Kumetangazwa hali ya hatari kimya kimya? Huu utoaji taarifa za Corona ni kinyume cha Sheria. Watanzania tuna Haki ya kupata habari za kweli

BREAKING NEWS
Wametangazwa wagonjwa wengine 196

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, ametangaza muda mfupi uliopita na hivyo kufanya idadi ya jumla ya wagonjwa wa COVID 19, kuwa 480, kwa nchi nzima, Bara na Visiwani
 
Shupaza shingo
Mkuu Paskali, pamoja na kukubali kuwa tuna haki ya kupata habari, hili la kulazimisha kupewa habari kuhusu mwenendo wa COVID-19 sikubaliani na wewe.

Sikubaliani na wewe kwa sababu ya mazingira ya maisha yetu na tabia zetu. Kuna ukweli ulio wazi kuwa wengi wetu WaTz tunaishi kwa mazoea tu, hatujali, tunadharau, tunakejeli, tunadhuhaki, na mienendo ya aina hiyo.

Pamoja na ushauri wa kitaalamu kuhusu kinga watu bado hawajali Nitatoa mifano kadhaa:
1) Watu hawavai barakoa inavyotakiwa, hata viongozi. Tunaona kwenye TV viongozi wakiongea na jamii au wanahabari ama hawakuvaa au barokoa imeteremshwa kwenye kidevu na wengine wabaishikashika kuiweka sawa usoni, du!
2) Vijana wanaonekana ndio hawajali kabisa kwani bado wanakusanyika kwenye sherehe, baa nk. Wakiambukizana huko ni dhahiri wakirudi nyumbani watawaambukiza wanafamilia.
3) Bado kuna misongamano ya watu kwenye sehemu za biashara km masoko na vyombo vya usafiri.

Pamoja na mapungufu hayo na mengine yaliyoainishwa na members humu JF, naamini hali ya maambukizi na vifo kutokana na COVID-19 yamethibitiwa. Ushahidi wa uklhakija unaweza kupatikana kutoka kwa kila mwanaJF humu iwapo atatoa ushuhuda kama ana mgonjwa/marehemu ambaye ni ndugu, jirani, mtaani, kazini, nk. ambaye amethibitishwa ni kutokana COVID-19. Vinginevyo ni uzushi mtupu wa kuichafua Serikali kwa sababu wanazozijua.

Mkuu Paskali, unailaumu Serikali kuwa inaficha ukweli unapodai watu wanawapoteza wapendwa wao na kutoruhusiwa kuwazika, tangu hiyo Ijumaa tuu mpaka jana, kuna visa zaidi ya 10 vimeripotiwa kwenye media tena wengine ni vigogo wakubwa kabisa, haiwezekani hadi leo Jumatano m, idadi ni ile ile ya vifo 10 toka Alhamisi iliyopita!?

Mkuu Paskali, mwanahabari nguri, nilitegemea ungetuhakikishia ukweli wa taarifa hizo, kwa jinsi ya taaluma yako. Labda nawe sasa unataka kuiaminisha jamii kuwa hapakuwa na vifo kabla ya COVID-19, au vipi, kiasi cha kuilaumu Serikali!

Naamini, Serikali iliyoko madarakani, pamoja na kuwa sikivu, ni makini, inawapenda na kuwajali watu wake. Ushahidi ni jinsi inavyotumia vizuri pesa ya walipa kodi, misaada na mikopo kwa ajili ya maendeleo na kuboresha huduma za jamii, ambapo matokea yake ni kuondoa umaskini.

Kwa pamoja tutavuka salama salimini tishio la COVID-19 kwa kila mtu kuzingatia ushauri.

JILINDE UMLINDE JIRANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi, kila nipatapo fursa, huwa nawaletea zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo huwa zinachapishwa katika gazeti la Habari Leo, kila siku za Jumatano.

Ili kuepuka kuitwa popote na kuhojiwa kuwa nimesema kitu fulani, yaani statements, makala hizi huja kwa mtindo wa maswali, yaani questions nikihoji, Jumatano ya leo, nazungumzia hiki tkinachoendelea huku Tanzania Bara, katika utoaji wa update ya ugonjwa wa Corona.

