya haki ya kupata habari.
Nawatakia Jumatano njema
Paskali.