Kumekucha: Wachina watinga Ludewa kuanza kazi ya madini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
DSCF5504.JPG
DSCF5520.JPG
DSCF5509.JPG
DSCF5507.JPG

DSCF5515.JPG
DSCF5519.JPG

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwapokea wageni wake wa mradi wa mchuchuma na Liganga kutoka China ambao wamekuja kuanza kazi katika wilaya hiyo. Hii ni ndoto ya siku nyingi ya wakazi wa wilaya ya Ludewa na mbunge wao Deo Filikunjombe kutaka madini ya mchuchuma na Liganga kuanza kuchimbwa.
 
Hivi wamekuja kama experts au wawekezaji?
KUNA WATAALAMU wetu watakaokuwa wanawaback hao wachina na kujifunza maujuzi?...

TANZANIA NCHI YANGU NAKULILIA.
 
Watatafuta namna ya kuiba madini haya na kuyapeleka kwao. Nchi nyingine mwekezaji anaambiwa alete labda 5% tu ya Wataalamu na wengine wote wawe ni local experts lakini kwetu inakuwa ni vice versa si ajabu wakati mwingine hata 100% ya wataalamu ni wageni!!!! Angalia kule Barricks kwa wachimba dhahabu.
 
Mbunge ndio anawapokea nilidhani wangepokelewa na Mbunge pamoja na mtu wa wizara yenye dhamana ya nishati na madini ama mtu toka NDC! Yote kheri inanikumbusha makala moja niliyoisoma inayosema "From Brettonwoods to China".
 
Mkuu wachina ni jamaa zetu lakini linapofika suala la kuleta wataalam wao wanalet kila mtu hata muendesha grader. Sheria zipo lakini ndugu zetu wa idara ya kazi huwa wanafumba macho!
 
Kuendelea kufumba macho hakutusaidii maana pamoja na utajiri mkubwa tuliokuwa nao katika rasilimali mbali mbali wanaofaidika ni wageni na sisi tukibaki bila maendeleo ya kweli.
 
Madini tumekuwa nayo miaka yote na hawa wataalamu tunao miaka yote na wanafanya majaribio bila kufikia jawabu kwamba utafiti na majaribio yamekamilika. Ukitaka tuendelee na usanii huu wa wataalumu wetu tutaendelea kupiga marktime badala ya endeleaz mbele, wachina wakishaanza kazi hakuna mwendo pole, ni mwendo kasi baada ya kupata amri ya endeleaz mbele.
 
Mkuu nabadili kauli"huwa wanafumbwa macho"
 
Kuendelea kufumba macho hakutusaidii maana pamoja na utajiri mkubwa tuliokuwa nao katika rasilimali mbali mbali wanaofaidika ni wageni na sisi tukibaki bila maendeleo ya kweli.

Nakubaliana na hoja yako, lakini tatizo si wageni wanaoiba utajiri wetu ila viongozi wetu wabinafsi ndio wanaachia mwanya. Hata wewe ukipata nafasi ya kula hutaiachia.

Kama alivyosema Jaji Bomani juzi, ni muhimu kuweka sheria za kunda rasilimali ikiwa ni pamoja na process za awali zifanyike hapa nchini na processed product ndizo ziuzwe nje, hapo kutakuwa na mfumo mzuri wa kiuchumi.
 
Madini tumekuwa nayo miaka yote na hawa wataalamu tunao miaka yote na wanafanya majaribio bila kufikia jawabu kwamba utafiti na majaribio yamekamilika. Ukitaka tuendelee na usanii huu wa wataalumu wetu tutaendelea kupiga marktime badala ya endeleaz mbele, wachina wakishaanza kazi hakuna mwendo pole, ni mwendo kasi baada ya kupata amri ya endeleaz mbele.

...Isije kuwa mwendo kama wa dhahabu ya wachukuaji kuchukua 97% na kuiachia nchi 3%....Huu ni wizi wa hali ya juu!!! Tena wa mchana kweupeeeeeee!!!!!
 
Mbunge ndio anawapokea nilidhani wangepokelewa na Mbunge pamoja na mtu wa wizara yenye dhamana ya nishati na madini ama mtu toka NDC! Yote kheri inanikumbusha makala moja niliyoisoma inayosema "From Brettonwoods to China".

Mbunge Filikunjombe kawazidi kete, maana wamegundua hapo hakuna ulaji kama ilivyozoeleka, vinginevyo Filikunjombe angeshapigwa kikumbo muda mrefu tu.
 
...Isije kuwa mwendo kama wa dhahabu ya wachukuaji kuchukua 97% na kuiachia nchi 3%....Huu ni wizi wa hali ya juu!!! Tena wa mchana kweupeeeeeee!!!!!

Jambo hili lilishajadiliwa hapa miezi michache iliyopita, na faida ambayo sisi tutapata ni bora kuliko wachimba madini wengine. Wachina ni bora kuliko hawa wa kutoka mataifa ya magharibi.
 
Nakubaliana na hoja yako, lakini tatizo si wageni wanaoiba utajiri wetu ila viongozi wetu wabinafsi ndio wanaachia mwanya. Hata wewe ukipata nafasi ya kula hutaiachia.

Kama alivyosema Jaji Bomani juzi, ni muhimu kuweka sheria za kunda rasilimali ikiwa ni pamoja na process za awali zifanyike hapa nchini na processed product ndizo ziuzwe nje, hapo kutakuwa na mfumo mzuri wa kiuchumi.
Mkuu wataalam wetu wanayajua yote haya.ndio maana utasikia we need to process our prodce/minerals in order to add value instead of selling raw products! Lakini wapi kola siku mambo yanaishia kwenye makaratasi: Tanzanite ya Tanzania inatoa ajira India kwenye kiwanda.cha kusafisha Tanzanite. Mchanga inasagirishwa kwenda.kusafishwa ughaibuni! Ajira wanapata wao sisi tunalia tu kwamba ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu. kwa nini tusiwalazimishe waweke hivyo viwanda hapa ambapo kina raw materials. Huu ni sawa tu na wakati wa ukoloni wakati tunatumika kulima pamba na tumbaku kwa ajili ya viwanda vya Ulaya!
 
Mbunge Filikunjombe kawazidi kete, maana wamegundua hapo hakuna ulaji kama ilivyozoeleka, vinginevyo Filikunjombe angeshapigwa kikumbo muda mrefu tu.
Hivi huu si ni mradi wa NDC au nachanganya madawa? Mwenyekiti wa NDC si ni mzee wa mabomu mh. (rtd) Chrisant Majiyatanga Mzindakaya? Wakicheza atawalipua!
 
Mzindakaya na "Filikunjombe wako bega kwa bega na huyo huyo Mzindakaya ndiye aliyefanya kazi ya ziada kuwaleta wachina baada ya kuona danadana zisizoisha ndani ya ofisi ya Jairo. NDC ni bomu kwani zaidi ya miaka 20 wanaendela na majaribio huku hakuna hata majaribio ya ndondo za kujengea. Wanakula tu bajeti kila mwaka bila matokeo.
 
..tatizo watu wanafikiri wachina wa leo hii ni kama wale waliojenga Tazara.

..hawa wa sasa hivi wako zaidi kibiashara. they r just as greedy as westners.

..ukizingatia sheria zetu za madini, na aina ya viongozi wanaozisimamia, this is not the right time kwa nchi hii kusaini mkataba wowote ule wa madini.
 
Back
Top Bottom