Declaration of Interest
Unapoibua hoja nzito za kitaifa kama hii yenye maslahi kwa taifa, wakati taifa lako liko vitani, na limeisha tangaza vita, kama hoja hiyo itakwenda kinyume cha status quo, unaweza kuonekana ni msaliti wa vita hii, hivyo ni muhimu ku decrare interest kuwa huu sio usaliti, bali ndiko kulisaidia taifa lako. Naomba kusisitiza mimi Paskali wa JF, naunga mkono msimamo wa rais Magufuli wa kutofanya lockdown na kuzuia Watanzania tusitishane kuhusu haka ka ugonjwa Kalona, ni ka ugonjwa kadogo, ila inapofikia hali ya kutisha kwa watu kufa, kwa Corona, the situation now bado sio ile ile ya Ka Corona, sio kaugonjwa ni janga, na sio tena tusitishane, bali tuambiane ukweli kuwa Corona ni ugonjwa hatari, unatisha!, na watu wanakufa kwa rate ya kutisha!.

Je kuna uwezekano sisi hapa nchini kwetu Tanzania, tumetangaziwa Hali ya Hatari kimya kimya bila Watanzania kutangaziwa rasmi?. Nimeuliza hivi kufuatia kutokuwepo kwa update yoyote ya hali ya ugonjwa wa Corona upande wa Tanzania bara, tangu baada ya Rais Magufuli kulihutubia Taifa akitokea Ikulu ya Chato!

Hiki kinachoendelea cha kutokutolewa kwa update yoyote, kingeweza kufanyika tuu endapo taifa liko kwenye hali ya hatari ambayo inao utaratibu wake kuitangaza, na haiwezi kutangazwa kimya kimya, tena kwa sababu janga hili ni la taifa zima, hali ya hatari haiwezi kutangazwa upande mmoja tuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku upande wa bara tuu pekee yake!, huu utoaji taarifa za Corona unaoendelea huku Tanzania Bara, wa kutotoa update yoyote tangu last Friday ni kinyume cha Sheria ya Haki ya Kupata Habari, The Right to Information, kupitia sheria hiyo, Watanzania tuna haki ya kupata habari sahihi na za kweli kuhusu hali ya maambukizi ya Corona, wangapi wameambukizwa, wangapi wamepona, wangapi wamekufa, wangapi bado wako quarantine, wangapi walikuwa quarantine na wamemaliza.

Mpaka ninapoandika hapa, kwa Tanzania idadi ya waliokufa kwa Corona tangu janga hili lilipoanza kwa mujibu wa taarifa rasmi ni watu 10 tuu!. Kwa sasa tunaishi kwenye the age of information world, tuko kwenye dunia ya utandawazi, information zina flows from every corner, watu tunaona kila kitu, hadi video za mazishi ya usiku usiku, miili inetelekezwa mabarani for days!, watu wanawapoteza wapendwa wao na kutoruhusiwa kuwazika, tangu hiyo Ijumaa tuu mpaka jana, kuna visa zaidi ya 10 vimeripotiwa kwenye media tena wengine ni vigogo wakubwa kabisa, haiwezekani hadi leo Jumatano m, idadi ni ile ile ya vifo 10 toka Alhamisi iliyopita!

This is not right, kama Tanzania tuna sheria ya haki ya kupata habari, haiwezekani serikali yetu ikaendelea kukalia habari kama hizi katika mazingira kama haya, no matter how bad the situation is, Watanzania tuambiwe ukweli hata kama unauma vipi, ndio ukweli wa hali halisi ni haki yetu kujua na kuambiwa ukweli na serikali yetu.

Kwanza naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kutokana na bandiko la mwana jf huyu
Hivi kwanini wananchi tunanyimwa taarifa ya maambukizi mapya na ya wale wanaokufa kwa ugonjwa wa COVID-19? - JamiiForums na hapa ninaomba kunakili sehemu tuu ya bandiko hilo
Mkuu Mystery, naunga mkono hoja, enzi za zamani, mambo ya kutoa habari kwa upande wa serikali ilikuwa iko huru kutoa habari au kutotoa, ikijisikia kutoa habari, inatoa, ikijisikia kutotoa habari, haitoi na hakuna yoyote mwenye mamlaka ya kuiuliza.

