Kumekucha: Wachina watinga Ludewa kuanza kazi ya madini

Mkuu ningekuomba tu unisome between the lines.. Nacho maanisha ni kwamba mradi huu una madhara makubwa sana sawa na bomu la nuklia kwetu.. Mafuriko yaliyotokea Dar nchi hizi ni sawa na bomba la maji jikoni..Simtishi mtu isipokuwa lazima tuweke tahadhali..

Mpango huu umepita jaitro akiwepo unachozungumza nini haswa... Rais na mawaziri wote mnaowaona wabovu ndio wamewezesha mradi huu kwa hiyo msitake kuwapa sifa watu wengine wakati wale wale wa 10% ndio wameweka saini..Hilo wala sii neno kwangu na wala halinitishi isipokuwa kikubwa zaidi kwangu ni UFISADI uliopo kwa mradi huu utagharimu maisha ya watu na mazingira kwa sababu kuchimba makaa ya mawe sio sawa na kuchimba Tanzanite wala dhahabu..

Inatakiwa makni ya hali ya juu sana maana hata Ulaya mwenyewe ipo miradi mingi yamakaa ya mawe imefungwa kutokana na madhara ya miradi hii...Hivyo kweli tunahitaji makaa ya mawe lakini Je, tumejiweka vema kukabiliana na madhara yake maanake hatuna tabia ya kudhibiti usalama wa wananchi..Meli zinazama hatuna mpango wa kuhakikisha haitokei tena, hiyo malaria tu tumebambikwa vyandarua na show za clouds..samahani Joe na Ruge wangu watanisamehe!

Jamani mnafanya mchezo na maisha ya watu nyie! sijui tumejiandaa vipi kuhakikisha madini yatokanayo na makaa ya mawe yanadhibitiwa vizuri na kuhakikisha vyanzo vya maji havipati madini hayo...Hao waajiriwa 8000 how long wataishi na Je, ikitokea maisha ya watu wa Ludewa wanakufa na maradhi yasiyojulikana hizo ajira zitalipa vipi?

Tumeshidnwa kuleta umeme wa dharura mega watts hazifiki hata 300 kwa mji mmoja tu for the past 6 years na bado tunahesabu siku na miaka, leo mnataka kunambia waamuzi wale wale wa mipango ile wataweza haya makubwa ?..

Tahadhari ni muhimu katika viwanda ambavyo ni heavy duty, hilo linaeleweka. Kwa vyo vyote vyombo vinavyohusika vinawajibika, na madhara yatokanayo na machimbao hayo, na madhara uliyosema hayawezi kututisha tusiendeshe miradi hiyo kwa maana kwamba jinsi unavyopaa juu zaidi ndivyo anguko litakavyokuwa kubwa zaidi. Matatizo ya tajiri ni makubwa zaidi kuliko ya maskini. Anayepata zaidi atadaiwa zaidi hata biblia imeainisha hilo.

Kinachotakiwa wakati ni ukuta na kwa sasa tunahitaji jambo hili lifanyike, na vyombo husika vitahakikisha mazingira ambayo ni bora kwa wahusika na mazingira hayo. Kama nchini Ujerumani jimbo la Essen ambalo kulikuwa na machimbo makubwa ya makaa ya mawe ambayo yalisaidia kuboresha uchumi wa ujerumani, kama wangeogopa uchumi wa ujerumani usingeboreka kama tunavyoona leo. Wale wajerumani wenye asili ya jimbo la Bavaria majitu ya miraba minne walihamia jimbo la Essen kwenye machimbo. Hata nchi zinazozalisha umeme wa nuklia kama marekani bado wangali na baadhi ya mitambo ya vinu vya kuzalisha umeme vinavyoendeshwa kwa makaa ya mawe ambayo ni gharama nafuu. Ndio maana West Virginia wangali na mahandaki makubwa ya machimbo ya makaa ya mawe yanayopakiwa kwenye mabehewa na kusambazwa kwenye vinu vya kufua umeme.

