KUMEKUCHA: Washereheshaji(MCs) na Wapiga picha kuanza kutozwa kodi

BUNGENI: Wabunge wataka Washehereshaji(MCs) na Wapiga picha waanze kutozwa kodi ili Serikali iweze kukusanya mapato ya kutosha.

Wakati huo huo, Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Allan Kiula amesema maeneo mapya ambayo yanaweza kuanzishiwa kodi kuwa ni pamoja na Ushauri Elekezi (Consultancy Agencies) sambamba na kuimarishwa kwa ukusanyaji wa kodi ya zuio ya asilimia 10 kutoka kwa wamiliki na wapangaji wa nyumba na makazi.

Duniani kote nchi zilizo endelea kila kitu kinatozwa kodi.
Harusi,Mc,Music, tena Washereheshaji na Kila Aina za starehe kodi yake ni kubwa kuliko vitu gingine
 
BUNGENI: Wabunge wataka Washehereshaji(MCs) na Wapiga picha waanze kutozwa kodi ili Serikali iweze kukusanya mapato ya kutosha.

Wakati huo huo, Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Allan Kiula amesema maeneo mapya ambayo yanaweza kuanzishiwa kodi kuwa ni pamoja na Ushauri Elekezi (Consultancy Agencies) sambamba na kuimarishwa kwa ukusanyaji wa kodi ya zuio ya asilimia 10 kutoka kwa wamiliki na wapangaji wa nyumba na makazi.
ni wapuuzi kweli hasa kwenye kujitangaza kwa bei wanazolipwa halafu kumbe hawalipi kodi. walitakiwa wawe wanapiga mpunga kimyakimya ili wasishitukiwe kuwa wanauza sanaa yao.
 
Watanzania wanapenda maendeleo lakini kUlipa kodo hawataki. Kila chanzo kinachobuniwa hawataki kulipa kodi. sasa kama mtu ndani ya siku moja tu anatengeneza malaki ya hela kwa kuwa MC tu wakati huo alifika ukumbini akitumia barabara, analindwa na vyombo vya usalama n.k. sasa kwanini asilipe kodi ili kuchangia ukarabati wa barabara, mishahara na vyombo vya ulinzi n.k? Sijui wanataka maendeleo yaje kwa miujiza!
 
Yeah.. This is too bad photographer kutozwa kodi,
Serikali imekuja mbio kwa spidi ya bolt bila hodi,
Hospitali nyingi zina feli hakuna kitu hakuna wodi,
Vijana wanalialia ajira hakuna somebody I told.

Freestyle rap.
 
Sasa kama hutaki watu walipe kodi hizo Hospitali zimapataje wodi? Watanzania wanapenda sana shushi. Wakisikia habari ya kodi povu linawatoka, wakati huo huo wanataka waletewe maendeleo. Popote duniani kodi ndo kila kitu. Hata hii misaada inayotoka huko Ulaya ni kodi za Wananchi wao. TULIPE KODI KWA MAENDELEO YETU.
 
Back
Top Bottom