Kupata Habari ni Haki sio Favour
Lakini kuanzia mwaka 2016, Tanzania tumepitisha sheria ya haki ya kupata habari, the right to information act, ambapo sasa kupata habari ni haki, sio favors, serikali inawajibika kutoa habari za kweli kwa wananchi, hiki kinachoendelea sasa kwenye utoaji wa habari za maendeleo ya ugonjwa wa Corona, ni kinyume cha sheria. Watanzania wana haki ya kupata habari, unless rais atangaze hali ya hatari, sheria zote na haki zote zinasimama!.
Kipengele cha Haki ya kupata habari ni hiki
View attachment 1434164
Lakini pamoja na haki hii, sheria hii pia inaipa serikali mamlala ya kuzuia habari andapo sarikali itakuwa na sababu za kuzuia habari fulani isitoke,
View attachment 1434165
kigezo pekee cha serikali kuzuia habari fulani isitoke ni endapo habari hizo zitakuwa na madhara kwa public interest, jee habari za vifo. vya Corona vina madhara kwa public interest?, jee jamii ya Watanzania wakiijua idadi kamili ya watu wanaokufa daily kwa Corona, tunapanic?. Mbona nchi za wenzetu wamekuwa wakitangaza daily na kuna nchi watu walikuwa wanakufa zaidi ya 1000 per day na wanatangaza, sisi tunaogopa nini?!.

Corona ni Janga Kweli, Jee Rais Atangaze Hali ya Hatari?.
Mamlaka ya rais kutangaza hali ya hatari ni haya
View attachment 1434166
Kwa hali ya Janga la Corona lilipofika, rais Magufuli anazo sababu zote za kweli na za kihali za kutangaza hali ya hatari kwa kutumia sababu hizi zilizoainishwa kwenye Katiba
View attachment 1434167
Kwa mujibu wa katiba yetu, rais Magufuli hawezi yeye tuu kuamua kujitangazia tuu hali ya hatari, tangazo la rais kutangaza hali ya hatari lazima liridhiwe na Bunge na kupigiwa kura ya ndio na theluthi mbili za wabunge wote wa Bunge la JMT,
View attachment 1434168

Sasa kwa vile hakuna kitu chochote kama hiki kimefanyika kwa Tanzania, hii withholding updates za Corona, inafanyika kwa sheria gani na mamlaka gani?

Leo Waziri Ummie Atatangaza Update.
Kuna kitu kinaniambia kuwa leo Waziri wa Afya, atatoa update, namuomba wazi Ummy wakati akitoa hiyo update ya leo, pia awe mkweli na muwazi kuhusu idadi halisi ya vifo vya Corona bila kusahau kuifafanua hii sintofahamu iliyotokea hapa katikati ya sababu ya kigugumizi cha ukmya wa siku 5 bila eny update.

Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali
Je kuna uwezekano sisi hapa nchini kwetu Tanzania, kuna Hali ya Hatari ya kisiri siri imetangazwa kimya kimya bila Watanzania kutangaziwa rasmi, hivyo huu ukimya wa kutotangaza update ya Corona ni utekelezaji tuu?, vinginevyo hiki kinachoendelea kwenye kutotoa update ya Corona ni kinyume cha sheria ya haki ya kupata habari.

Nawatakia Jumatano njema
Paskali.
Serikali imelifanyia kazi ombi la Mwigulu Nchemba la kutotangaza maambukizi na vifo vya corona. Heko Nchemba, kwa hekima zako. Kwenye baraza la mawaziri umesharejeshwa hivyo kwa kuihekimisha serikali!!!!!!! Anza kusherehekea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona ndege zilizonunuliwa tuliambiwa idadi yake?? Inshindikanaje kwenye coron na tutaipamaje serikali utendaji wake kama haitoi taarifa sahihi?
Kutofautiana kimawazo sio vibaya ili mradi mawazo yote yasiwe tu ya kubomoa kwa sababu ktk kutofautiana huko ndiko kujenga nyumba iliyobora