Matatizo ya umeme wa dharura si upatikanaji wa vinu tu, ila gharama ya uendeshaji ni kubwa mno, ndio maana hata vinu vilivyopo vinatupa taabu ya kuagiza malighafi ya uendeshaji toka nje. Afadhali kama tutazalisha umeme wa hapa hapa nyumbani wakati malighafi ni ya kutoka ndani ya mipaka ya nchi yetu. Hata serikali ikishindwa kulipa gharama zake, shares zake zinaweza kupunguza gharama ambazo serikali imejitwisha kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo kwa sasa.

Jambo moja muhimu katika kujadili Watanzania tuwe reliable, kuangalia pande zote advantage nadisadvantage. Wengi wetu wakishakaa upande wa kupinga hata kukiwa na hoja nzuri hazikubaliwi tunabaki kupinga kwa nguvu zote, kwa mwendo huu hakuna chema tunachoweza kuona, ila yote mabaya tu, hii ni kasoro na kwa mwendo huu hatuwezi kujenga nchi kwa kuona upande mbaya tu. Ni mtazamo wangu binafsi, ila inafaa to weigh both sides, lets balance isues isiwe kila kitu kupinga hakuna tunachokubaliana, haiwezekani kusiwe na faida ila hasara tu, na mwenye akili timamu hawezi kusimamia mkataba wenye hasara tu miaka yote na viongozi wote wawe wanaokubaliana na mikataba ya hasara tu.

Wawekezaji wenyewe hawawezi kuja kama mikataba ya hasara kwao. Kwa vyo vyote faida lazima ipo ndio maana wanakubali vinginevyo hatawakubali kuja. Lets be fair. Kwa pande zote mbili kwa vyo vyote kuna upande utakaonyongeka kidogo, wageni kwa vyo vyote watanufaika zaidi kwa kuwa tumewaomba, kama tunataka tupate yote tungefanya wenyewe, lakini hayo yametushinda, nini bora? Kubaki maskini au tuite wageni watunasue kwenye linda la umaskini? Kama tumewaita tukubali kugawana.
 
Hamna kitu hawa Wachina ni wanadharau sana wanachapa mpaka viboko wafanyakazi pili wanaleta mpaka mtu wa chini ambaye mtanzania wa kawaida anaweza kuifanya hiiyo kazi mfano grader operator,dumper nk,pili wanalipa mishahara midogo sana tena kwa unyanyasaji wanaongoza kampuni kama BARRICK au kusini kwa Waaustralia huwezi kulinganisha na Wachina sana sana huko Watz wanakimbila kidebe cha mafuta halafu Kwa Mchina hata security ya kazi hakuna cha HR yaani hata fundi mekanika anaweza kukufukuza kazi yaani hao hakuna kabisa hata safety ni ziro utasikia watu watakavyo kufa au kuathirika na mgodi na sijui sheria zetu zinatulinda vipi ukimuuliza huyo Filikunjombe sidhani kama anajua hilo asifurahie kuja kwa Wachina baadae watz wa Ludewa waje wamlilie

Tumezoea lelemama, nawatambua wachina nilivyosimuliwa na wazee wakati wanafanya kazi ya kujenga TAZARA ni kama ukoo wa wajerumani, wakiwa kazini ni kazi si longolongo.

Hata walioendelea wamefikia kiwango hicho kwa uchapaji kazi si longolgono za kibongo, maendeleo si maneno bali kujituma katika kazi. Wale wavivu wala wasiende kuomba kazi kwa wachina wataaibika.

Ulaya kama mtu hujitumi unafukuwa papo hapo na hakuna mafao ya kwenda kukimbilia kama bongo idara ya kazi, kwani idara ya kazi bongo inafuga wavivu na wazembe, ndio maana tunapiga mark time wakati wenzetu wanaendeleaz mbele.
 
DSCF5520.JPG


Tujifunza hawa wawekezaji Wachina wanavyobana matumizi kwa kutumia kausafiri ka kawaida tu tena basi moja ambalo linawachukua wao na vifaa vyao licha ya mabilioni wanayokuja kuwekeza.

Serikali ya Tanzania hapa licha ya msululu wa magari zaidi ya mia kungekuwa na helkopta zinazozunguka angani kusindikiza msafara. Sijui matumizi makubwa serikalini yataisa lini?
 
Back
Top Bottom