Mimi, sikubaliani kabisa na kutangaza idadi ya wagonjwa, idadi ya vifo n.k

Ila naomba Serikali ijidhatiti katika mambo ambayo yatakuwa sababu ya kupunguza maambukizi, kama kutoa Matangazo na kuelimisha wananchi hatua za kufanya ili kuepuka maambukizi mapya, najua Matangazo yapo Ila kutiliwe mkazo zaidi

Pili, Serikari iendelee kupima watu tena Kwa Kasi zaidi na wagonjwa wanaopatikana wapelekwa karantini na huduma zote wapate

Serikari ijielekeze kuboresha na kuhakikisha vifaa tiba vipi na vinakidhi

Serikali ikae na wataamu wake, hasa Madactari ili wajadiri changamoto zote zinavyowakabiri Wakunga hawa na serikali kutatua changamoto hizo Kwa haraka iwezekanavyo

Wananchi nao, wamekuwa ni sehemu ya kusababisha janga hili kuwa kubwa pasipo sababu za msingi, Watu wote wenye Dalili za maambukizi waijitokeze hadharani kupima ili na wao wasiwe sababu ya kuwaambukiza wengine, kila familia zichukue hatua zote zinazoelekezwa na wizara husika

Nakataa kutangaza vifo, au maambukizi mapya Kwa sababu, haiwezi kubadiri Kasi yake ya maambukizi na vifo Kutokea zaidi Sana inaleta hofu zaidi Kwa wananchi wenyewe

Na bahatu mbaya kwamba, hakuna Sheria either ya kimataifa au ya Tanzania inayodai kwamba ni lazima kutangaza vifo na maambukiz Pindi vinapotokea

Tusipozingatia kufuata maelekezo ya wataalamu hasa kutoka kwenye familia zetu, Corona haina utani Ati, inafanya kweli

MUNGU Ponya Taifa letu Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kusema tangia last friday hatujapata taarifa yoyote ile ya janga Hili la korona. The last update ya Friday imebaki ile ile, idadi ya cases,wailopona na waliokufa ni ile ile. Sasa tunapodai ninhski yetu kupata taarifa manake kisaikolojia unajustify kwamba case zipo Lkn hazitangazwi.

Tusilazimishe ukweli uwe uwongo. Nimeona watu wameshaanza kuilalamikia serikali kuhusu kukosekana kwa Taarifa ya ugonjwa wa corona. Watanzania wenzangu tunatakiwa tuelewe kuwa hamna tamko lolote la serikali kwamba limesitisha kutoa takwimu za wagonjwa wa corana. Ila tunachotakiwa kuamini Ni kwamba cases zitakapoongezeka tutapewa taarifa. Kwahiyo tuendelee kutunza kumbukumbu ya takwimu tulizokuwa nazo za Mara ya mwisho.

Kwahiyo tunatakiwa kuamini kuwa kutotangazwa cases mpya za wagojwa wa korona Ni Neema kwetu wa Tanzania kwamb mapambano ya kudhibiti ueneaji upo vizuri

Mwisho Ilishatangazwa kuwa sio kila anayekufa au kuumwa siku hizi Ni corona. Makala Kama hizi brother paskal ndio zinazotengeneza taharuki na hata pengine wahudumu wetu wa afya kuanza kuwakimbia wagonjwa hata wengine ambao sio wagojwa wa korona. Tunatakiwa kuimini serikali ndio yenye mamlaka ya kutupa taarifa lkn kuendelea kuchukua Tahadhari.

Hata km hujapata taarifa ya cases za corona unatakiwa kutambua kuwa janga Hili lipo na tunachotakiwa ninkuchukua Tahadhari na sio kuanza kutafuta taarifa za kujiridhisha Hali upoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi, kila nipatapo fursa, huwa nawaletea zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo huwa zinachapishwa katika gazeti la Habari Leo, kila siku za Jumatano.

Ili kuepuka kuitwa popote na kuhojiwa kuwa nimesema kitu fulani, yaani statements, makala hizi huja kwa mtindo wa maswali, yaani questions nikihoji, Jumatano ya leo, nazungumzia hiki tkinachoendelea huku Tanzania Bara, katika utoaji wa update ya ugonjwa wa Corona.

Declaration of Interest
Unapoibua hoja nzito za kitaifa kama hii yenye maslahi kwa taifa, wakati taifa lako liko vitani, na limeisha tangaza vita, kama hoja hiyo itakwenda kinyume cha status quo, unaweza kuonekana ni msaliti wa vita hii, hivyo ni muhimu ku decrare interest kuwa huu sio usaliti, bali ndiko kulisaidia taifa lako. Naomba kusisitiza mimi Paskali wa JF, naunga mkono msimamo wa rais Magufuli wa kutofanya lockdown na kuzuia Watanzania tusitishane kuhusu haka ka ugonjwa Kalona, ni ka ugonjwa kadogo, ila inapofikia hali ya kutisha kwa watu kufa, kwa Corona, the situation now bado sio ile ile ya Ka Corona, sio kaugonjwa ni janga, na sio tena tusitishane, bali tuambiane ukweli kuwa Corona ni ugonjwa hatari, unatisha!, na watu wanakufa kwa rate ya kutisha!.

Je kuna uwezekano sisi hapa nchini kwetu Tanzania, tumetangaziwa Hali ya Hatari kimya kimya bila Watanzania kutangaziwa rasmi?. Nimeuliza hivi kufuatia kutokuwepo kwa update yoyote ya hali ya ugonjwa wa Corona upande wa Tanzania bara, tangu baada ya Rais Magufuli kulihutubia Taifa akitokea Ikulu ya Chato!

Hiki kinachoendelea cha kutokutolewa kwa update yoyote, kingeweza kufanyika tuu endapo taifa liko kwenye hali ya hatari ambayo inao utaratibu wake kuitangaza, na haiwezi kutangazwa kimya kimya, tena kwa sababu janga hili ni la taifa zima, hali ya hatari haiwezi kutangazwa upande mmoja tuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku upande wa bara tuu pekee yake!, huu utoaji taarifa za Corona unaoendelea huku Tanzania Bara, wa kutotoa update yoyote tangu last Friday ni kinyume cha Sheria ya Haki ya Kupata Habari, The Right to Information, kupitia sheria hiyo, Watanzania tuna haki ya kupata habari sahihi na za kweli kuhusu hali ya maambukizi ya Corona, wangapi wameambukizwa, wangapi wamepona, wangapi wamekufa, wangapi bado wako quarantine, wangapi walikuwa quarantine na wamemaliza.

Mpaka ninapoandika hapa, kwa Tanzania idadi ya waliokufa kwa Corona tangu janga hili lilipoanza kwa mujibu wa taarifa rasmi ni watu 10 tuu!. Kwa sasa tunaishi kwenye the age of information world, tuko kwenye dunia ya utandawazi, information zina flows from every corner, watu tunaona kila kitu, hadi video za mazishi ya usiku usiku, miili inetelekezwa mabarani for days!, watu wanawapoteza wapendwa wao na kutoruhusiwa kuwazika, tangu hiyo Ijumaa tuu mpaka jana, kuna visa zaidi ya 10 vimeripotiwa kwenye media tena wengine ni vigogo wakubwa kabisa, haiwezekani hadi leo Jumatano m, idadi ni ile ile ya vifo 10 toka Alhamisi iliyopita!

This is not right, kama Tanzania tuna sheria ya haki ya kupata habari, haiwezekani serikali yetu ikaendelea kukalia habari kama hizi katika mazingira kama haya, no matter how bad the situation is, Watanzania tuambiwe ukweli hata kama unauma vipi, ndio ukweli wa hali halisi ni haki yetu kujua na kuambiwa ukweli na serikali yetu.

Kwanza naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kutokana na bandiko la mwana jf huyu
Hivi kwanini wananchi tunanyimwa taarifa ya maambukizi mapya na ya wale wanaokufa kwa ugonjwa wa COVID-19? - JamiiForums na hapa ninaomba kunakili sehemu tuu ya bandiko hilo
Mkuu Mystery, naunga mkono hoja, enzi za zamani, mambo ya kutoa habari kwa upande wa serikali ilikuwa iko huru kutoa habari au kutotoa, ikijisikia kutoa habari, inatoa, ikijisikia kutotoa habari, haitoi na hakuna yoyote mwenye mamlaka ya kuiuliza.

Kupata Habari ni Haki sio Favour
Lakini kuanzia mwaka 2016, Tanzania tumepitisha sheria ya haki ya kupata habari, the right to information act, ambapo sasa kupata habari ni haki, sio favors, serikali inawajibika kutoa habari za kweli kwa wananchi, hiki kinachoendelea sasa kwenye utoaji wa habari za maendeleo ya ugonjwa wa Corona, ni kinyume cha sheria. Watanzania wana haki ya kupata habari, unless rais atangaze hali ya hatari, sheria zote na haki zote zinasimama!.
Kipengele cha Haki ya kupata habari ni hiki
View attachment 1434164
Lakini pamoja na haki hii, sheria hii pia inaipa serikali mamlala ya kuzuia habari andapo sarikali itakuwa na sababu za kuzuia habari fulani isitoke,
View attachment 1434165
kigezo pekee cha serikali kuzuia habari fulani isitoke ni endapo habari hizo zitakuwa na madhara kwa public interest, jee habari za vifo. vya Corona vina madhara kwa public interest?, jee jamii ya Watanzania wakiijua idadi kamili ya watu wanaokufa daily kwa Corona, tunapanic?. Mbona nchi za wenzetu wamekuwa wakitangaza daily na kuna nchi watu walikuwa wanakufa zaidi ya 1000 per day na wanatangaza, sisi tunaogopa nini?!.

Corona ni Janga Kweli, Jee Rais Atangaze Hali ya Hatari?.
Mamlaka ya rais kutangaza hali ya hatari ni haya
View attachment 1434166
Kwa hali ya Janga la Corona lilipofika, rais Magufuli anazo sababu zote za kweli na za kihali za kutangaza hali ya hatari kwa kutumia sababu hizi zilizoainishwa kwenye Katiba
View attachment 1434167
Kwa mujibu wa katiba yetu, rais Magufuli hawezi yeye tuu kuamua kujitangazia tuu hali ya hatari, tangazo la rais kutangaza hali ya hatari lazima liridhiwe na Bunge na kupigiwa kura ya ndio na theluthi mbili za wabunge wote wa Bunge la JMT,
View attachment 1434168

Sasa kwa vile hakuna kitu chochote kama hiki kimefanyika kwa Tanzania, hii withholding updates za Corona, inafanyika kwa sheria gani na mamlaka gani?

Leo Waziri Ummie Atatangaza Update.
Kuna kitu kinaniambia kuwa leo Waziri wa Afya, atatoa update, namuomba wazi Ummy wakati akitoa hiyo update ya leo, pia awe mkweli na muwazi kuhusu idadi halisi ya vifo vya Corona bila kusahau kuifafanua hii sintofahamu iliyotokea hapa katikati ya sababu ya kigugumizi cha ukmya wa siku 5 bila eny update.

Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali
Je kuna uwezekano sisi hapa nchini kwetu Tanzania, kuna Hali ya Hatari ya kisiri siri imetangazwa kimya kimya bila Watanzania kutangaziwa rasmi, hivyo huu ukimya wa kutotangaza update ya Corona ni utekelezaji tuu?, vinginevyo hiki kinachoendelea kwenye kutotoa update ya Corona ni kinyume cha sheria ya haki ya kupata habari.

Nawatakia Jumatano njema
Paskali.
uzi wako umemuibua MAJALIWA, kaleta taarifa yake ila ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAO.
 
Huogopi kusikia vifo ila hutaki kufa wewe, hebu ufe basi tukutangaze... watu wanajifukiza unataka afe nani.?
Kama nilivyosema hapo mwanzo. Ni kuwa takwimu zinatoka na taarifa zote. Maambukizi yamefika 480, waliopona 167, walikufa wameongezeka na kufikia 17.

Maambukizi sio kifo. Bado kuna possibility ya kupona.
Sasa ww hup uwoga wako hautokusaidia lolote. In the end ukweli utajulikana tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
73 Reactions
Reply
Back
Top Bottom